Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 55
Jamani we don't need external management kwani hata watanzania wanaweza kuendesha mashirika yetu sema wameweka mbele matumbo yao na hakuna anayewakemea.
Statement yako ni nzuri na umemaliza kwa kusisitiza kuwa we need some new people so that we can refresh our minds, that's external management team. Kwa hali ilivyo katika uendeshaji wa ATCL tunahitaji watu wengine kabisa wenye utaalam na kuelewa current aviation economic affairs arround the world.
ATCL inahitaji wataalam ambao watafanya utafiti wa kina na wakutosha juu ya muundo na uendeshaji wake.
ATCL inahitaji kutengeneza business strategies za kweli na kuanisha jinsi ya kuzitekeleza.
Mapungufu ya kiutendaji ndani ya ATCL hayatoi uwezo wa kutosha kwa watendaji wake kuweza kufanya hayo niliyoyaeleza hapo juu.
Nitatoa mfano mmoja, Kumekuwa na Busines Plan ambayo ndiyo Uongozi wa ATCL imeishikilia mkononi kwamba ndiyo dira yao. Hiyo Business Plan ni defective kwa maana hailengi kuifanya ATCL ifanye kazi zake na kutimiza malengo yanayotakiwa. Aidha, Business Plan imeandaliwa kama 'cover' ya uongozi kuonesha kuwa something kinaendelea lakini ukweli hakuna uwezekano wa kuitekeleza, haitekelezeki.
Namna hii ya Business plan ni ushahidi wa dhahiri ni namna gani wahusika wanaidanganya serikali. Wanafanya hivyo kwa kujua kabisa serikali haina uwezo wa kufuatilia na ku-control activities zinazoendelea ndani ya ATCL. Mfano mdogo wa kudhihirisha haya ninayoyasema ni pale ATCL walipoambiwa warekebishe masuala kadhaa na Civil Aviation Authority, lakini wakaa bila ya kutimiza yote kwa mwaka mzima hadi walipofungiwa na kuyatimiza kwa muda wa week mbili.
Udanganyifu huu kwa serikali ndiyo unatumika wa aina ile ile ya SAA walivyoidanya serikali kwa kuandika Business Plan ya kuchukulia ATCL wakati wakijua kabisa kuwa Business Plan hiyo haitekelezeki.
Mimi binafsi ninaamini kuwa kujipanga ni muhimu, lakini tunaanzia wapi kujipanga au tunajipanga namna gani.
Nikukumbushe, hata Football Association ya Uingereza ilipoona kuwa kiwango cha kumeneji timu ya taifa kimefikia ukomo kwa wazalendo, waliaamua kutoka nje na ku-refresh kwa kuajiri Meneja wa Timi ya taifa mgeni Bw. Erikson.
Na sisi hapa tulipofika tunahitaji kubadilsha mambo kabisa ndani ya ATCL ikiwa ni panoja na utamaduni wa kiutendaji ili iwe rahisi kuchukua fursa hizo kujenga uwezo wa wananchi wetu.
Nilishatoa maoni yangu mara nyingi kupitia hapa JF na kwingineko kuwa we need urgently team ya wataalam wa Aviation ili kuweza kuinasua ATCL hapo ilipo kwa sasa. Kuipa fedha ATCL pekee haitoshi, tunataka kuona fedha hiyo inaendana sambamba na dhamira halisi ya kuiondoa ATCL katika utegemezi wa serikali.
I believe kauli ya Mh. Rais haitatumiwa vibaya kwa maana ya watendaji kuacha kuangalia masuala ya msingi na badala yake kutenda visivyo kwa kisingizio kuwa tunatimiza amri ya Rais. Vilevile, iko haja kwa watendaji, hasa katika wizara, toka Waziri na washauri wake wote wachukue nafasi hii kujipima uwezo katika kutatua matatizo ya wananchi. Haieleweki vizuri tatizo la ATCL lilimekuwepo kwa muda sasa halijatolewa ufumbuzi wowote hadi Rais aingile kati na kuelekeza nini cha kufanya. Hili la ATCL limekuwa wazi na watu wengi wameliona mmeshindwa kulitolea maamuzi, je, shida nyingine za wananchi huko Newala au Muleba inakuwaje?
Nilikuwa kwenye shirika moja la serikali wakati linakuwa restructured wageni wailokuja hawakuongeza chochote zaidi ya kucontrol expenditure na kurestracture operating and administrative costs basi and what happened shirika lilianza kutengeneza faida kutoka kwenye hasara ndani ya miaka 2 tu.
Ni kweli watendaji makini siku zote wanaangalia ni jinsi gani watadhibiti matumizi, kupunguza cost na kuongeza mapato. Hizi ndiyo ABC za kufanya biashara. Kama menejimenti haifanyi hayo basi haiwezi kuwaridhisha shareholders wake kwani thamani ya hisa hupungua na uwezekano na uwezekano wa kupata gawio zuri haupo.
Kazi kubwa ya menejimenti ni kuhakikisha kuwa inalinda maslahi ya mwenye mali kwa kubuni na kutekeleza yale yote ambayo yanatarajiwa na mmiliki. Kinyume cha hapo kama mafanikio hayakupatikana pamoja na maelezo mazuri waungwana hutoa nafasi kwa mtu mwingine aweze kufanya kazi ile. Na kama kweli watendaji wakuu wa ATCL wapo pale kwa manufaa ya watanzania wote basi hawana budi kufikiria mara mbili uwepo wao, kinyume cha hapo ina maana wanaelewa ni nini kinachowaweka hapo.
Tunakula sana tunajisahau kuwa ni mali za watanzania wote tunageuza kuwa miradi binafsi, hiki ndicho tunachotakiwa kukiondoa kwenye mashirika ya umma. ATCL imeliwa tunaiona na tumepiga kelele lakini hawakujali hata kidogo na wanapanga kuwapa mapesa zaidi waliokula ya kwanza ili wale zaidi.
tunahitaji damu mpya kwenye management ya mashirika yetu jamani nothing else.
-----------------------------------------------------------------