Kwa hili bado kuna Mtanzania anayehoji PhD ya Waziri Mwakyembe?

Kwa hili bado kuna Mtanzania anayehoji PhD ya Waziri Mwakyembe?

Kwani umeweka nia ya kugombea kile kiti au kuna unaempigia kampeni akinyakue? Hao ndio wanaodukuliwa

Shabiby alidukuliwa Akimtongoza DC mmoja japo hana nia ya kugombea Urais , Mzee akamchana

Waziri wa Afya alidukuliwa akigombana na Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mzee akasema akaamua kuwaweka pamoja


Mzee Baba akiwa free anasema tu em nipeni message au audio za fulan nisikilize

Ukubwa raha sana

Ukiwa Mkubwa ukifanya lolote lenye ukakasi Wapambe wako wnakutetea wanasema ‘... Kafanya kwa nia njema kwa maslahi ya Taifa ...’
 
Shabiby alidukuliwa Akimtongoza DC mmoja japo hana nia ya kugombea Urais , Mzee akamchana

Waziri wa Afya alidukuliwa akigombana na Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mzee akasema akaamua kuwaweka pamoja


Mzee Baba akiwa free anasema tu em nipeni message au audio za fulan nisikilize

Ukubwa raha sana
Dah! Amakweli wakubwa wanafaidi! But seriously its not fair. The same thing akifanya raia ni criminal offence.....serious offence

Hata kama katiba au sheria ya usalama wa taifa inatoa mamlaka kwa watu fulani ku access mawasiliano ya faragha ya watu wengine nadhani mamlaka hayo yana mipaka ikiwa ni aina ya mazungumzo ya kudukua na na pili ni kutokuyaweka hadharani kama ilivyofanyika kwenye case mbili ulizozitaja
 
Wasomi wa Kiafrika walioelimika kweli kweli wapo duniani. Hawa mnaowaona bongo kama wakina Kabudi na Mwakyembe ni wale ambao PHd zao ni za kuunga unga ndio maana hawawezi kutendea haki huo usomi ambao kimsingi hawana.
 
Yeye kama Waziri tokea Mchakato mzima wa Uwekezaji wa Klabu ya Simba alikuwepo, alihusishwa na natambua huku nikiwa na uhakika kuwa mara nyingi kama Waziri alikuwa anakuwa Consulted na akawa anabariki yaliyokuwa yakiendelea na mpaka Siku ya mwisho ya Maamuzi ambayo yalifanywa na Wanachama huku Yeye akiwa Mgeni rasmi alibariki Uwekezaji wa Mo Dewji wa 49% ndani ya Simba SC hatimaye leo tena huyo huyo Waziri anageuka na kutaka kuleta Mtafaruku na matatizo ndani ya Klabu ya Simba.

Kama kuna Watanzania ambao wanaziaibisha PhD's walizonazo Wasomi wengine basi ni huyu Waziri Mwakyembe na nadhani kama anaweza atuombe Radhi upesi wana Simba SC kwani Kauli yake imetuchanganya na imetukwaza mno tu. Na kwa upande wa Serikali watambue kuwa kama kuna Timu ambazo zinaamua pia Rais wa nchi hii awe nani basi ni Wapenzi na Wanachama wa hii Timu hivyo kuna uwezekano mkubwa Kauli hii ya Kipumbavu ya Waziri Mwakyembe ikawa na Athari kubwa Kwao Kisiasa na wakajuta huku wakiwa hawaamini kitakachotokea.

Hivi ni kwanini Serikali ya Awamu hii tokea Kutekwa na Kupatikana kwa Mwekezaji wa Simba SC Mo Dewji mmeanza Kuonyesha Chuki zenu za wazi wazi Kwake huku mkiwakumbatia kwa ukaribu mno Maadui zake wa Kibiashara? Mo Dewji wa Watu amewakoseeni nini? Hivi hizi Juhudi zake anazozifanya kwa Simba SC nyie hamuoni kuwa anailetea nchi Sifa lakini pia anaunda Fursa kadhaa za Kiajira kwa Watanzania hivyo Kuwapunguzieni mzigo mkubwa wa Tatizo la Ajira ambalo linawashindeni kila Siku hapa nchini?

Na kama mnajua fika kuwa sasa hamumpendi tena Mo Dewji labda mna Hasira nae pengine kwakuwa amekataa Kuchangia Kitu fulani Kwenu huku mzikidi Kumfilsi Mali zake huko Tanga na Kumkomoa kwa hapa na pale kwanini msimwambie tu wazi wazi bila Unafiki kuwa hamumtaki ili awaachie Simba SC hao Wafanyabishara wenu ambao huwa mnawatisha hadi wanawalambeni Miguu ili wawasaidie kwa Pesa ili muendelee Kutawala na kuwa Madarakani?

Kwa mfano kwa aina ya Uwekezaji mkubwa hasa wa Kiufadhili ambao tayari Mo Dewji ameshaanza Kuuweka ndani ya Simba SC leo hii akiamua Kujitoa na Kuachana na Simba SC nyie ( Serikali ) hasa kupitia Waziri Mwakyembe mtakuwa na uwezo wa Kulipa Mishahara Wachezaji na Watendaji wengine wa Simba SC na Kuendesha Operations za Klabu? Kwanini mnapenda Kuliangalia Jambo hili kwa upeo Wenu mfupi mlionao japo wengi wenu mnajifanya mna PhD's wakati kumbe ni za hovyo hovyo, Feki na bado mnaonyesha tu Upumbavu wenu?

Mwisho kabisa naomba leo niwaambie wana Simba SC japo najua wengi wenu mlikuwa hamjui kwamba kama kuna Jasusi ambaye anatumika na Waziri husika ( kwa Uratibu mzima wa Serikali ) ili Kuipeleleza Simba SC na kuhakikisha kuwa Mwekezaji Mo Dewji anasumbuliwa hadi akate Tamaa kuwa Mwekezaji wa Simba SC ni Ndugu Ismail Aden Rage na labda niwaombe tu wana Simba hasa Mwekezaji, Mwenyekiti na Bodi nzima ya Wadhamini na Uongozi mzima wa Simba SC wawe nae makini sana na ikiwezekana wamuepuke kwani Ismail Aden Rage ndiyo Kirusi katika Kufanikisha Mo Dewji anafanikiwa na ndiyo huyu huyu yupo nyuma ya Mzee Kilomoni ili hatimaye wote hawa wakishafanikiwa basi Tajiri Mmoja mkubwa nchini Tanzania ( aliyefiwa na Watumishi wake hivi karibuni ) anayewatumia ( anayependwa pia na Serikali ) mwenye Kuitaka sana Simba SC afanikiwe na Wao waule.

Waziri Mwakyembe awe makini na asije Kutulaumu wana Simba SC kama na Sisi tukisema liwalo na liwe Kwake. Tumemchoka!
Si mlikuwa mnafurahi alipokuwa anadhalilishwa Yusuph Manji? sasa zamu yenu,jambo la kujifunza ni kwamba usifurahie mwenzio anapopata shida coz hujui kesho itakuwaje
 
Kwel.ccm inaharibu uwezo wa kufikiria wa ma phd wetu. Ilianza na yule propesa sa hiv kwishiney na wengine wengi na sasa hiv ni zamu ya huyu. Kaa mbali na imani za watu tutakuchukia wewe na ccm lako. Sisi tunataka.maendeleo ya mpira sio blah blah za asilimia. Kwam hata akichukia hisa zote kama timu inaiwakilisha nchi vzr ninyi mnashida gani? Hawa watu vipi na ikitokea mo amemwaga unga hatutawaelewa. Msitugombanishe na rais wetu tukaanza kumchukia kwa ujinga ujinga.
 
Hatuwezi kumpa timu hivi hivi kienyejically. Lazima "tule" kwanza.

Kwani Mo ni nani hata asituone wazee?
Imeendeshwa na wanachama wazalendo miaka mingi sana ww umepata nini? Au timu imefikia wapi? Tuwe na soni basi tuache mpira ujiendeshe wenyewe siasa kwenye mpira haiwezi kutufikisha mahali
 
Imeendeshwa na wanachama wazalendo miaka mingi sana ww umepata nini? Au timu imefikia wapi? Tuwe na soni basi tuache mpira ujiendeshe wenyewe siasa kwenye mpira haiwezi kutufikisha mahali
Hakuna kijiji kisicho na wazee
 
Back
Top Bottom