Kwa hili la kuagiza Umeme Ethiopia, wananchi tunahitaji maelezo ya ziada, tulijenga mitambo ya bwawa la Mwalimu kwa nini?

Haya masuali ya umeme yana taka elimu.

Ujarumani ina zalisha umeme mwingi sana
Sasa ina uza nje kwa karibu 70000 GWH na ina nunuwa 51000 GWH
Lakujiuliza kwa nini wanauza na kwa nini wana nunuwa.
France ni pia inanunuwa na kuuza.

Kuna ajabu gani Tanzania ikafanya hivyo kuuza na kununuwa.

Mfano kama Tanzania ina zalisha umeme kusini.
na wana hitaji umeme kaskazini. Basi ni bora kaskazini kununuwa na ule umeme wa kusini kuuza.
 
Kuwa na akili kujibu dondoo zilizowekwa.
 
Kwakweli ni muhimu serikali kuleta majibu sahihi katika suala hili.
 
Maelezo yanayotolewa kujustify ununuzi wa umeme toka Ethiopia ni propaganda tu kama ilivyokuwa kwa Richmond..

Hoja ya power loss ni hoja nyepesi inayotumiwa kuficha uongo unaopigiwa debe.

Katika nadhariia ya umeme power loss ni kitu kisichokwepeka na kinachokubalika ni sawa na Lori linalotembea kuna vyuma na parts vinasagika hivyo baada ya muda huwa vinabadilishwa. Hivyo mwenye gari anapochaji gharama za uchukuzi wa miizigo anaweka pia gharama za uchakavu ili baadae aweze kununua spea pale zitakapokuwa zimechakaa.

Umeme unaposafirishwa hata ndani ya wilaya moja au toka nyumba moja kwenda nyumba nyingine kuna power loss inatokea ambayo kitaalamu ni ( I squared times R). Ni kweli jinsi umbali unavyoongezeka ndivyo power loss nayo inaongezeka lakini ni kwa kiasi kidogo sana.

Kukabiliana na hilo la power loss, umeme unapozalishwa hatua ya kwanza unapandishwa juu sana mfano kutoka 33 KV zilizozalishwa kwenda 220 KV kwa kutumia step up transformer kabla ya kusafirishwa; hivyo unasafirishwa katika very high voltage; kitendo hiki kinasababisha current( I) ipungue sana hivyo kushusha power loss kitaalamu ( kumbuka formula ya power loss kihesabu za umeme ni (I times I times R). Umeme ukifika unakoenda unashushwa voltage kwa kutumia step down transformer hadi kiwango kidogo cha voltage mfano 11 KV katika sub stations, nao unasafirishwa ndani ya mji hadi majumbani na kushushwa tena kwa kutumia step down transformer zilizoko katika nguzo za umeme ili kuwa 415 Volts. Kitendo cha kupunguza voltage hupandisha current ( I ). Hizi ndio technique zinazotumika kudhibiti power loss kitaalam.

Ndio maana miaka yote huko nyuma umeme wa kidatu ulisafirishwa hadi Mwanza, Mbeya na maeneo ya mipakani kama Tarime ambapo ni zaidi ya km 1300 lakini tulikuwa hatusikii hizi ngonjera za power loss. Jiulize kwa nini sasa Kafulila na wengine wanapigia kelele ngonjera za power loss.

Mfumo wa tarrif wa kutoza gharama za.matumizi ya umeme unazingatia gharama zote kuanzia uzalishaji, usafirishaji, usambazaji, matengenezo, uchakavu,. Pia gharama walizotozwa watumiaji zililingana. TANESCO tangu mwaka 1991 imekuwa ikikumbwa na ubadhirifu mbalimbali unaotokana na mikataba isiyozingafia maslahi ya nchi na hiyo ndiyo ilifanya gharama za umeme ziwe juu kulinganisha na nchi zingine

Kuutoa umeme toka kwenye nguzo hadi ofisini au nyumbani kwake kuna power loss pia. Ni kama nilivyoeleza juu kwa kutumia mfano wa gari ya mizigo inapobeba mizigo.

Kingine, umeme unapozalishwa toka vyanzo mbalimbali unachanganywa katika grid ya Taifa ni kama maji yanavyochanganyika na kuwa kitu kimoja kwa sababu dunia nzima umeme unazalishwa katika makundi matatu tu yanayoitwa kitaalamu three phases huwa zinakuwa labelled Red, blue & yellow phases. Sasa wanaposema tunauza umeme wa mpakani sio sahihi kwa sababu umeme unakuwa umechanganyika kama maji huwezi kuutenga kuwa huu ni umeme wa pangani na huu ni wa kidatu na huu ni wa Rusumo nk hivyo ninauza umeme wa Rusumo siuzi umeme wa kidatu.

Hili bwawa la Rufiji viongozi na wanasiasa wengi hawakutaka kabisa lijengwe ndio maana sasa wametafuta hoja ya kulizuia lisitumike kikamilifu. Kama Magufuli asingetawala Bwawa ka umeme la Rufiji lisingejengwa kamwe.

Tanganyika licha ya kuwa na vyanzo vingi vya umeme vinavyofanya kazi pia ina potential ya kuzalisha kwa kutumia vyanzo vipya kama kule Singida kwa kutumia upepo, joto ardhi nk

Hivyo concept ya power loss inayotumiwa sasa ni vehicle tu ya kuhalalisha maamuzi mabovu na ni hoja mufilisi Kama zingine zote za awali ambazo tumekuwa tukiambiwa tangu mwaka 1991.
 
On this I concur.
Mahali pa energy ndio miaka yote kuna upigaji mwingi.
 
Miradi ya kuwapa Wastaafu mafao ya Kikokotoo kama ile PSPF😭😭.
 
Hivi Nyumba ya Mungu na Hale Pangani hawazalishi tena Umeme??
 
Du....mbo mbo ngafu!
 
Umenena vema mkuu!
 
Ila ni ajabu sana umeme kutoka bwawa hilohilo unafika Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora na Mwanza ilahuo umeme hauwezi kufika KAT
 
Ila ni ajabu sana umeme kutoka bwawa hilohilo unafika Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora na Mwanza ilahuo umeme hauwezi kufika KAT
Huo umeme umechanjiwa, kuna sehemu hautaki kwenda.
 
Umeme unazalishwa JNHP unafika mikoa ya mbali kama Singida halafu ishindikane kwenda Tanda Arusha na Klm
 
Sijajua Motives Ya Tanzania kununua Umeme Ethiopia, Lakini Hili Jambo sio geni wala Sio baya.

Inawezekana Kabisa ukawa na nyumba Bagamoyo, Lakini ukapanga Kimara kwasababu ni karibu na shughuri Zako za kila siku.

Hivyo tuendelee kuomba ufafanuzi wa motives ya TANESCO kununua umeme nje
 
Hakuna tatizo la umeme wala uhaba.
Usafirishaji wa umeme una changamoto ambazo ni kama unatoka Ethiopia ukiwa 200MW mpaka unafika Tanzania unakuta umepungua na kufika 110MW so 90MW zimeshapotea njiani. Hivyo Tanzania haihusiki na upotevu huo na hasara hiyo.Tanzania Italipa Megga Watts zilizopokelewa Sub Station tu. Serikali yetu haihusiki na upotevu ama kupunguza kwake wakati wa kuusafirisha.
➡️Like wise miundombinu ya kutoa umeme Bwawa la Mwalimu ni ghali zaidi +leakage kuliko kununua ambao umeshafikishiwa sub station.
 
Kwa hiyo tunafanya vitu vya maendeleo bila kufikiri au kufanya utafit.
Kwani Feasibility study iliyofanyika kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la JNHP .
Tunajenga kitu kikubwa sana kwa Trillioni 7 halafu hakina manufaa kwa nchi nzima?
 
Watu kama nyinyi ndio mnakaaga kwenye nyumba za kupanga kisa heti kujenga nyumba yako ni garama kubwa huu ni ujinga na upuuzi, uwezi kwenda kununua bidhaa kwa jirani wakati wewe mwenyewe hiyo bidhaa unayo kisa unaofia gharama,tunao viongozi wazembe wa kufikiri ndio Maana taifa aliwezi piga hatua.
 
Fikiri kidogo.
Ethiopia wao wajinga sisi wajanja?

Soma andiko langu hapo juu nimeandika kitaalamu halafu mtafute mtu aliyesomea umeme muulize..

Rufiji hadi mwanza na Tarime linganisha umbali na Ethiopia arusha. Unafahamu Pangani na bwawa la nyumba ya mungu umeme unazalishwa? KIihansi huko Kilombero umeme unazalishwa?

Usidandie jambo la kitaalamu bila kusoma kwanza nadharia za kitaalamu zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…