Kwa hili la wananchi kufurika ofisi za NIDA ili kuokoa line zao zisifungwe linaonyesha kuwa ufahamu wa wananchi bado ni duni

Kwa hili la wananchi kufurika ofisi za NIDA ili kuokoa line zao zisifungwe linaonyesha kuwa ufahamu wa wananchi bado ni duni

Habari ndugu wananchi!

Mafuriko ya wananchi kwenye ofisi za NIDA hasa kipindi hiki kuelekea tarehe za kufungwa line ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole linatupa ukakasi juu ya ufahamu na uelewa wa wananchi.

Kitambulisho cha taifa si kwa ajili ya kusajilia line, suala la kitambulisho cha taifa kusajilia line ni jambo la ziada tu.

Kitambulisho cha taifa kinamtambulisha Mtanzania uraia wake na ndio dhima haswa. Kila mwananchi hapaswi kupuuza kufuatilia na kukipata kitambulisho hiki na si kwaajili ya kumuezesha kupata pass ya kusafiria au kusajilia line za simu tu.

Yaani watu hawakuona umuhimu wa kitambulisho cha UTAIFA NA URAIA WAO mpaka walipoambiwa kuwa line zao zitawekwa rumande!!

Inasikitisha sana.
Wewe mbumbumbu Ofisi za Nida zinafurika kila siku hakuna siku hazikufurika ila kwasasa mafuriko yamekuwa makali zaidi. Nida Warudi mtaani tena kama walivyoanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wengi walikuwa wanakomea uhamiaji baada ya kuambiwa wakaoneshe makabuli ya babu zao
 
Wananchi wana haki ya kupata kitambulisho cha utaifa wao ili waweze kutambuliwa kila watakapohitaji huduma. Sasa cha ajabu kuna wakati wakaacha au walisimama kufuatilia kitambulisho hiki. Sasa wameamka kwa nguvu baada ya kusikia kitatumika kusajilia line zao.
Are you MAD bro? NIDA wangekuwa wanatoa hivyo vitambulisho badala ya NAMBA tu, tena bila USUMBUFU na kwa wakati unadhani kuna Mwananchi ambaye angepuuzia?
 
Watu wanahangaishwa kuvipata hivyo vitambulisho vya taifa, hao NIDA either hawapo efficient au hawana pesa kutekeleza hilo zoezi kwa kasi inayotakiwa
 
Habari ndugu wananchi!

Mafuriko ya wananchi kwenye ofisi za NIDA hasa kipindi hiki kuelekea tarehe za kufungwa line ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole linatupa ukakasi juu ya ufahamu na uelewa wa wananchi.

Kitambulisho cha taifa si kwa ajili ya kusajilia line, suala la kitambulisho cha taifa kusajilia line ni jambo la ziada tu.

Kitambulisho cha taifa kinamtambulisha Mtanzania uraia wake na ndio dhima haswa. Kila mwananchi hapaswi kupuuza kufuatilia na kukipata kitambulisho hiki na si kwaajili ya kumuezesha kupata pass ya kusafiria au kusajilia line za simu tu.

Yaani watu hawakuona umuhimu wa kitambulisho cha UTAIFA NA URAIA WAO mpaka walipoambiwa kuwa line zao zitawekwa rumande!!

Inasikitisha sana.
Maelezo yako hayana ukweli, bila shaka watu wamesubilia sana feedback ya vitambulisho baada ya zoezi la uandikishaji bila mafanikio.

Wananchi waliamini baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika mtawasambazia kwa utaratibu ule ule vitambulisho vyao mahala walipo lakini mpaka sasa kuna maeneo hawajui hivo vitambulisho lini vitarudi, na wengine hata verification kwa mitandao hakuna majibu waliyotegemea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo Mafuriko ya watu kupata Vitambulisho vya NIDA ili kunusuru line zao inathibitisha kabisa kuwa tunathamini like zetu kuliko vitambulisho vyenyewe na bila shaka bila ya strategy hii ya kulazimisha watu kusajili lime zao kwa ID za Taifa basi watu wengi wangevipotezea
 
Habari ndugu wananchi!

Mafuriko ya wananchi kwenye ofisi za NIDA hasa kipindi hiki kuelekea tarehe za kufungwa line ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole linatupa ukakasi juu ya ufahamu na uelewa wa wananchi.

Kitambulisho cha taifa si kwa ajili ya kusajilia line, suala la kitambulisho cha taifa kusajilia line ni jambo la ziada tu.

Kitambulisho cha taifa kinamtambulisha Mtanzania uraia wake na ndio dhima haswa. Kila mwananchi hapaswi kupuuza kufuatilia na kukipata kitambulisho hiki na si kwaajili ya kumuezesha kupata pass ya kusafiria au kusajilia line za simu tu.

Yaani watu hawakuona umuhimu wa kitambulisho cha UTAIFA NA URAIA WAO mpaka walipoambiwa kuwa line zao zitawekwa rumande!!

Inasikitisha sana.

Hakuna cha kusikitisha hapa, mtu kazaliwa na kukulia TZ halafu leo unataka umwambie awe na kitambulisho cha Uraia??!!, uraia wa nchi gani??, mtu hajui ni lini atasafiri kwenda nje ya Tz!!,

Kwa yule anayeona umuhimu wa kuwa na kitabulisho basi na afanye mchakato wa kuwanacho lakini isiwe jambo la "lazima."

Tanzani nchi yetu aliyetupatia Mungu mwenyezi, Wtz tuko Peace tu.🤣🤣
 
Na vile vitambulisho vya mpiga kura vilitolewaje mpaka kila mtu anaestaili akapata?

Hivi vya nida ni nn kimetokea mpaka waseme watazifungia line za wasiokuwa na vitambulisho?

Na yule mkuu wa nida alitumbuliwa kwa ajili ya kuchelewesha zoezi hili.
Huyu wa sasa kafanya nn hata asitumbuliwe!?

Mkuu utaratibu mzima wa uandikishaji, uhamasishaji na upatikanaji wa vitambulisho, ndo tatizo! Sio wananchi.

Hata ikifika hiyo tr 20, nida hawatakuwa wameandikisha watu wote.

Wazifunge tu hizo line.

Ni jana tu nimesajili line kwa alama za vidole vya mtu nisiemjua na nataka nikanune line nyingine ya safaricom maisha yaendelee. Nida Watakavokuwa sawa nitaenda"
Hayo Mafuriko ya watu kupata Vitambulisho vya NIDA ili kunusuru line zao inathibitisha kabisa kuwa tunathamini like zetu kuliko vitambulisho vyenyewe na bila shaka bila ya strategy hii ya kulazimisha watu kusajili lime zao kwa ID za Taifa basi watu wengi wangevipotezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Vema Uangalie Vizuri, Iwapo Tatizo Ni Wananchi Ama Serikali Yenyewe. Ofisi Za NIDA Zipo Mikoani
Huko Vijijini Wanatakiwa Wafunge Safari
Ikumbukwe Kabla Ya Sasa Hivi
Lazima Mwananchi Alitakiwa Aende Mkoani
Kennedy,
Ni kweli NIDA wana matatizo,lakini niamini kwamba tangu wameanza zoezi la kuandisha watu kwa ajili ya kupata vitambulisho vya taifa mtu,mtu serious asingekuwa amepata kitambulisho kweli?Mbona wengine tulioanza mapema tumepata bila shida?Najua watu wengi ambao siku nilipokwenda kujiandikisha niliwaambia twendeni, lakini hawakujali.Na hata niliporudi nilijaribu kuwahamasisha,lakini hawakujali na sasa wanahangaika.The funny thing is,eti watu kama hao nao wanailamu NIDA!Sikatai there could be genuine complainants,but some complaints are unfair.
 
Back
Top Bottom