Kwa heshima kabisa Pastor Tony kaa kimya, Unakoelekea unaharibu

Kwa heshima kabisa Pastor Tony kaa kimya, Unakoelekea unaharibu

inspectorbenja

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
657
Reaction score
733
Baada ya mke wa Pastor Tony,kushuhudia ibadani kuwa kuna siku waliishiwa gesi,Pastor Tony akaupuliza mrija,wakapata gesi ya kutumia wiki mbili,nchi ni kama imerindima na kupatwa na taharuki

Wengine wanaona,ni usanii at its maximum point,wengine wanajiuliza maswali ya kufikirisha sana,ambayo haipaswi kuyabeza,mfano mmoja amejaribu kuwaza kama PT ana mikoko ya kufa mtu imejaa parking.Tena ya thamani kubwa sana,anakosa fedha ya gesi kabisa.Lakini kwa nafasi yake kama public figure,si angeagiza tu aletewe gesi na vendor yoyote hata kwa mkopo.Au angemuagiza tu mzee wa kanisa,niletee gesi.Hizo ni tafakuri tu

Ila mimi siwezi kusema PT ni msanii,ninaamini ni mtumiishi wa Mungu,na anafanta kazi ya Mungu.Je hiyo stori ni ya kweli au famba,siwezi nikasemea,ila ninachoamini Mungu huwa anafanya miujiza,ila huo wa PT kwa kweli siwezi kusemea walq sina majibu

Ila ninaona respinse za PT,kwa kweli naona kama amereact kupita kawaida,amekosa stamina ya kuvumilia kudhihakiwa,kukashifiwa na kufedheheshwa.Kwa mtumishi wa Mungu hiyo ni kawaida sana.Anasema mtu akikuambia mchungaji wako kapuliza upepo geai ikajaa,mwambie na wewe mbona unajiuza ili kupata fedha.Common sense yangu inaniambia,hapo kuna kitu hakijakaa sawa kwa mtumishi wa Mungu ambaye amepakwa mafuta na kuitwa kumtumikia Mungu kwa wito mkuu

Mimi nadhani hata asingehangaika kujibu,angepuuza tu na kuendelea na kazi kubwa iliyo mbele yake.

Ni ayo tu,the Awol Diplomat Sympasizer
 
Back
Top Bottom