Kwa hili la chama simba yatupasa kufanya maamuzi magumu

XII Tz

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
4,345
Reaction score
7,076
Habari wakuu

Clatous chota chama ameifanyia simba makubwa sana kwa misimu kadhaa nyuma ila imefika wakati simba tunapaswa kuachana nae na kuangalia maisha mengine.

Yanga waliachana na Saido ntibazonkiza, Feisal salum, Yannick Bangala, Djuma shaban wote hao wakiwa muhimu sana kwenye kikosi chao na kufanikiwa kupata the right replacement na ndani ya muda mfupi hakuna anaye wakumbuka.

Manchester city ya pep Guardiola, karibia kila msimu wanaachana na wachezaji wao wenye majina makubwa na kuleta damu changa zenye njaa ya mafanikio na kuipambania klabu, Joao cancelo alipoleta u-star alipigwa chini na pep immediately saivi yupo Barcelona, ameachana na Mahrez na Gundogan akaleta madogo akina Jeremy Doku na wanakichafua balaa.

Chama kwa umri wake ameshafika mwisho hana kipya anaweza kukupa, njaa ya mafanikio hana tena, anacheza ilimradi tu, na bila kusahau chama ni the most influential player pale simba ana nguvu kubwa ya ushawishi, yeye ndiye kinara wa kuanzisha vimigomo baridi ndani ya klabu na kushawishi wachezaji wenzao kucheza chini ya kiwango ndo maana timu imekuwa haieleweki.

Mfano mzuri ni mechi ya ufunguzi ya AFL dhidi ya Al ahly kwa mkapa, simba tulipiga mpira mwingi sana hadi ukawa unamwagika fighting spirit ya wachezaji ilikuwa juu mno na karibia kila aliyepewa nafasi kwenye ile mechi aliuwasha. Yote ni kwasababu ile mechi ilikuwa na attention kubwa karibia duniani kote hivyo wachezaji walitaka kutumia ile mechi kujiweka sokoni.

Baada ya hapo wote tunafahamu kilichofuatia, tulikandika Hamsa na ntani, na timu ilicheza kama walevi wa gongo, hawaeleweki. Ni hatari sana kuwa na wachezaji wenye majina makubwa na kujiona wako juu ya timu kama chama, tukiataka ku-revive simba yetu inapaswa tuachane na Chama, Aishi manula, Bocco etc . Hawa ndo wachochezi wa migomo ndani ya klabu na kushawishi wachezaji wenzao wacheze chini ya kiwango ili kuwakomoa viongozi.

Simba haipaswi kujali kwamba atakwenda upande wa pili au la muhimu zaidi ni timu, inatupasa kufanya maamuzi magumu. La sivyo tutaendelea kuimba wimbo huo huo daily kwamba sajili mbovu kumbe kuna watu wachache wana tuhujumu na mwisho wa siku tunaoumia ni sisi mashabiki.

Tukiendelea kubaki na hawa wapuuzi tutafukuza sana makocha na hata huyu Benchika ni swala la muda tu ataanza kuonekana hafai sababu mwisho wa siku itategemea na willingness ya mchezaji kutekeleza maelekezo ya mwalimu uwanjani sasa kama kuna migomo baridi na kuambizana kucheza chini ya kiwango unadhani nini kitatokea?.

Narudia tena kwa msisitizo tusipofanya maamuzi magumu tutegemee maumivu tu maana utopolo makombe watanyanyua hadi mikono iwaume. Na tutarajie maparedi ya kila rangi.

Nguvu moja [emoji881]
 
Kati ya wachezaji ambao siwakubali ni chama na manula.
Waondoke tu
Upo sahihi mkuu, Manula huwajibika uwanjani pale anapopaswa kuwajibika tu, anapoona kosa sio lake hawezi kuwajibika ataacha tu goli liingie ili badae watu waseme tu kwamba kipa hana makosa pale, japokuwa angeweza kutumia uwezo wake kufanya jambo aokoe timu kama wafanyavyo diarra na hata kipa mpya wa simba Ayubu.
 
Chama bado ana mchango mkubwa Simba, tusikimbilie kuaminishana kuwa kila kitu ni uhujumu wawachezaji mda mwingine bimadam tunateleza maana ni hulka za kibinadam pia. Mi naamini katika uwezo wa chama na naiona nafasi ya chama bado
Chama hataki tena kubakia simba, alishapata timu tangu mwanzoni mwa msimu hivyo hachezi tena kwa kujituma na pia kumbuka ni the most influential player hivyo ana shawishi wachezaji wengine pia kucheza chini ya kiwango na vimigomo vya hapa na pale.

Yanga waliachana na Saido, bangala, fei wakiwa muhimu sana kwenye timu yao.
 
Hili suala la Chama lina pande mbili. Kuna wanaotaka Chama abakie, hasa mashabiki wa simba ambao wanakumbuka historia ya simba na makubwa ambayo chama amefanya kwa Simba toka enzi za Uchebe na umuhimu wake wa kutoa assist na kufunga magoli kwenye mechi muhimu na mechi zenye historia kubwa kwa Simba. Na wengine wanataka chama atoke hao wamejigawa aina mbili
1. Mashabiki wa Simba ambao wako tayari kwa mabadiliko kutokana na mfumo mpya wa kocha Benchika.

2. Mashabiki wa Yanga ambao wanaojifanya mashabiki wa Simba na wanachochea chama atoke. Ili Simba iwe dhaifu au Yanga wamsajili Chama.
 
Habari wakuu

Clatous chota chama ameifanyia simba makubwa sana kwa misimu kadhaa nyuma ila imefika wakati simba tunapaswa kuachana nae na kuangalia maisha mengine.

Yanga waliachana na Saido ntibazonkiza, Feisal salum, Yannick Bangala, Djuma shaban wote hao wakiwa muhimu sana kwenye kikosi chao na kufanikiwa kupata the right replacement na ndani ya muda mfupi hakuna anaye wakumbuka.

Manchester city ya pep Guardiola, karibia kila msimu wanaachana na wachezaji wao wenye majina makubwa na kuleta damu changa zenye njaa ya mafanikio na kuipambania klabu, Joao cancelo alipoleta u-star alipigwa chini na pep immediately saivi yupo Barcelona, ameachana na Mahrez na Gundogan akaleta madogo akina Jeremy Doku na wanakichafua balaa.

Chama kwa umri wake ameshafika mwisho hana kipya anaweza kukupa, njaa ya mafanikio hana tena, anacheza ilimradi tu, na bila kusahau chama ni the most influential player pale simba ana nguvu kubwa ya ushawishi, yeye ndiye kinara wa kuanzisha vimigomo baridi ndani ya klabu na kushawishi wachezaji wenzao kucheza chini ya kiwango ndo maana timu imekuwa haieleweki.

Mfano mzuri ni mechi ya ufunguzi ya AFL dhidi ya Al ahly kwa mkapa, simba tulipiga mpira mwingi sana hadi ukawa unamwagika fighting spirit ya wachezaji ilikuwa juu mno na karibia kila aliyepewa nafasi kwenye ile mechi aliuwasha. Yote ni kwasababu ile mechi ilikuwa na attention kubwa karibia duniani kote hivyo wachezaji walitaka kutumia ile mechi kujiweka sokoni.

Baada ya hapo wote tunafahamu kilichofuatia, tulikandika Hamsa na ntani, na timu ilicheza kama walevi wa gongo, hawaeleweki. Ni hatari sana kuwa na wachezaji wenye majina makubwa na kujiona wako juu ya timu kama chama, tukiataka ku-revive simba yetu inapaswa tuachane na Chama, Aishi manula, Bocco etc . Hawa ndo wachochezi wa migomo ndani ya klabu na kushawishi wachezaji wenzao wacheze chini ya kiwango ili kuwakomoa viongozi.

Simba haipaswi kujali kwamba atakwenda upande wa pili au la muhimu zaidi ni timu, inatupasa kufanya maamuzi magumu. La sivyo tutaendelea kuimba wimbo huo huo daily kwamba sajili mbovu kumbe kuna watu wachache wana tuhujumu na mwisho wa siku tunaoumia ni sisi mashabiki.

Tukiendelea kubaki na hawa wapuuzi tutafukuza sana makocha na hata huyu Benchika ni swala la muda tu ataanza kuonekana hafai sababu mwisho wa siku itategemea na willingness ya mchezaji kutekeleza maelekezo ya mwalimu uwanjani sasa kama kuna migomo baridi na kuambizana kucheza chini ya kiwango unadhani nini kitatokea?.

Narudia tena kwa msisitizo tusipofanya maamuzi magumu tutegemee maumivu tu maana utopolo makombe watanyanyua hadi mikono iwaume. Na tutarajie maparedi ya kila rangi.

Nguvu moja [emoji881]
Upo sahihi tutafute mbadala wake hapo mwakani maana muda wake upo ukingoni.
 
Hili suala la Chama lina pande mbili. Kuna wanaotaka Chama abakie, hasa mashabiki wa simba ambao wanakumbuka historia ya simba na makubwa ambayo chama amefanya kwa Simba toka enzi za Uchebe na umuhimu wake wa kutoa assist na kufunga magoli kwenye mechi muhimu na mechi zenye historia kubwa kwa Simba. Na wengine wanataka chama atoke hao wamejigawa aina mbili
1. Mashabiki wa Simba ambao wako tayari kwa mabadiliko kutokana na mfumo mpya wa kocha Benchika.

2. Mashabiki wa Yanga ambao wanaojifanya mashabiki wa Simba na wanachochea chama atoke. Ili Simba iwe dhaifu au Yanga wamsajili Chama.
Nasimama na mashabiki wa simba ambao wapo tayari kwaajiri ya mabadiliko huyo chama hata kama atasajiliwa na yanga na aende tu sio mara ya kwanza mchezaji kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu.
 
Upo sahihi tutafute mbadala wake hapo mwakani maana muda wake upo ukingoni.
simba inapaswa kufumwa upya bila ya uwepo wa hicho kiumbe, tunahitaji damu changa zenye njaa ya mafanikio, hana jipya ameshafika mwisho.
 
Nasimama na mashabiki wa simba ambao wapo tayari kwaajiri ya mabadiliko huyo chama hata kama atasajiliwa na yanga na aende tu sio mara ya kwanza mchezaji kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu.
Kuna watu wanatamani wakupige wakupasue. Hasa wale simba Lialia wanaompenda Chama 🤣🤣🤣.

Au wewe ni yanga unajifanya mwanasimba 🤣 halafu unatetea chama atoke 🤣🤣🤣
 
Naona chama kaanza kupewa jina baya kama mbwa anavyofanywa, anapewa jina baya ili apigwe vizuri
 
Kuna watu wanatamani wakupige wakupasue. Hasa wale simba Lialia wanaompenda Chama [emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Au wewe ni yanga unajifanya mwanasimba [emoji1787] halafu unatetea chama atoke [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mimi ni simba damu mkuu, angalia hata post zangu za nyuma, ila kama Simba tunapaswa kufuma timu yetu upya hari ya upambanaji irudi na pia iwe tishio kote barani afrika kama ilivyokuwa zamani. Tukubali zama za hicho kiumbe zimefika mwisho ata Real Madrid walikuwa na Cristiano ronaldo na sasa wapo akina Vini na Rodrygo
 
Back
Top Bottom