Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mimi ni mmoja wa watu nisioridhika na maelezo yaliyotolewa na serikali kupitia kwa Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba, juu ya sababu za kuagiza umeme toka Ethiopia.
Sababu zilizotolewa;
- Umeme wa mikoa ya kaskazini unapelea au kukosekana kabisa
- Kukosekana kwa umeme huko kunatookana na umbali kutoka sehemu za uzalishaji umeme, yaani Dar esalaam, kwa umeme kutokana na mitambo ya gesi, na umeme toka Mkoa wa Pwani/Morogroro toka Bwawa la Mwalimu Nyerere
- Mikoa ya kaskazini inakosa umeme wa uhakika na kupungua sana kwa msongo(voltage)
- Serikali itaagiza umeme wa 100MW, ili kurekebisha matatizo Moshi, Arusha na Manyara, na kwa kufanya hivyo Songwe itaweza kupata 17MW
Najiuliza maswali yafuatayo,
- Je, kuna ukosefu wa Power production? jibu ni hapana kwani sasa hivi umeme unaozalishwa nchini 3,796MW, wakati mahitaji ni 2,200MW(Bwawa la Mwalimu Nyerere bado halijatenngeneza umeme at full caoacity)
- Katika ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere hapakuwepo Feasibility study? Study ambayo ingeweza kuona jinsi ya kusambaza umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere sehemu zote za nchi?
- Na je, ni mikakati gani itatumiwa na serikali kuona kwamba umeme wetu unaozaliwa Bwawa la Mwalimu Nyerere unatumika kikamilifu?
- Na je huko Ethiopia, si tunalipa kwa fedha za kigeni? Hizo gharama si zingetumika kusafirisha na kusambaza umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere
Wananchi tunajiuliza haya maswali mengi maana tunajua mradi wa ujenzi wa umeme wa Bwawa la Mwalimi Nyerere umetugharimu sana, tena sana, kiasi cha karibia Trillioni 7, fedha za kitanzania.
Swali linalotukatisha tamaa, ni je hizo Trillioni 7 za Bwawa la Mwalimu Nyerer ni wasted investment?
Tupate ufafanuzi tafadhali!!