Kwa haya mambo mawili Serikali imepigwa mweleka

Kwa haya mambo mawili Serikali imepigwa mweleka

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
3,156
Reaction score
3,628
Salamu wanajamvi!

Niende moja kwa moja kwenye mada. Kuna mambo mawili ambayo kwa mtazamo wangu serikali ni kama imepigwa KO! Au unaweza kusema imepigwa mweleka kabisa. La kwanza ni kuhusu ajira kwa vijana. Tangu mwaka 2016 serikali haija ajiri vijana wanao hitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati mpaka mwaka 2021. Ukikusanya takwimu za vijana wenye elimu lakini hawana ajira utachoka! Ni wengi, ni wengi kweli kweli. Ni vijana wachache sana walio some ualimu masomo ya sayansi ndio walio ajiriwa kati ya 2016 mpaka 2021. Ni kama serikali inasema kila mtu atajijua na watoto wake. Serikali haina solution na haitaki kuweka mambo hadharani ili sekta binafsi isaidie.

Eneo jingine ni kuhusu ugonjwa huu mpya kabisa COVID-19. Serikali imefumba macho na kuziba kabisa masikio. Leo nimesoma habari ya kusikitisha sana. Kijana mmoja amewapoteza baba yake, baba yake mkubwa na shangazi yake siku moja kwasababu wote walikuwa na tatizo la kushindwa kupumua! Hospitali zote alizo wapeleka wagonjwa wake zilikuwa hazina ventilators ambazo hazitumiki. TMJ, Hindu mandali na kaigaruki zote hazikuwa na nafasi. Mwisho wagonjwa wakapoteza maisha. Kwa hili pia ni kama serikali inasema Covid -19 itaua lakini haitatuua wote. NO CONCERN AT ALL.

Jamani msikimbilie kuwa viongozi kama mbinu za kupambana na CRISIS hamna! Ajira kwa vijana ni bomu lakini COVID -19 ni BALLISTIC MISSILE YA AINA YAKE.

Nini kifanyike? Kuhusu Covid-19 , kampeni kubwa ifanyike kuhusu kulazimisha watu kuvaa barakoa na kila sehemu kuwekwe maji tiririka na vitakasa mikono. Tuzingatie maelekezo ya WHO na wataalamu wa afya.

Ama kuhusu ajira kwa vijana ni lazima tuongeze juhudi za kukaribisha wawekezaji kutoka kote Duniani kwa masharti nafuu. Serikali iweke mazingira wezeshi kwa ustawi wa sekta binafsi ili zipunguze tatizo la ajira. Serikali iondoe kodi kabisa kwa biashara zinazo anza walau kwa miaka miwili ya kwanza ili ziweze kuimarika.
 
Miundombinu ya barabara, madaraja, reli, Stieglers Gorge na vivuko ndiyo kipaumbele,mengine hayapewi nafasi.Pathetic!
 
Miundombinu ya barabara,madaraja, reli,Stieglers Gorge na vivuko ndiyo kipaumbele,mengine hayapewi nafasi.Pathetic!
Hiyo ndio miradi yenye 10 percent.

Unamzungumziaje ajira wakati hazimpi faida yoyote.

Nakumbuka 2015 wakati anaingia madarakani aliiponda kinyama yaani sheria ya manunuzi mpaka akatunga mpya.

Kilichotokea hiyo sheria imekufa, YEYE NDIYE MTOAJI WA TENDER na MNUNUZI ( Procurer in Chief )
 
The most idiotic statement of the year. Yaani kabisa unataka serikali ilazimishe watu kuvaa barakoa? Ikimaliza hilo unataka ilazimishe nini kingine? 😬😬😬
Watu dhaifu huwa hawana hoja! Hivi hujui kuwa Nchi hii asilimia 70 ni darasa la 3B kama wewe hivyo wanahitaji kulazimishwa baadhi ya mambo ya msingi kama haya? Think twice before you utter your non sense!
 
NYUMONIA KALI ATTACK LEVELS

Level 1 - Inatibika
[emoji117]Mwili kuchoka
[emoji117] Maumivu ya mwili mzima na viungo
[emoji117] Kichwa kuuma & Kizunguzungu

Level 2 - Inatibika
[emoji117]Kukosa hamu ya kula
[emoji117]Kushindwa kunusa harufu
[emoji117]Homa
[emoji117]Kikohozi
[emoji117]Kukosa pumzi (Kupumua kwa shida)

Level 3 - Hatari na ngumu kutibika
[emoji117]Kifua kubana
[emoji117]Makohozi yenye damu au njano nzito
[emoji117]Kushindwa kupumua/Kukosa hewa
[emoji117]Homa kali
[emoji117]Mapafu kujaa maji (Pneumonia)

Tuchukue tahadhari tafadhali
[/color][/color]
 
Nchi zinazojali uhai wa raia wake kuvaa barakoa nk, katika wakati huu dunia ikikabiliwa na COVID, ni kitu cha lazima.
 
Good points lakini hakuna wakukusikia. Nimependa pale uliposema "tusikimbilie uongozi kama hatuna mbinu za kukabiliana na matatizo'...not word to word though.

Iko hivi, huku afrika, hakuna kiongozi aliyekwenda pale kutatua matatizo, wote wanakwenda kutafuta unafuu wa maisha.

In Afrika', siasa ndio biashara/kazi inayolipa zaidi. Ndio maana kubaki madarakani ni project ya muhimu mno kwa vyama vya siasa hapa afrika kuliko uhai wa binadamu.
 
Watu dhaifu huwa hawana hoja! Hivi hujui kuwa Nchi hii asilimia 70 ni darasa la 3B kama wewe hivyo wanahitaji kulazimishwa baadhi ya mambo ya msingi kama haya? Think twice before you utter your non sense!
Hiyo research uliifanyia wapi mkuu?
 
Ni kweli masuala hayo 2 ni mabomu mapigo makubwa kwa CCM. Lkn wanalo tegemeo lao kubwa ktk chaguzi zote zijazo watategemea Tume na dola.
 
Kesho Usaili 08.02 Wilaya Ya Buhigwe
Nafasi Ni Moja Waliotwa Ni Mia Moja Na Hamsini
Mambo Uliyoyasema Ni Kweli Tupu
Watu Tunateseka Sana, Kila Mtu Ameguswa
 
Good points lakini hakuna wakukusikia. Nimependa pale uliposema "tusikimbilie uongozi kama hatuna mbinu za kukabiliana na matatizo'...not word to word though...
Wow! What a school! Truly you made my day and i dare to say YOU ARE A GREAT THINKER OF OUR TIME.
 
Ni kweli masuala hayo 2 ni mabomu mapigo makubwa kwa CCM. Lkn wanalo tegemeo lao kubwa ktk chaguzi zote zijazo watategemea Tume na dola.
Haita wasaidia milele. A day is coming watalia na kusaga meno.
 
NYUMONIA KALI ATTACK LEVELS

Level 1 - Inatibika
[emoji117]Mwili kuchoka
[emoji117] Maumivu ya mwili mzima na viungo
[emoji117] Kichwa kuuma & Kizunguzungu

Level 2 - Inatibika
[emoji117]Kukosa hamu ya kula
[emoji117]Kushindwa kunusa harufu
[emoji117]Homa
[emoji117]Kikohozi
[emoji117]Kukosa pumzi (Kupumua kwa shida)

Level 3 - Hatari na ngumu kutibika
[emoji117]Kifua kubana
[emoji117]Makohozi yenye damu au njano nzito
[emoji117]Kushindwa kupumua/Kukosa hewa
[emoji117]Homa kali
[emoji117]Mapafu kujaa maji (Pneumonia)

Tuchukue tahadhari tafadhali
[/color][/color]

Shukrani mkuu.
 
Watu dhaifu huwa hawana hoja! Hivi hujui kuwa Nchi hii asilimia 70 ni darasa la 3B kama wewe hivyo wanahitaji kulazimishwa baadhi ya mambo ya msingi kama haya? Think twice before you utter your non sense!
Serikali ikiona ni jambo la msingi kuongeza idadi ya watu, itakuwa sahihi ikikulazimisha kupata watoto zaidi?
Unadhani hao asilimia 70 ni mazombie wasiojua kitu wanaopaswa kulazimishwa kama watumwa?
 
Serikali ikiona ni jambo la msingi kuongeza idadi ya watu, itakuwa sahihi ikikulazimisha kupata watoto zaidi?
Unadhani hao asilimia 70 ni mazombie wasiojua kitu wanaopaswa kulazimishwa kama watumwa?
Kwenye mlipuko wa kipindupindu watu hulazimishwa na serikali kuweka mazingira safi na mabwana afya hupita kukagua hadi nyumba za watu!. Unafikiri kwa nini nguvu za dola hutumika kwenye kipindupindu lakini ishindwe kutumika kwenye COVID?
 
Back
Top Bottom