Kwa Hili la wimbo wa Simba (official audio) viongozi Simba mmeleta utani!!

Kwa Hili la wimbo wa Simba (official audio) viongozi Simba mmeleta utani!!

Jamani nyimbo ya mc sudi naipenda simba mshabiki wa damu hii ilikuwa bonge la nyimbo
 
Ngoja nimsikilize pepe kale hapa na lile song akiimbia timu wananchi
 
Kama ingewezekana baadhi ya mambo kabla ya kupitishwa rasmi basi uongozi/viongozi wangetoa nafasi ya kupata maoni toka wapenzi, nk.
Mfano, kama nafasi ya maoni ingetolewa kuhusu slogan ya mwaka huu ya "IGA UFE, THIS IS NEXT LEVEL" kabla ya kupitishwana au kutangazwa rasmi nadhani watu wengi sana wangeshauri kuachana na maneno ya IGA UFE. Hili neno halijakaa vizuri. Linaakisi kama neno la MIPASHO fulani hivi. Labda lingetafutwa neno la mshikamano zaidi. Mfano, "Simba Tushikamane, This is Next Level " Ten Years.........
Yani wewe uwezi kufanya market Tanzania. Unapofanya suala la marketing angalia culture ya watu husika na nini watu wanahitaji kwa wakati huo.
Wakati huo Yanga wameiga kuweka wiki ya mwananchi unafikiri Wanasimba walikua wanahitaji nini?
 
Clubs za mpira nyimbo yake inakuwa moja tu mfano BARCA, LIVERPOOL, MADRID,BAYERN
hizo team nyimbo yao waga haibadiriki kabiasa.

nashangaaga sana bongo mara nyimbo kaimba msagasumu , mara tundaman, mara Steve Nyerere, mara shilole ,sunura ,mara sholo mwamba,tena wanaimba wakitoka kuvuta bangi nyimbo inakuwa kama wameimbiwa wahuni flani Tu.

mashabiki wa izo team washaurini kina manara waache uswahili Kwenye mpira soccer sio kigodoro.
Hao mashabiki wenyewe aslimia 89 wanashikiwa akili.
 
Yani wewe uwezi kufanya market Tanzania. Unapofanya suala la marketing angalia culture ya watu husika na nini watu wanahitaji kwa wakati huo.
Wakati huo Yanga wameiga kuweka wiki ya mwananchi unafikiri Wanasimba walikua wanahitaji nini?
Wimbo wa Klabu ni sawa na wimbo wa Taifa. Unatakiwa kwanza uimbwe kiheshima sana. Sasa huo wimbo gani? Sema hata hivyo % kubwa ya mashabiki ni waswahili akili ya kushikiwa.
 
ule mchiriku anachezaga manara naipenda simba mshibiki wa damu ni bora mara 1000 kwa huu
 
aisee kama kweli ndo wimbo huu tulikuwa tunasubiri afadhali usiimbwe tu!!!
 
Nimeusikiliza nikakosa cha kusema. Ni mbovu, hauna chorus na kikawaida chorus ndio hushikwa na mashabiki. Tatizo hawajashirikisha watu bali walijifungia studio.
Wimbo hata hjeleweki kinaimbwa nini. Huu sio wimbo wa Simba.
Ni wimbo wa kutangaza utalii kuhusu Mnyama Simba na sio Simba FC
 
Wimbo wa Klabu ni sawa na wimbo wa Taifa. Unatakiwa kwanza uimbwe kiheshima sana. Sasa huo wimbo gani? Sema hata hivyo % kubwa ya mashabiki ni waswahili akili ya kushikiwa.
Yaani wewe ka si ushabiki na mihemko basi ni miongoni mwa wale unaosema wanashikiwa akili.

Mi nimefanya quotation hapo ya kile nilicho comment lakini wewe unakuja kuzungumzia wimbo. Aliyesema wimbo ni mzr nani. Kuelewa uwezi hata kuona pia.
Rudia tena ile comment yangu.
 
Kuna wimbo sikumbuki ni mwaka gani ila simba ilikua inacheza na Al shandy nadhani sina uhakika.

Simba ilishinda hii mechi ukapigwa wimbo kuhusu Simba, ulikua wimbo mzuri mtu unatamani hadi kucheza, bora hata ungewekwa ule.
 
Bora tenda tungempatia msaga sumu
 
Kwangu mimi ule wimbo uliopita " Naipenda Simba mshabiki wa Damu" ni bora mara 100, Kitu cha muhimu zaidi ni kujua malengo ya wimbo kama huu, kama ni kuhamasisha basi tutoe kitu cheche kuhamasisha, kama ni kwa ajili ya dua ya dua iwe dua, halafu baada ya maombi show la kibabe la kuhamasisha lianze. Nafikiri kwa wimbo huu hatukujua nini tunataka, tumekwama kati ya maombi (Wimbo wa taifa wa Simba) na Kuhamasisha
 
Back
Top Bottom