hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 3,553
- 7,334
Hapana.hiyo maandmano ndiyo shughuli ya maendeleo?
Maandamano sio shughuli ya maendeleo ila ni shughuli inayoweza kuchochea mabadiliko na kuleta fikra chanya kwa viongozi wasiotaka kubadilika na kuleta unafuu kwenye maisha ya mtanzania wa hali ya chini.
Maandamano ni njia ya kuonyesha kwamba wananchi haturidhishwi na utendaji wa kiongozi au na utolewaji wa huduma au haki muongoni mwetu.
Maandamano ni njia ya kuwashinikiza kuwakumbusha na hata kuwalazimisha kwa nguvu viongozi wanaoenda kinyume na katiba na sheria kufuata katiba na sheria.
Ndiyo maana nchi zinazojielewa zote maandamano hayapigwi marufuku kama alivyofanya yule mungu wenu jiwe.
Umeona wafanyabiashara wa kariakoo walivyogoma viongozi wa serikali walikuja kuwasikiliza na kuyajenga na nchi ndiyo inatakiwa iendeshwe hivyo.
Kama hatutabadilisha kitu kwanini mnatumia nguvu kubwa kuzuia maandamano.Hivi mkiachwa mnaandamana hata kila siku mtabadilisha nini?
Mnatumia mpaka jeshi la wananchi kuzuia maandamano kijanja achilia mbali poliCCM.
Kama hatutabadilisha kitu si mtuache.
Haya ni mawazo yako tu.Unato mfano wa watu wapumbavu km wakenya?
Kenya wapo juu yetu kiuchumi kisiasa na hata kielimu.
Mtu aliyekuzidi vitu hivyo katu hawezi kuwa mpumbavu.
Hata wakulima wanaisoma namba kama watanzania wengine.Acheni upumbavu fanyeni kazi, mbona wakulima hawa muda huo wa kijinga nyakati zao za kilimo
Jiwe alivyoharibu kilimo cha korosho mtwara usifikiri wakulima walifurahi.
Ni uoga wetu tu watanzania ndo ulifanya wakae kimya.
Hapa umeamua tu kudanganya.Wakulima ni mfano mzuri wa wachapakazi nchi hii hawana malalamiko ya kipuuzi
Wakulima mpaka sasa hawana soko la uhakika la bidhaa zao na wakiuza wanauza kwa bei ya hasara kupitia madalali bado useme hawalalamiki na ni wachapa kazi.Una matatizo sio bure.
Huu ni ubabe na ni kinyume kabisa cha katiba na sheria.Ingekua enzi ya jiwe angewanyanganya na leseni kabisa,
Ubabe aujawahi kuwa staili nzuri ya kuongoza na mwisho wake uwa ni mbaya sana.
Maandamano kupinga huduma mbovu au maamuzi mabovu ya viongozi sio mambo ya kipuuzi ni mjinga tu ndo anaweza kudhani hivyo.Mambo ya kipuuzi mengine hayawezi kujitokeza.