Kimsingi hapa duniani huwezi fanya uovu halafu usilipie gharama za huo uovu wakati ukiwa hai. Moto anaopitia Gambo kwa sasa ni gharama za uovu alioufanya wakati akiwa RC. Kwa msiojua ni kuwa kuna mambo mengi mabaya hayakufika kwenye media yaliyofanywa na Gambo, Sabaya na Makonda enzi wakiwa viongozi awamu ya 5.
Kwa mfano kwenye ajali ya Lucky Vicent, huyu Gambo aliwatia ndani viongozi wa dini pamoja na watu wengine walioenda moja kwa moja kwenye familia za wahanga kutoa rambirambi. Mstahiki Meya wa sasa Mh Max aliponea chupuchupu kuwa miongoni mwa waliokamatwa. Wakati huo hakuwa kiongozi. Marafiki zake walilala selo kwa amri ya RC.
Uki-connect dots kwa azimio la jana la madiwani kumuomba Makonda agombee ubunge Arusha utaona sio bahati mbaya. Nyuma ya pazia kuna Meya wa jiji la Arusha. Ikumbukwe mtoto wa Meya ni mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha. Meya kajipanga. Pia madiwani wengi walikuwa CHADEMA enzi za JPM ila wakaunga juhudi na kuhamia CCM. Bila kufikiri mara 2 ni kuwa nao wana machungu yao waliyofanyiwa enzi Gambo akiwa RC.
Ninamshauri Gambo awe mtulivu na aachane na habari za ubunge maana atapoteza tu fedha zake. Kipaji chake cha fitina hakitamsadia kitu kwa sasa. Huu muziki wa Meya kwa kushirikiana na RC ni mnene sana hatauweza. Nyuma yao kuna vigogo wengi wa utalii na wafanyabiashara wengi wakubwa. Gambo kasahau yeye ndo alisimamia watu wa bureau de change kuporwa pesa zao?
Soma Pia:

- Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha
- Gambo: Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali ni Mbunge, Makonda anahitaji kuelimishwa
- Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini
- Mrisho Gambo: Nitaenda kuwajibu nini wananchi wa Arusha. Jiji kama Arusha linakosaje stendi?