Kwa Heri Dar (Mkoani) Karibu Dodoma HQ. Serikali Kuifanya Dodoma kuwa Kitovu Kikuu Cha Uchumi wa Nchi

Kwa Heri Dar (Mkoani) Karibu Dodoma HQ. Serikali Kuifanya Dodoma kuwa Kitovu Kikuu Cha Uchumi wa Nchi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Sasa Dar inaenda kuwa kama Mombasa na Dom kuwa kama Nairobi.

Siku zote anakolala Baba ndiko taulo linatunzwa.Pia soma Jiji la Dodoma Laipiku Dar na Kuwa Kimbilio la Biashara ya Kupangisha Nyumba za Kuishi na Biashara (Frame) | JamiiForums Tanzania Jiji la Dodoma Laipiku Dar na Kuwa Kimbilio la Biashara ya Kupangisha Nyumba za Kuishi na Biashara (Frame)

Kwa Heri watu wa Dar Sasa mtaitwa wa Mkoani na Karibu Dom Makao Makuu.
Serikali imetangaza mkakati wa kuigeuza Dodoma kutoka kuwa makao makuu pekee na kuwa kitovu kikuu cha uchumi, biashara, uwekezaji na usafirishaji nchini, hatua inayotarajiwa kuifanya mji huo kuwa lango muhimu la shughuli za kiuchumi kwa Tanzania na nchi jirani katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/27 bungeni jijini Dodoma leo, Waziri wa Fedha, Dk. Khamis Mussa Omar, amesema nafasi ya kijiografia ya Dodoma katikati ya Tanzania inaipa fursa ya kipekee ya kuwa kitovu cha usafirishaji wa bidhaa, huduma na watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje ya mipaka ya Tanzania. Serikali imeeleza kuwa maendeleo ya mji huo yatachangia kuongeza ushindani wa uchumi wa Taifa na kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Waziri amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya kimkakati inayounganisha Dodoma na mikoa mingine pamoja na nchi jirani, ikiwemo reli ya kisasa ya SGR, barabara, viwanja vya ndege na huduma nyingine muhimu za kiuchumi. Kwa mujibu wa Serikali, uwekezaji huo utaifanya Dodoma kuwa kitovu kikubwa cha usafirishaji wa mizigo na abiria, huku ukichochea ukuaji wa biashara na viwanda katika maeneo ya katikati ya nchi.

View: https://youtu.be/7dsn9E05WP0?si=3rlSU5_mntOQsYiJ
 
My Take
Sasa Dar inaenda kuwa kama Mombasa na Dom kuwa kama Nairobi.

Siku zote anakolala Baba ndiko taulo linatunzwa.Pia soma Jiji la Dodoma Laipiku Dar na Kuwa Kimbilio la Biashara ya Kupangisha Nyumba za Kuishi na Biashara (Frame) | JamiiForums Tanzania Jiji la Dodoma Laipiku Dar na Kuwa Kimbilio la Biashara ya Kupangisha Nyumba za Kuishi na Biashara (Frame)

Kwa Heri watu wa Dar Sasa mtaitwa wa Mkoani na Karibu Dom Makao Makuu.

View: https://www.instagram.com/p/DZcu6x2DH3I/?igsh=MmFxeHkwMnR4eDZm

Bora mtatupunguzia zahma kwa kweli.
 
Mwendazake ni nani? Mimi sio mshabiki wa kitu chochote Wala Sina chama, Wala sio chawa wa kuwekewa bando la mwezi nije kusifia watu mitandaoni kama wewe.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😆😆😆
 
Zamu ya Mbeya yako itafika lini?
Siku Tukipata Rais mwanauchumi ambae anaweza kimkakati kwamba Kila Kanda kijengwe Jiji kuu ambalo litakuwa centre ya Uchumi badala ya kutegemea Dar pekee kama ilivyo Sasa.
 
Back
Top Bottom