Kwa kweli wakenya mmejitahidi sana kwenye Miundombinu ya Usafirishaji, (Majini, ardhini na angani)
Kwa hilo nawapongeza,
Nimekuwa Nairobi mara kadhaa niseme tu Ni jambo jema kuona mnafanya Mambo mazuri kwa ajili ya kila mwananchi,
Rais wa Tanzania JPM ni muumini mzuri wa Miundombinu, amebana vyuma kila angle kuhakikisha anawekeza kwenye Miundombinu,
Natumaini 2025 tutakuwa na Miundombinu yenye ushindani kiasi cha kuinua biashara ndani na nje ya mipaka ya Africa Mashariki,
Pamoja na Tofauti na vijembe vya hapa na pale, Tanzania na Kenya ni ndugu wa Damu,
Ni suala la muda tu nchi za Africa mashariki zitaungana na kuwa nchi moja na ndio itakuwa superpower of Africa,
Wakati huo pia tutakuwa kwenye hatua nzuri za kuunganisha Africa nzima na kuwa jumuia moja yenye Nguvu Duniani.
Mungu abariki watoto wa Africa.