Kwa hili DC Maswa, Dkt. Vicent Naano unastahili pongezi

Kwa hili DC Maswa, Dkt. Vicent Naano unastahili pongezi

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Kitendo cha Serikali ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kukaa meza moja na wananchi wanne wa kijiji cha Iyogelo Kata ya Binza wanaodai fidia baada ya sehemu ya maeneo yao ya ardhi kutwaliwa na Wizara ya Maji kupitia Bonde la Ziwa Victoria kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la maji katika kijiji hicho kwenye kitongoji cha Bugarama.

Kwa uamuzi wa Mkuu wa wilaya ya Maswa,Dkt Vicent Naano kuamua kukaa na waathirika hao na kupata ukweli juu ya malalamiko yao na kuwaagiza waandike barua ili tathimini iweze kufanyika na walipwe fidia tofauti na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Kata hiyo kuwa maeneo hayo yalitolewa bure bila hata kuwepo kwa makubaliano yoyote ya kimaandishi,

Kwa uamuzi huo unastahili pongezi kwa kuwasikiliza na kuwasaidia wananchi hao ambao walitaka kupokonywa haki yao na baadhi ya viongozi wa Kata hiyo wenye maslahi binafsi.

Wananchi hao Mwita Jilala Hinda,Lwenge Doma Malale, Mahona John Mathias na Gwisu Jilala Hinda ambao ndiyo waathirika sasa wanakwenda kupata haki yao.

Hivyo nikuombe Dc Maswa, Dkt. Naano sasa una mwezi mmoja tangu uhamie wilaya ya Maswa ukitokea wilaya ya Bunda jitahidi sana kuyafanyia uchunguzi mambo yote unayoelezwa na walio chini yako kwani kwa wilaya ya Maswa majungu, chuki na fitina zipo za kutosha.
 
Back
Top Bottom