Kwa hili la TANROADS na Mfugale nadhani Magufuli ameanza kunielewa

Aisee kuna mengi tusiyoyajua,Magufuli hatamgusa swaiba wake..
 
Endeleeni kupiga ramli, mwacheni rais afanye kazi yake.
Hivi unajua hao unaowaambia wanapiga ramli ndio wanaolipia kwa kodi zinazokatwa kwenye mishahara yao na biashara wanazofanya?

Unaonyesha either hujui unaongea nini au hujafikia umri wa kuchangia maendeleo ya taifa hili.

Mkisikia Rais sijui mnamuona kama Mungu? Ni mtu kama wewe na mimi. Ni mfanyakazi wetu tumemuajiri asimamie maendeleo ya taifa. Sasa mwajiri analazimikaje kumwogopa mfanyakazi?

Au mfanyakazi kashatuloga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu hawafai kabisa na siwezi kuendesha gari huko tena katika maisha yangu
Ni hivi nilikuwa namsaidia dereva aliekuwa kachoka usiku
Qhafla nikakutana na kifusi kikubwa cha na kwenye kifusi ndio wameweka alama ya diversion
Bahati nzuri nilikuwa naenda taratibu tu yaani unaweza kukutana na daraja limekatika ukadumbukia tu
Kweli sisi bado sana katika usalama wa barabara


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwa kifupi Mfugale kadumaa na kufubaa pale ujenzi, hivi sasa kazeeka hawezi kwenda na wakati na technologies yake anayoijua imepitwa na wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kavideo mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusimulaumu Mfugale bali tumulaumu anayetaka asitoke ofisini. Mtu ana miaka zaidi ya 67 bado hutaki astaafu. Mzee kachoka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiwezekani, ana miaka 67? Kwani hiyo position ni uteuzi wa kisiasa? Umri wa watumishi wa seikali kustaafu ni miaka mingapi?
 
Mkuu unatuchanganya hapa. Madaraja yanajengwaje kisiasa? Uokoaji changamoto ajali zikitokea?

..kwanza, barabara zinatakiwa ziwe na UPANA wa kutosha kwa magari kupishana kwa usalama.

..pili, zinatakiwa zijengwe kwa namna ambayo inawezesha shughuli za UOKOAJI ikiwa kutatokea ajali.

..hayo yanatakiwa yazingatiwe juu ya UBORA wa barabara zenyewe.

..sasa niambie kama ujenzi wa barabara zetu umezingatia hayo mawili.
 
Mie nadhani anajisahau sana kutokana na kujua yuko karibu na Magufuli. Sasa hapo changanya na kale katabia ka Kihehe ka kuwa na "kidada"
Hili la ukaguzi wa barabara hasa sehemu mashimo nikupongeze. Umepaza sauti sana na umetoa ushauri mzuri. Pongezi sana.
 
Ati rais anamwogopa mtu, mnafikiri huyu ni Vasco Da Gama? JPM anafanya kazi ambayo rais yeyote anayejitambua anafanya. Natumaini unapata salam kila kinachoendelea ndani ya TZ.
 
Unanikumbusha ajali ya Majinja eneo la kukaribia Mafinga kama unatoka Nyororo uzembe ule Tanroads wakakaa kimya kabisa, kuna barabara ya Igawa-Tunduma haiko vizuri kabisa na inamagari mengi sana, Tanroads kuna tatizo kubwa la kiutendaji
 
Kula kulala huyo usikute anaishi kwa Mme wa Dada yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…