Kwa hii tabia ya wanawake ku pretend b4 marriagge tufanyaje?

Kwa hii tabia ya wanawake ku pretend b4 marriagge tufanyaje?

Tatizo watu tukiambiwa tuingie kwenye courtship kabla ya ndoa tuna waza kutoana out na kulewa na kungonoka mpaka tunasahau maana halisi ya uchumba.
Trust me ukikaa na mtu vizuri ikupasavyo kwenye uchumba utamjua tu! hata apretend vipi, tabia sugu za mtu zitakuwa zina popup na yeye anazi suppress ukimsoma vizuri utajua tu....
Kwa mfano kama mbeya atajisahau tu siku ataanza kukueleza habari za umbeya..
Kama namchukia ndugu yako siku wakiwa wote utaona tu anabadilika tofauti na anavyokuwa na wewe...
Kama mchoyo do I need to explain? Utaona tu the way anavyobehave na vitu vyake...

Ni kweli kabisa na pia ukae na mtu angalau miaka miwili ndo muoane sa unakuta mtu kapata demu after 6 months anaoa ndo inapokulaga kwao hapo
 
Huwezi kuokota embe chini ya mfenesi.

Kuna shemeji yangu yeye alikuwa na uhusiano na binti mwenye roho mbaya kwa miaka zaidi ya mitano. Na dada wala alikuwa a pretend...kila mtu alikuwa anajua tabia yake.

Ujinga wa huyu binti alikuwa anawachukia saaaana marafiki wa shemeji yangu (jamaa yake)...akiwakuta sebuleni kwa jamaa asalimii anaingi rum straight huku kanuna. Kama kuna watu zaidi ya shemeji yangu ndani..hapiki aoshi vyombo...shemeji yangu anaingia mwenyewe jikoni afu dada anakuja kula huku kanuna. Sikujua ni kwa nini alikuwa hampendi mtu yeyote zaidi ya huyu shemeji yangu...ila kuna habari kuwa dada alikuwa mapepe na watu walikuwa wanakutana nae viwanja na wanaume wengine...sasa nadhani alikuwa anaona wanaleta umbea kwa husband to be.

Mume wangu hakuwahi kumwambia kitu kaka yake kwa kuwa anamjua kuwa ashauriki...ila rafiki zake walishambwambia kuwa ukimwoa huyu binti kwako hatukanyagi. Afu shemeji yangu ni mtu wa watu...ana marafiki wengi na anapendekeka. Kila mtu alikuwa anasikitika why...kwanza jamaa ni bonge la handsome ukilinganisha na binti huyo jeuri.

Cha kusikitisha shemeji alikuja kupata akili ya kumpiga chini huyu binti baada ya kumzalisha na kumtolea mahali na kitcheni party juu.

Hata mama mkwe alisikitika sana kwa kumwacha huyo binti kwa kuwa japo mama mkwe hakumpenda...it was too late kuachana nae baada ya kuzaa na kutoa mahali.

Kwa hiyo kuna wanaokaa na wasichana for years lakini bado wanakuwa blind hawaoni mapungufu yaliyo wazi.
 
ngoma droo tu siku hizi, hata wanamme wana-pretend tu.
 
Kama unakubali kuwa tabia kwa asilimia kubwa inatokana na malezi...ukitaka kujua tabia ya mkeo mtarajiwa chunguza tabia ya mama yake. Fuatilia kwa majirani zao uliza mama mkwe ana tabia gani...simpo

Nakumbuka mama yangu alimkataza kaka yangu aimwoe dada fulani kwa kuwa kwao though kulikuwa mbali kidogo na kwetu tulikuwa tunapajua na mama alikuwa anamjua mama mzaa chema nje ndani...Mama yake huyu mdada alikuwa na sifa ya kumweka mumewe kiganjani; afurukuti; na ni mke wa kati kati ya wake watatu...hivyo mama yangu alikuwa anasema mama wa huyu dada lazima atakuwa keshamfundisha mwanawe ushirikina.Lol. Hivyo kaka akioa nae asubiri kutengenezwa.

Imehusiana vipi na ushirikina na mtu kumuweka mumewe kiganjani? Pia kwa msingi wa kuangalia mawazo ya mama ili kumjua mtoto, wanaume wangeambiwa wasioe kwenu kwa sababu mama yenu anaamini ushirikina ingekuwa sahihi?
 
Inawezekana alishaona familia yenu ina maneno maneno, waroho sana na mna ukorofi na ndio maana alipoolewa amebadilika ili msije mkamtawala. Kuna ukoo zingine ndugu yao akishaoa ukoo mzima unahamia hapo. Mwanamke bila kuwa kauzu mtakuwa hamfiki popote. Kama mtu kabadilika baada ya ndoa hamuhisi tu kama na nyie mnaweza kuwa ni chanzo?
 
Upo???? Nime miss comments zako. Lol.

Imehusiana vipi na ushirikina na mtu kumuweka mumewe kiganjani? Pia kwa msingi wa kuangalia mawazo ya mama ili kumjua mtoto, wanaume wangeambiwa wasioe kwenu kwa sababu mama yenu anaamini ushirikina ingekuwa sahihi?
 
Nachelea kuchangia hapa,unaposema mke wa ndugu yako mchoyo na mbinafsi......

Maana saa nyingine ndugu wa mume mmezoea kupokea, sasa mtu akioa na kuanza kubajeti kila senti ndugu za mume mnamuita mchoyo.......ingawa kuna wanawake wachoyo tu hata kama zipo na kuna shida ukweni hasaidii
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mtu hawezi kushindwa kuendelea eti sababu ya ndugu wa mume. Nina mdogo wangu ameolewa na kijana ambaye ni first born na baba yao amefariki muda si mrefu. Mdogo wangu anaishi na ndugu wa mumewe kibao...na bado ana uwezo kuliko sie tunaoishi kwenye nuclear family. Mungu anazidisha neema na akili ya kutafuta kutokana na challenge mtu alizo nazo maishani.

Jaribu kuchunguza wenye uwezo utaona wanaishi na ndugu kibao. Chakula chakula nini bana kinaishia chooni.
 
Nashindwa nisimame wapi kwenye hii mada..
But matatizo yako kote kote..kuna kabila flani mke akiolewa anakuwa wa wote..yaan hata mashemeji wanataka kumuendesha including mawifi..sasa kama binti hakuyaelewa haya mazingira mapema lazima watamletea swaga za hivi za kusema sio mkarimu ama mchoyo

Kuna mazingira mengine wanawake wenyewe ni wahovyo tu..
Yaan akishaolewa anamfanya mumewake kama asiye na ndugu..
Yaan anataka kujua each and everything na anataka ku'control' hata maamuzi..
My take:Couples wanahitaji long courtship and and pre-marriage counselling
 
Tatizo watu tukiambiwa tuingie kwenye courtship kabla ya ndoa tuna waza kutoana out na kulewa na kungonoka mpaka tunasahau maana halisi ya uchumba.
Trust me ukikaa na mtu vizuri ikupasavyo kwenye uchumba utamjua tu! hata apretend vipi, tabia sugu za mtu zitakuwa zina popup na yeye anazi suppress ukimsoma vizuri utajua tu....
Kwa mfano kama mbeya atajisahau tu siku ataanza kukueleza habari za umbeya..
Kama namchukia ndugu yako siku wakiwa wote utaona tu anabadilika tofauti na anavyokuwa na wewe...
Kama mchoyo do I need to explain? Utaona tu the way anavyobehave na vitu vyake...

Ukweli ndio huu!
 
It is very easy Wala haiitaji saokilojia, mnapenda too much, hamtaki ushauri, mnajidai mnapesa sana utajuaje yote Haya? Mimi wakati namtokea mama watoto pesa Nilikuwa nayo, ila akitaka twende out mana Alikuwa na Kazi Alikuwa analipa yeye, si Katoa wazo? Kama Sina hela, Ila Nyie watotot Wa Siku hizi hata Kama walipwa laki. 4 utataka masifa! Sasa utajuaje Tabia yake? Kuna vitabia via wazungu vizuri lazima tuige!
 
Kuwepo na pre-marriage!

Ataendelea kupretend hata katika hiyo pre-marriage mkuu.
Kukubwa ni kuwa na muda mzuri mrefu wa kuwa na huyo mtarajiwa, tena kwa ukaribu utabaini tu tabia haijifichi.
Tatizo kubwa siku hizi watu wanapendana, 2 months baadae wanatangaza ndoa.
Huwezi jua vizuri tabi yake.
 
Umasikini tu unasumbua binadamu,mtu kishaamua kuoa au kuolewa si inatakiwa kuwapa nafasi wajenge maisha Yao?Sasa ndugu wanatafuta nini?na inasikitisha zaidi unapokuta ndugu wanaotoa maneno hayo wana nguvu na uwezo wa kufanya kazi......
 
  • Thanks
Reactions: LD
Pretending, Pretending, Pretending niliwahi kuingia kwenye huu mkenge wakati fulani hivi......Tangia nimejifunza kutoka kwa huyo Pretender sijawahi danganywa tena. Sitadanganywa tena labda niamue kukubali kudanganywa.

Ukiwa na Mungu utamjua tu mtu anayekuibia....wala huwezi msahau. Kikubwa ni kutulia na kutokuwa na haraka ya NDOA na mtu kabla hujamjua. Mtu mchoyo anajulikana tu, mtu anayependa kupokea kuliko kutoa utamjua tu.

Utaona tu umaskini wa roho yake, mbinafsi, mtu wa changu changu anayejidai anayajua maisha kuliko kawaida...khaaa utamjua tu kwanza anavyokuwa mbaya hasa akiwa MWANAUME ndio kabisaaaaaa.
 
Mtu hawezi kushindwa kuendelea eti sababu ya ndugu wa mume. Nina mdogo wangu ameolewa na kijana ambaye ni first born na baba yao amefariki muda si mrefu. Mdogo wangu anaishi na ndugu wa mumewe kibao...na bado ana uwezo kuliko sie tunaoishi kwenye nuclear family. Mungu anazidisha neema na akili ya kutafuta kutokana na challenge mtu alizo nazo maishani.

Jaribu kuchunguza wenye uwezo utaona wanaishi na ndugu kibao. Chakula chakula nini bana kinaishia chooni.

Wewe Nyumba kubwa ungekuwa jirani hapa ningeku-chum. Umeongea niliyokuwa nafikiria kuyaongea. Watu hawajui kuwa kuna mibaraka mingi katika kuwasaidia ndugu wahitaji na hasa wazazi wako. Katika kuishi kwangu nimeshuhudia watu wanaosaidia wengine wakineemeka kuliko wale wanaokataa kusaidia ndugu zao kwa kisingizio cha kubana matumizi na kuweka savings za baadaye. Kuna siri katika kutoa mbayo nadhani hatujaielewa vyema.
 
Linapokuja suala zima la kuoa...huwa natoka knock out na kichwa kinauma na umri ndio unazidi kusongesha!!
 
Nimeshuhudia mara nyingi sana kwa ndugu ana marafiki zangu wanapoamua kuoa,vile ambavyo tabia halisi ya mwanamke inakuwa imefichwa anapretend kuwa ni mnyenykevu sana,mwenye upendo ila akishaolewa na kuingia ndani ni noma. Nina nduguyangu ambaye baada ya kuoa ndipo tulipotambua kuwa shemeji yetu ni mchoyo ana ubinafsi, m2 wa maneno mengi wafanyakazi wanakimbia -hebu tusaidiane wataalamu wa saikolojia ya tabia je? kuna namna unaweza kutambua kuwa hapa m2 (mtalajiwa) anapretend tu .vilevile wawezaje kujua mwanamke mbinfsi anayepretend kuwa mwema.

Duh....
Japokuwa sijaoa lakini binafsi kuna kitu nafikiria kuhusu ndoa.......
Mimi naamini mwanaume ndo anayeweza kuipeleka ndoa yake mbele au akaivunja vilevile,
Ukiwa mwanaume legelege wa kujifanya unampa nafasi saaana mwanamke katika kuendesha familia yako utakwisha wewe na nduguzo(sorry hapa,najua kuna watu nimewakwaza tayari,lakini ndio ukweli wenyewe huu)......
Nina experience ya kuishi kwa ndugu zangu tofauti tofauti tangia nikiwa darasa la nne hadi namaliza chuo kikuu......nimeyashuhudia mengi sana kwenye familia zaidi ya sita nilizowahi kuishi nazo katika vipindi tofauti tofauti na mahali tofauti tofauti........


ndio mana nasema mwisho wa siku,nimegundua kama mwanaume akilemaa,mwanamke yeyote yule anaweza kuonekana mbaya wakati unaweza kuta ni vitabia vya kuendekezwa tu........

by the way,,kwa maisha niliyopitia,hata kama nisingekuwa kwenye mahusiano na mpenzi wanu huyu....bado naamini ningeweza kuoa mwanamke yeyote na mahali popote na akakaa kwenye mstari tu.............
 
Back
Top Bottom