Kwa haya, Nyerere alitawaliwa na ubinafsi

Kwa haya, Nyerere alitawaliwa na ubinafsi

1. Hakuna Rais aliyewekeza katika elimu ya juu zaidi ya Nyerere. Ni kweli, vyuo vikuu vilikuwa vichache, lakini ubora wa elimu ulikuwa ni wa juu sana. Nasikitika kuwa sasa kuna vyuo vikuu vingi vya "kata". Huwezi kulinganisha ubora wa elimu ya wakati wa Nyerere na na ya sasa. Zaidi ya yote alitengeneza ajira kwa ajili ya wahitimu wote. Kwenda Chuo Kikuu, wakati wa Nyerere na hata wakati wa Mwinyi (mpaka 1992), kulikuwa na hadhi yake.

2. Kuhusu katiba kumpa Rais madaraka makubwa: Katiba haikutungwa na Rais, na ndio maana aliwapinga waliopitisha katiba hiyo. Ilikuwa ni kazi ya bunge kutunga katiba nzuri na wala si Nyerere.
 
Binafsi nakushangaa mtoa mada kwa kupoteza muda wako kushawishi jamii juu ya jambo ambalo ni kama dunia nzima inakubaliana kuwa NYERERE alikuwa ni kiongozi wa aina yake kwa maneno na kwa vitendo.kwa sisi tuliosoma enzi za Nyerere kila mtu alitamani awe na elimu ya kweli kama yeye,awe na uwezo wa kupambanua mambo kama yeye,awe mchapakazi kama yeye, awe mwadilifu kama yeye na awe na confidence kama yake. SASA wewe kujua kusoma na kuandika tu unadhani unaweza kuchambua philosophy ya NYERERE, bado kajipange.DUNIA INAMKUBALI NYERERE MWANZO MWISHO.
 
1. Hakuna Rais aliyewekeza katika elimu ya juu zaidi ya Nyerere. Ni kweli, vyuo vikuu vilikuwa vichache, lakini ubora wa elimu ulikuwa ni wa juu sana. Nasikitika kuwa sasa kuna vyuo vikuu vingi vya "kata". Huwezi kulinganisha ubora wa elimu ya wakati wa Nyerere na na ya sasa. Zaidi ya yote alitengeneza ajira kwa ajili ya wahitimu wote. Kwenda Chuo Kikuu, wakati wa Nyerere na hata wakati wa Mwinyi (mpaka 1992), kulikuwa na hadhi yake.

2. Kuhusu katiba kumpa Rais madaraka makubwa: Katiba haikutungwa na Rais, na ndio maana aliwapinga waliopitisha katiba hiyo. Ilikuwa ni kazi ya bunge kutunga katiba nzuri na wala si Nyerere.

Umenena yote sawa kabisa. you deserve the msema kweli award.wakati wa NYERERE ile tu kuchaguliwa kuingia unversity kila mtu alijua kuwa wewe ni kichwa na soon utakuwa mtu mhimu kwa taifa hili. aliwekeza kikweli.
 
Umemgusa mwanaheri watatokwa povu mbaya.Kadikteta kazamani
 
Kuna msemo mmoja huwa unasema kuwa, TUSIWASIMANGE NA KUWASEMA WALIOKWISHKUFA! RIP NYERERE
Huwezi kujenga katiba mpya nzuri kama hujaona makosa ya nyerere. Kosa lake katika kuweka katiba dhaifu na kipengere kisemacho Raisi asishitakiwe akimaliza muda limeleta madhara makali sana kwa watanzania. RIChmone, Rada< Mikataba mibovu haya ni mambo ambayo watu walifanya huku wakijua fika kuwa hawatapelekwa kokote mahakamani

Mazuri aloyofanya kama protective policcy ya kulinda mali na bidhaa zitengenezwamo tanznaia lazima tuliweke katika katiba. maana hili lina manufaa mazuri sana kwa kulinda kazi za watu.

nimekutajia mambo hayo mazuri na mabya katika katiba ya nyerere. Hivyo yale yote mabaya lazima yaanikwe wakati huu wa kujenga katiba mpya ikiwemo kuweka mahakama huru, tume ya uchaguzi iwe huru na baadhi ya vyeo , waziri wa fedha, mwansheria mkuu na waziri wa ulinzi na mabo ya Nje lazima wapigiwe kura Bungeni.

Kenya wameweka katiba yao nzuri sana baada ya kuchinjana na watu kadhaa kupoteza maisha. Sasa na sisi tungojee mpaka matokeo ya uchaguzi mkuu yawanyonge watu, ndipo tuanze kujua umuhimu wa mahakama kuwa huru, Bunge kuwa huru na baadhi ya vyeo kupara kura bungeni? Iam telling you ma bro, as god is my witness. Unless supreme court and election commission are free before 2015 G election,tanzanians will shed blood twice as much as Kenyan suffered.
 
Nyerere alikuwa anajua katiba haijakaa vizuri inampa madaraka makubwa raisi kiasi anaweza kuwa dictator lakini hakutaka kubadilisha katiba ambayo ingewapa madaraka wananchi ili raisi yoyote atakayeingia asiwe dictator. Nyerere kwa kuiacha katiba ambayo yeye mwenyewe alijuwa ni ya kidictator, Nyerere alikuwa DICTATOR na alipenda udictator period (hana sifa za kuitwa baba wa taifa)

Nyerere alijuwa umuhimu wa elimu lakini hakupenda wasomi wawe wengi ndio maana haku invest sana kwenye elimu ya juu. Hili linaelezwa na wengi kuwa wasomi wengi waliokuwepo wakati huo walikuwa wanamchallengi nyerere katika mitazamo na itikadi zake kama akina kambona. Nyerere aliwaogopa wasomi kwa sababu tu ya kupenda madaraka na kutopenda mawazo tofauti na yake ndio maana wakati wake kulikuwa na usemi wa zidumu fikra zake. Nyerere alijua kuwa ili nchi iendelee inahitaji kuwekeza kwenye elimu ili wasomi waje walete mapinduzi kwenye kilimo viwanda na sector nyingine kama madini lakini alijua riski ya kuwa na wasomi wengi wangemchallengi kwenye sera na utawala wake. kwa hiyo alipopima maslahi yake against maslahi ya nchi, akaona afadhali alinde maslahi yake, na ndio maana alitawala miaka 23. yeye mwenyewe alisema madini yasichimbwe mpaka tutakapokuwa na uwezo wa kuchimba wenyewe, mbona huo uwezo hakuujenga mpaka anaondoka. alitegemea nani aje ajenge huo uwezo aweke mamlaka yake mashakani.

bottom line is this: Nyerere naye ni mbinafsi kama wengine ila watu wengi kwa sababu ya uelewa mdogo na kipimo kikubwa cha ubinafsi kinachojulikana na jamii ni kuhodhi mali, nyerere alifanikiwa kupenya kwenye chujio la ubinafsi kwa sababu ya kutojilimbikizia mali. KUTOKUWA MBINAFSI NI ZAIDI YA KUTOJILIMBIKIZIA MALI, kujilimbikizia madaraka ya wewe kuteua mawaziri,wakuu wa majeshi,mikoa,wilaya,mashirika ya uma, nk ni ubinafisi mbaya kuliko wa mali.

Jana wenzetu kenya walikuwa wanawafanyia televised interview watu walioomba nafasi ya IGP na deputies wa polisi. hii ni level nyingine, IGP atakayepita hapa kwenye interview hawezi kumpigia simu eti kamuhanda awakatalie chadema kufanya mikutano. Yaani hadi natamani kuhamia kenya.
ndugu yangu ubarikiwe na mungu akulinde. Maana umeongea vizuri sana na umetoa neno hilo zuri wakati huu wa watanzania tunaandika katiba mpyaa.Kinachotakiwa ni sisi watanzania tujenge katiba mpya yenye nguvu kulikjo Raisi. haya aliyafanya George washington, David Ben Gurion na wafalme wengi wa Ulaya wakati huo wa mapinduzi ya viwanda. Kipengere cha raisi asishitakiwe akimaliza muda lazima kifutwe. Mahakama kuu na Bunge lazima viwe na madaraka sawa na Raisi. Na adhabu ya kifo kwa wezi wa mali ya umma lazima iwemo katiba mpya. Hapo ndipo patakuwa na maana ya kuwa wananchi wanamtawala raisi kikatiba na yeye ni mtekelezaji tuu wa matakwa yetu.

nani aliutaka ujamaa hapa Tanzania na kukubali upuuuzi wa zimio la Arusha? Azimio la Musoma? sisi tulitaka bodi ya mikopo na siyo azimio la musoma.sisi hatukutaka mabepari wachukiwe na kunyanganywa mali zao, sisi tulitaka mabepari wawepo wengi sana ili unemployment rate ipungue. mbona sasa tunawalilia mabepari kuliko hata Kenya?

katiba mpya itakuw ina maana moja tuu, nayo ni kuwa tunapata uhuru kamili wanachi wa Tanznaia baada ya utumwa wa Ujamaa na kujitegemea kututawala vibaya sana sana tena sana.
 
Nyerere alijuwa umuhimu wa elimu lakini hakupenda wasomi wawe wengi ndio maana haku invest sana kwenye elimu ya juu.

....na ndio maana alitawala miaka 23. yeye mwenyewe alisema madini yasichimbwe mpaka tutakapokuwa na uwezo wa kuchimba.

...... Yaani hadi natamani kuhamia kenya.

Chuki binafsi na udini vitakuua shekhe! Mifano yenyewe unayotoa inakinzana kabisa na theme nzima ya uzi wako. Mtanzania yeyote na hata asiye mtanzania lakini anayeijua vizuri Tanzania atakwambia legacy aliyoiacha Baba wa Taifa (I am sorry if this salutation irritates you) Mwl. Nyerere katika masuala ya elimu na uwekezaji kwenye sekta ya elimu.

Nimesoma thread mpaka nimehisi kichefuchefu, ptuuuuuuuuu!!! Hivi ni nani aliyekuzuia kuomba uraia wa Kenya!!!?
 
Umemgusa mwanaheri watatokwa povu mbaya.Kadikteta kazamani

Ni ujinga tu ndio unaokusumbua, hata maana ya mtu kutangazwa kuwa mwenye heri huijui (na kwa "elimu" yako ya mahali fulani haitatokea uijue maana ulishajazwa ujinga kichwani).
 
mwaka 1976, waziri wa michezo wakati huo GEN: Mirisha sarakikya aliwafukuza hapa nchini Kocha wa Yanga tambwe Leya na Nabi Camara. Nani aliyempatia amri waziri huy kuwafukuza makocha hao wa kigeni wakati huo? Waziri anweza kufanya hivyo bila kibali cha raisi? Halafu tukapewa sababu za kitoto sana za kufukuzwa kwao hapa nchini. Eti walikuwa majasusi wa CIA! Yaani mpaka leo, hakuna mtu aliyeelewa sababu za makocha hao kufukuzwa na Sarakikya hapa nchini. wewe hapo unapata picha gani?
 
Nyerere aliamua kung'atuka baada ya kuona nchi imemshinda na hayuko tayari kupokea mawazo mbadala kwa watu wengine kwa kuwa tokea mwanzo alishawaaminisha watu kuwa yeye ndiye mwenye mawazo sahihi hapa tanzania, na wengine wote wanafikiri ushuzi tu. Nina amini kama nyerere angeruhusu demokrasia na kuthamini mawazo ya watu wengine katika inner circle yake ambapo vilikuwepo vichwa kama akina kambona waliokuwa na maono tofauti na mwalimu jinsi ya kuipeleka inchi katika vision nyingine, leo hii pengine tusingekuwa tunaongelea haya matatizo sijui mtu kasign mkataba hata haujui.

Nyerere alichopenda ni kuendelea kutawala tu bila hata kutathimini hizo sera zake kama zinafanyakazi au vipi. Mimi sijui haka kama alikuwa na mipango yenye time frame maana kama una mipango ya muda mfupi,kati na mrefu, miaka 23 ni mingi sana kujua kipi kina work na kipi hakiwork. Dictator yeyote yule ana sifa ya kujenga hofu kwa wanaomzunguka wamuogope ili hata kama wana mawazo tofauti na yeye wasiweze kusema. hii sifa nyerere alikuwa nayo.

Ndio maana hata wakatoliki wamegoma kumpitisha kuwa mwenyeheri wanajua uzaifu wake.
 
Kitendo cha nyerere kukiri hadharani kwamba katiba yetu ni ya kidiktator, na kufumbia macho isirekebishwe vipengere vyote ambavyo vinampa madaraka makubwa raisi kuwa dictator licha ya nafasi zote zilizojitokeza za kufanyia mabadiliko katiba, na yeye nyerere kuendelea kuitumikia katiba hiyo hiyo ya kidictator . NYERERE ALIKUWA DICTATOR. ambaye haelewi hii logic basi hata kuchangia hii thread asichangie.

Wakati akikaribia kuondoka madarakani nyerere alibadilisha katiba kwa kuongeza kifungu kinachoelezea ukomo wa vipindi vya uraisi bila kufanyia marekebisho mengine muhimu ambayo kama yangefanyika hata kama tungepata raisi wa maisha angekuwa kama mfalme wa UK ambapo nafasi zote za utendaji mamlaka za uteuzi zingetoka kwa wananchi. Ila yeye nyerere nongwa yake ni raisi mwingine kutawala kipindi kirefu kama yeye ndio maana akaongeza kipengele hicho tu.

Kwangu mimi nyerere hana tofauti sana na waliomfuata maana hata successor wenzake nao yapo mazuri waliyoyafanya ambayo kama tukiyapima kwenye mizani kila mtu atapata majibu yake kutokana na vipimo anavyotumia. Tena kwangu mimi DHAIFU ndio namuona 'mwenyeheri' kulinganisha maraisi wote waliopita, tatizo lake kubwa ni kuendekeza ushikaji na urafiki sana kwenye utawala wake mpaka anashindwa kuwawajibisha watendaji wazembe, ambalo ni tatizo la kibinadamu.
 
Unachopaswa kujua ni kuwa Nyerere alikuwa anawazidi wasomi kwa nguvu ya hoja,pengine wasomi wetu walikuwa na hoja za msingi lakini katika kuzitetea ndipo alipowabwaga,wengi wao walitawaliwa na tamaa na ubinafsi,wengi wa wanaompinga mwalimu leo hii hoja zao ni za nguvu zikiwa zikiwa zimejikita kwenye udini!
 
Hizi mada za kumponda Nyerere hazina tija na hutolewa na watu ambao sijui wanatumwa au wana ufinyu kweli wa kufikiri, sina hakika.

Nyerere kama binadamu alikuwa na madhaifu yake. Lakini nani anaitilia mashaka nia ya Nyerere zaidi ya Wasomi tulionao? Wewe muanzisha mada, ulitaka Nyerere awasikilize 'the so called wasomi' bila kujali hao wasomi wana mawazo gani?

Leo hii wakati tunalia juu ya UFISADI na ufujaji wa mali yetu, sio hawa WASOMI wanaotusaidia kuimaliza kwa mikataba mibovu?

Yule aliyesaini mkataba wa Richmond na ule wa Radar si wasomi wale? Hawa wanaosaini 3% yetu, 97% ya mwekezaji kwenye madini sio wasomi hawa?

Shida yako unaathiriwa na fikra kwamba Uzalendo haukuwa na nafasi. Si kweli kama Nyerere hakupenda wasomi. Nachojua mimi ni kuwa alizingatia kwanza itikadi za hao wasomi na nia zao. Usomi haumaanishi una nia njema kwa taifa, ndio maana leo wasomi wanaligharimu taifa letu.

Asimame mwanaume hapa JF atende dhambi ya kusema Nyerere angesaini ule mkataba aliosaini Chenge, mmoja tu nimpigie salute. Acheni hizo wakuu, Nyerere amekufa more than a decade ago, mbona ndio kwanza tunazidi kuibiwa?
 
nyerere alikuwa anajua katiba haijakaa vizuri inampa madaraka makubwa raisi kiasi anaweza kuwa dictator lakini hakutaka kubadilisha katiba ambayo ingewapa madaraka wananchi ili raisi yoyote atakayeingia asiwe dictator. Nyerere kwa kuiacha katiba ambayo yeye mwenyewe alijuwa ni ya kidictator, nyerere alikuwa dictator na alipenda udictator period (hana sifa za kuitwa baba wa taifa)

nyerere alijuwa umuhimu wa elimu lakini hakupenda wasomi wawe wengi ndio maana haku invest sana kwenye elimu ya juu. Hili linaelezwa na wengi kuwa wasomi wengi waliokuwepo wakati huo walikuwa wanamchallengi nyerere katika mitazamo na itikadi zake kama akina kambona. Nyerere aliwaogopa wasomi kwa sababu tu ya kupenda madaraka na kutopenda mawazo tofauti na yake ndio maana wakati wake kulikuwa na usemi wa zidumu fikra zake. Nyerere alijua kuwa ili nchi iendelee inahitaji kuwekeza kwenye elimu ili wasomi waje walete mapinduzi kwenye kilimo viwanda na sector nyingine kama madini lakini alijua riski ya kuwa na wasomi wengi wangemchallengi kwenye sera na utawala wake. Kwa hiyo alipopima maslahi yake against maslahi ya nchi, akaona afadhali alinde maslahi yake, na ndio maana alitawala miaka 23. Yeye mwenyewe alisema madini yasichimbwe mpaka tutakapokuwa na uwezo wa kuchimba wenyewe, mbona huo uwezo hakuujenga mpaka anaondoka. Alitegemea nani aje ajenge huo uwezo aweke mamlaka yake mashakani.

Bottom line is this: Nyerere naye ni mbinafsi kama wengine ila watu wengi kwa sababu ya uelewa mdogo na kipimo kikubwa cha ubinafsi kinachojulikana na jamii ni kuhodhi mali, nyerere alifanikiwa kupenya kwenye chujio la ubinafsi kwa sababu ya kutojilimbikizia mali. Kutokuwa mbinafsi ni zaidi ya kutojilimbikizia mali, kujilimbikizia madaraka ya wewe kuteua mawaziri,wakuu wa majeshi,mikoa,wilaya,mashirika ya uma, nk ni ubinafisi mbaya kuliko wa mali.

Jana wenzetu kenya walikuwa wanawafanyia televised interview watu walioomba nafasi ya igp na deputies wa polisi. Hii ni level nyingine, igp atakayepita hapa kwenye interview hawezi kumpigia simu eti kamuhanda awakatalie chadema kufanya mikutano. Yaani hadi natamani kuhamia kenya.
ndugu yangu ninachokiona sana kwako na kinachokusababisha uwe na hoja hizo zisizo kua na msingi juu ya baba wa taifa ni kuwa msikilizaji sana wa radio imaan ya morogoro ambayo siku zote imekua ikiwa mislead wasikilizaji wake sana hasa kwa kueneza chuki juu ya mwalimu,amka kutoka gizani kijana watu wa darasa la pili wasikupeleke wanavyotaka wao kwa misimamo yao mibovu
 
ndugu yangu ubarikiwe na mungu akulinde. Maana umeongea vizuri sana na umetoa neno hilo zuri wakati huu wa watanzania tunaandika katiba mpyaa.Kinachotakiwa ni sisi watanzania tujenge katiba mpya yenye nguvu kulikjo Raisi. haya aliyafanya George washington, David Ben Gurion na wafalme wengi wa Ulaya wakati huo wa mapinduzi ya viwanda. Kipengere cha raisi asishitakiwe akimaliza muda lazima kifutwe. Mahakama kuu na Bunge lazima viwe na madaraka sawa na Raisi. Na adhabu ya kifo kwa wezi wa mali ya umma lazima iwemo katiba mpya. Hapo ndipo patakuwa na maana ya kuwa wananchi wanamtawala raisi kikatiba na yeye ni mtekelezaji tuu wa matakwa yetu.

nani aliutaka ujamaa hapa Tanzania na kukubali upuuuzi wa zimio la Arusha? Azimio la Musoma? sisi tulitaka bodi ya mikopo na siyo azimio la musoma.sisi hatukutaka mabepari wachukiwe na kunyanganywa mali zao, sisi tulitaka mabepari wawepo wengi sana ili unemployment rate ipungue. mbona sasa tunawalilia mabepari kuliko hata Kenya?

katiba mpya itakuw ina maana moja tuu, nayo ni kuwa tunapata uhuru kamili wanachi wa Tanznaia baada ya utumwa wa Ujamaa na kujitegemea kututawala vibaya sana sana tena sana.

Katiba mpya itakuwa na maana zaidi kama ikitamka watu wenye akili zilizodumaa kama hizi watapelekwa jangwani wakachaji akili kwa ugumu wa maisha.
 
Hivi mwanzilishi wa threadi hii unajua maana ya baba wa taifa au unajua kwa nini Nyerere aliitwa baba wa taifa?

Haya assume unachokisema ni kweli pendekeza kiongozi yeyote unayadhani anafaa kuitwa baba wa taifa na utuambie kwa nini.
 
Nadhani huyu aliyeanzisha thread hii amezaliwa kati ya 1980's mawazo ya wasioifahamu vizuri Tanzania hata hivyo nampa hongera sana anaweza kuandika vizuri. Kama unamtu anayeitwa Babu awe ni mzaa mama au mzaa baba kaa nao hawa halafu sikiliza vizuri yale watakayokwambia kumhusu Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere. Acha kujifanya "Mwanaharakati"
 
Back
Top Bottom