Kwa hili la wananchi kufurika ofisi za NIDA ili kuokoa line zao zisifungwe linaonyesha kuwa ufahamu wa wananchi bado ni duni

Kwa hili la wananchi kufurika ofisi za NIDA ili kuokoa line zao zisifungwe linaonyesha kuwa ufahamu wa wananchi bado ni duni

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,943
Habari ndugu wananchi!

Mafuriko ya wananchi kwenye ofisi za NIDA hasa kipindi hiki kuelekea tarehe za kufungwa line ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole linatupa ukakasi juu ya ufahamu na uelewa wa wananchi.

Kitambulisho cha taifa si kwa ajili ya kusajilia line, suala la kitambulisho cha taifa kusajilia line ni jambo la ziada tu.

Kitambulisho cha taifa kinamtambulisha Mtanzania uraia wake na ndio dhima haswa. Kila mwananchi hapaswi kupuuza kufuatilia na kukipata kitambulisho hiki na si kwaajili ya kumuezesha kupata pass ya kusafiria au kusajilia line za simu tu.

Yaani watu hawakuona umuhimu wa kitambulisho cha UTAIFA NA URAIA WAO mpaka walipoambiwa kuwa line zao zitawekwa rumande!!

Inasikitisha sana.
 
Wananchi wana haki ya kupata kitambulisho cha utaifa wao ili waweze kutambuliwa kila watakapohitaji huduma. Sasa cha ajabu kuna wakati wakaacha au walisimama kufuatilia kitambulisho hiki. Sasa wameamka kwa nguvu baada ya kusikia kitatumika kusajilia line zao.
Utafikiri tatizo ni wananchi au waliotoa Tangazo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonde la Baraka,
Nawashangaa Watanzania sana.Tulikuwa na muda wa kutosha kuandaa vitambulisho ili hatimaye tuweze kusajili line zetu,lakini hatukujali kabisa kufanya hivyo.Matatizo watu wanayopata ya kujazana kwenye ofisi za NIDA na makampuni ya simu,kukanyagana na kupoteza muda kiukweli yangeweza kuepukika.Nadhani tuna shida kubwa sana kwenye akili zetu,we tend to do everything at the last minute,and this is wrong.People need to be more organized.Ni lazima tubalike,hatuwezi kuendelea hivi.

Hata hivyo namshukuru Rais kwa kuliona tatizo na kuongeza siku 20.
 
Ni Vema Uangalie Vizuri, Iwapo Tatizo Ni Wananchi Ama Serikali Yenyewe. Ofisi Za NIDA Zipo Mikoani
Huko Vijijini Wanatakiwa Wafunge Safari
Ikumbukwe Kabla Ya Sasa Hivi
Lazima Mwananchi Alitakiwa Aende Mkoani
 
Mbona tunajitoa akili kwani hamjui kua tatizo liko wapi? Waliojiandisha NIDA vitambulisho au namba hazikupatikana kwa wakati! Au hatujui tatizo liko wapi?
 
Mimi kwahili nakupinga ! Nakumbuka zoezi lenyewe lilikuwa ni mkurupuko.com ; halafu lilikuwa la muda mchache sana! Mfano kwa wilaya ya Nyangh'are ilikuwa Kila kitongoji ni siku 3 hapohapo waandikishaji wanakuja saa 4 asbh wanaondoka saa 10 jion,, siku nyingine walikikosa mafuta ya gari hawaji kabisaa!

Kabla hatujawalaumu wananchi inatakiwa tuungalie serikali na NIDA walitekeleza wajibu wao kikamilifu hapo mwanzoni ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kimsingi baada ya kuonekana watu hawana mwamko wa kujisajili ili wapate vitambulisho hivyo, ndio ikabuniwa njia ya kuwalazimisha waone umuhimu huo. Na kiukweli kwa njia hii wamefanikiwa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi hii ilikuwa njia ya kuhamasisha ?
Kama ni kweli basi aliyebuni ni kichwa sana
 
Mimi nafikiri hili swala linaweza kufanyika online hasa ukilinganisha matumizi ya internet ni makubwa sana kwa simu za mikononi na hata Internet cafes kwenye maeneo mengine na kwa wale wasioweza ndio kundi hili lifike NIDA moja kwa moja zoezi hili likifanyika online litaenda kwa kasi nzuri
 
Bonde la Baraka,
Wewe ndio una fikra duni, sio hao wananchi, Kwanza umetembea nchi nzima kujionea mafuriko? Au umeanza kujenga hoja kwa uongo? Na nani kakwambia wananchi wanafuatilia kitambulisho cha taifa kwa sababu ya kusajili line tu? Je kitambulisho cha zamani cha kupigia kura walikitumia kusajili line pekee au walikitumia kwenye shughuli mbalimbali? Pia wewe unaona sawa mtu kufungiwa line yake? Dunia ya sasa utakaaje bila line ya simu? Wewe ufahamu wako ndio mdogo sio wananchi! Kwanza huo mchakato wa kupata kitambulisho cha taifa ni mwepesi kiasi gani ??
 
Bonde la Baraka,
Wala usiwalaumu wameelewa vizuri kuliko hata wewe. Hiki kitambulisho ndio kazi yake maana ingekuwa kitambulisho cha urai kama kinavyosemekana basi kisingewaacha baadhi ya raia.

Mfano, kwa mujibu wa sheria yetu inamtambua raia kuanzia siku anapozaliwa maadam amezaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania ndio maana sensa inapofanyika kujua idadi ya watz huwa ni kwa wote sasa inakuwaje watz waliochini ya miaka 18 hawahusiki na hivi vitambulisho? Au wao sio sehemu ya watz.?

Pia kilichofanya waelewe hivyo ni mfumo waliotumia wakuu wetu kukitambulisha kwa wananchi. Inamaana wao hawakuona uzito wa hiki kitambulisho hadi wapitie kwenye simu? Kwann wasingeanzisha uhakiki wa RAIA kupitia kitambulisho hiki nchi nzima ili kukipa hadhi na thamani yake. Sasa swali kwako mwananchi atakielewaje hiki kitambulisho na umhimu wake kama wao wamepitia kwenye laini za simu? Maana kama ni kuishi bila kuwa nacho habugudhiwi na huru hataona thamani yake kama ni cha uraia. Laiti kama wangepitisha sensa ya raia kwa kutumia kitambulisho hiki watu wangeelewa kuwa ni uraia lakin kwa mfumo alotumia wananchi wana haki ya kuelewa walivyoelewa.
 
Mimi Dar es salaam nina miaka 5 sasa.
Ofisi za NIDA zilikuwa wazi kutoa huduma ila hazikuwa na watu. Waliokwenda NIDA wengi walikuwa wanakwenda kuulizia vitambulisho vyao.ulipozinduliwa mfumo wa PASSPORT ZA KISASA ambapo mwombaji alipaswa kuwa na kitambulisho cha taifa ndipo watu wakaanza kifuata huduma ili wakapate passport UHAMIAJI.
Mimi kwahili nakupinga ! Nakumbuka zoezi lenyewe lilikuwa ni mkurupuko.com ; halafu lilikuwa la muda mchache sana! Mfano kwa wilaya ya Nyangh'are ilikuwa Kila kitongoji ni siku 3 hapohapo waandikishaji wanakuja saa 4 asbh wanaondoka saa 10 jion,, siku nyingine walikikosa mafuta ya gari hawaji kabisaa!

Kabla hatujawalaumu wananchi inatakiwa tuungalie serikali na NIDA walitekeleza wajibu wao kikamilifu hapo mwanzoni ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ndugu wananchi!

Mafuriko ya wananchi kwenye ofisi za NIDA hasa kipindi hiki kuelekea tarehe za kufungwa line ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole linatupa ukakasi juu ya ufahamu na uelewa wa wananchi.

Kitambulisho cha taifa si kwa ajili ya kusajilia line, suala la kitambulisho cha taifa kusajilia line ni jambo la ziada tu.

Kitambulisho cha taifa kinamtambulisha Mtanzania uraia wake na ndio dhima haswa. Kila mwananchi hapaswi kupuuza kufuatilia na kukipata kitambulisho hiki na si kwaajili ya kumuezesha kupata pass ya kusafiria au kusajilia line za simu tu.

Yaani watu hawakuona umuhimu wa kitambulisho cha UTAIFA NA URAIA WAO mpaka walipoambiwa kuwa line zao zitawekwa rumande!!

Inasikitisha sana.
Mkuu Mimi naenda kinyume na wewe na kuwatetea wananchi.
Wananchi si kwamba hawajui umuhimu wa kuwa na kitambulisho Bali watoaji wa vitambulisho ndio uelewa wao ni mdogo kutokana na urasimu wanaoufanya.
Yaani mwananchi aache shughuli zake na kufuatilia kitambulisho mwezi mzima na apange foleni masaa nane kusubiria kuandikishwa kitambulisho na bado apewe ahadi za uongo za kila siku nenda rudi.
Huo urasimu ndio huwafanya raia kususa na kupotezea mambo ya kitambulisho.
Nchi za wenzetu kitambulisho ni kitu Cha kuchukua siku moja tu kwa sababu wanajua umuhimu wa muda.
Na hii hali sio kwenye kitambulisho Cha nida tu bali hata kile Cha kura na hati ya kusafiria uzembe ni ule ule.
Sasa kwa mazingira Kama haya utawalaumu vipi wananchi na kusema eti hawajielewi?Ni wananchi au waliopewa dhamana ya kutoa hivyo vitambulisho ndio hawajielewi?Jibu umeshalipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom