View attachment 3266577
Mimi ni mmoja wa watu nisioridhika na maelezo yaliyotolewa na serikali kupitia kwa Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba, juu ya sababu za kuagiza umeme toka Ethiopia.
Sababu zilizotolewa;
- Umeme wa mikoa ya kaskazini unapelea au kukosekana kabisa
- Kukosekana kwa umeme huko kunatookana na umbali kutoka sehemu za uzalishaji umeme, yaani Dar esalaam, kwa umeme kutokana na mitambo ya gesi, na umeme toka Mkoa wa Pwani/Morogroro toka Bwawa la Mwalimu Nyerere
- Mikoa ya kaskazini inakosa umeme wa uhakika na kupungua sana kwa msongo(voltage)
- Serikali itaagiza umeme wa 100MW, ili kurekebisha matatizo Moshi, Arusha na Manyara, na kwa kufanya hivyo Songwe itaweza kupata 17MW
Bhati mbaya haya maelezo hayakidhi.
Najiuliza maswali yafuatayo,
- Je, kuna ukosefu wa Power production? jibu ni hapana kwani sasa hivi umeme unaozalishwa nchini 3,796MW, wakati mahitaji ni 2,200MW(Bwawa la Mwalimu Nyerere bado halijatenngeneza umeme at full caoacity)
- Katika ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere hapakuwepo Feasibility study? Study ambayo ingeweza kuona jinsi ya kusambaza umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere sehemu zote za nchi?
- Na je, ni mikakati gani itatumiwa na serikali kuona kwamba umeme wetu unaozaliwa Bwawa la Mwalimu Nyerere unatumika kikamilifu?
- Na je huko Ethiopia, si tunalipa kwa fedha za kigeni? Hizo gharama si zingetumika kusafirisha na kusambaza umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere
Wananchi tunajiuliza haya maswali mengi maana tunajua mradi wa ujenzi wa umeme wa Bwawa la Mwalimi Nyerere umetugharimu sana, tena sana, kiasi cha karibia Trillioni 7, fedha za kitanzania.
Swali linalotukatisha tamaa, ni je hizo Trillioni 7 za Bwawa la Mwalimu Nyerer ni wasted investment?
Tupate ufafanuzi tafadhali!!
Maelezo yanayotolewa kujustify ununuzi wa umeme toka Ethiopia ni propaganda tu kama ilivyokuwa kwa Richmond..
Hoja ya power loss ni hoja nyepesi inayotumiwa kuficha uongo unaopigiwa debe.
Katika nadhariia ya umeme power loss ni kitu kisichokwepeka na kinachokubalika ni sawa na Lori linalotembea kuna vyuma na parts vinasagika hivyo baada ya muda huwa vinabadilishwa. Hivyo mwenye gari anapochaji gharama za uchukuzi wa miizigo anaweka pia gharama za uchakavu ili baadae aweze kununua spea pale zitakapokuwa zimechakaa.
Umeme unaposafirishwa hata ndani ya wilaya moja au toka nyumba moja kwenda nyumba nyingine kuna power loss inatokea ambayo kitaalamu ni ( I squared times R). Ni kweli jinsi umbali unavyoongezeka ndivyo power loss nayo inaongezeka lakini ni kwa kiasi kidogo sana.
Kukabiliana na hilo la power loss, umeme unapozalishwa hatua ya kwanza unapandishwa juu sana mfano kutoka 33 KV zilizozalishwa kwenda 220 KV kwa kutumia step up transformer kabla ya kusafirishwa; hivyo unasafirishwa katika very high voltage; kitendo hiki kinasababisha current( I) ipungue sana hivyo kushusha power loss kitaalamu ( kumbuka formula ya power loss kihesabu za umeme ni (I times I times R). Umeme ukifika unakoenda unashushwa voltage kwa kutumia step down transformer hadi kiwango kidogo cha voltage mfano 11 KV katika sub stations, nao unasafirishwa ndani ya mji hadi majumbani na kushushwa tena kwa kutumia step down transformer zilizoko katika nguzo za umeme ili kuwa 415 Volts. Kitendo cha kupunguza voltage hupandisha current ( I ). Hizi ndio technique zinazotumika kudhibiti power loss kitaalam.
Ndio maana miaka yote huko nyuma umeme wa kidatu ulisafirishwa hadi Mwanza, Mbeya na maeneo ya mipakani kama Tarime ambapo ni zaidi ya km 1300 lakini tulikuwa hatusikii hizi ngonjera za power loss. Jiulize kwa nini sasa Kafulila na wengine wanapigia kelele ngonjera za power loss.
Mfumo wa tarrif wa kutoza gharama za.matumizi ya umeme unazingatia gharama zote kuanzia uzalishaji, usafirishaji, usambazaji, matengenezo, uchakavu,. Pia gharama walizotozwa watumiaji zililingana. TANESCO tangu mwaka 1991 imekuwa ikikumbwa na ubadhirifu mbalimbali unaotokana na mikataba isiyozingafia maslahi ya nchi na hiyo ndiyo ilifanya gharama za umeme ziwe juu kulinganisha na nchi zingine
Kuutoa umeme toka kwenye nguzo hadi ofisini au nyumbani kwake kuna power loss pia. Ni kama nilivyoeleza juu kwa kutumia mfano wa gari ya mizigo inapobeba mizigo.
Kingine, umeme unapozalishwa toka vyanzo mbalimbali unachanganywa katika grid ya Taifa ni kama maji yanavyochanganyika na kuwa kitu kimoja kwa sababu dunia nzima umeme unazalishwa katika makundi matatu tu yanayoitwa kitaalamu three phases huwa zinakuwa labelled Red, blue & yellow phases. Sasa wanaposema tunauza umeme wa mpakani sio sahihi kwa sababu umeme unakuwa umechanganyika kama maji huwezi kuutenga kuwa huu ni umeme wa pangani na huu ni wa kidatu na huu ni wa Rusumo nk hivyo ninauza umeme wa Rusumo siuzi umeme wa kidatu.
Hili bwawa la Rufiji viongozi na wanasiasa wengi hawakutaka kabisa lijengwe ndio maana sasa wametafuta hoja ya kulizuia lisitumike kikamilifu. Kama Magufuli asingetawala Bwawa ka umeme la Rufiji lisingejengwa kamwe.
Tanganyika licha ya kuwa na vyanzo vingi vya umeme vinavyofanya kazi pia ina potential ya kuzalisha kwa kutumia vyanzo vipya kama kule Singida kwa kutumia upepo, joto ardhi nk
Hivyo concept ya power loss inayotumiwa sasa ni vehicle tu ya kuhalalisha maamuzi mabovu na ni hoja mufilisi Kama zingine zote za awali ambazo tumekuwa tukiambiwa tangu mwaka 1991.