Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Mm ni muumini wa dhana ya wajibu wa raia kwa viongozi, kama ulivyo wajibu wa viongozi kwa raia. Kama raia wema tunao wajibu kuikosoa serikali inapokosea ili ijisahihishe, vilevile tunao wajibu wa kuwapongeza viongozi wetu wanapofanya vizuri ili kuwatia moyo wafanye vzr zaidi.
Serikali ilipoyafungia makanisa ya ufufuo na uzima tulinuna. Lakini ushuhuda wa Mtume Mwamposa akieleza ushiriki wa serkali kufanikisha ujenzi wa hema lakukutania umetupa faraja.
Katika Dunia ya leo ya diplomasia, ni matazamio yetu wanachi kuwa serikali itafanya kazi na viongozi wetu wa kiroho wa madhehebu yote kudumisha utengamano wa kitaifa. Ushiriki wa Serikali katika kuhakikisha ustawi wa taasisi zetu za kidini ni hatua muhimu katika kujenga utamaduni huo.
Kwasababu hiyo tunampongeza Rais kwa jambo hili. Aidha tunaendelea kumsihi, akiwa kama mlezi wa taifa, kusamehe pale anapoona amekosewa, na ikimpendeza aridhie makanisa ya ufufuo na uzima kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kutangaza Injili.
Mwisho ni muhimu kuwasihi viongozi wetu wa kidini, kujiepusha kufanya siasa mimbarini. Ni jambo lililowazi kuwa wanao wajibu wa kukosoa, kukemea, kuonya na hata kupongeza serikali kwa kadri inavyobidi kama wadau muhimu wa ustawi wa nchi yetu. Lakini namna gani hilo linafanyika ina muhimu wa namna yake pia.
Mungu ibariki Tanzania yetu.