XII Tz
JF-Expert Member
- Aug 16, 2020
- 4,345
- 7,076
Habari wakuu
Clatous chota chama ameifanyia simba makubwa sana kwa misimu kadhaa nyuma ila imefika wakati simba tunapaswa kuachana nae na kuangalia maisha mengine.
Yanga waliachana na Saido ntibazonkiza, Feisal salum, Yannick Bangala, Djuma shaban wote hao wakiwa muhimu sana kwenye kikosi chao na kufanikiwa kupata the right replacement na ndani ya muda mfupi hakuna anaye wakumbuka.
Manchester city ya pep Guardiola, karibia kila msimu wanaachana na wachezaji wao wenye majina makubwa na kuleta damu changa zenye njaa ya mafanikio na kuipambania klabu, Joao cancelo alipoleta u-star alipigwa chini na pep immediately saivi yupo Barcelona, ameachana na Mahrez na Gundogan akaleta madogo akina Jeremy Doku na wanakichafua balaa.
Chama kwa umri wake ameshafika mwisho hana kipya anaweza kukupa, njaa ya mafanikio hana tena, anacheza ilimradi tu, na bila kusahau chama ni the most influential player pale simba ana nguvu kubwa ya ushawishi, yeye ndiye kinara wa kuanzisha vimigomo baridi ndani ya klabu na kushawishi wachezaji wenzao kucheza chini ya kiwango ndo maana timu imekuwa haieleweki.
Mfano mzuri ni mechi ya ufunguzi ya AFL dhidi ya Al ahly kwa mkapa, simba tulipiga mpira mwingi sana hadi ukawa unamwagika fighting spirit ya wachezaji ilikuwa juu mno na karibia kila aliyepewa nafasi kwenye ile mechi aliuwasha. Yote ni kwasababu ile mechi ilikuwa na attention kubwa karibia duniani kote hivyo wachezaji walitaka kutumia ile mechi kujiweka sokoni.
Baada ya hapo wote tunafahamu kilichofuatia, tulikandika Hamsa na ntani, na timu ilicheza kama walevi wa gongo, hawaeleweki. Ni hatari sana kuwa na wachezaji wenye majina makubwa na kujiona wako juu ya timu kama chama, tukiataka ku-revive simba yetu inapaswa tuachane na Chama, Aishi manula, Bocco etc . Hawa ndo wachochezi wa migomo ndani ya klabu na kushawishi wachezaji wenzao wacheze chini ya kiwango ili kuwakomoa viongozi.
Simba haipaswi kujali kwamba atakwenda upande wa pili au la muhimu zaidi ni timu, inatupasa kufanya maamuzi magumu. La sivyo tutaendelea kuimba wimbo huo huo daily kwamba sajili mbovu kumbe kuna watu wachache wana tuhujumu na mwisho wa siku tunaoumia ni sisi mashabiki.
Tukiendelea kubaki na hawa wapuuzi tutafukuza sana makocha na hata huyu Benchika ni swala la muda tu ataanza kuonekana hafai sababu mwisho wa siku itategemea na willingness ya mchezaji kutekeleza maelekezo ya mwalimu uwanjani sasa kama kuna migomo baridi na kuambizana kucheza chini ya kiwango unadhani nini kitatokea?.
Narudia tena kwa msisitizo tusipofanya maamuzi magumu tutegemee maumivu tu maana utopolo makombe watanyanyua hadi mikono iwaume. Na tutarajie maparedi ya kila rangi.
Nguvu moja [emoji881]