Kwa Hili la wimbo wa Simba (official audio) viongozi Simba mmeleta utani!!

Kwa Hili la wimbo wa Simba (official audio) viongozi Simba mmeleta utani!!

Nimesikia huu Ni wimbo wa Hamasa sio anthem kwa maana ya wimbo rasmi wa klabu wenyewe bado unatengenezwa...

Ila hata uitweje bado haufai kutumika Kwenye shughuli rasmi ya simba
 
wampe Juma Nature kazi hatawaangusha.........
 
Mimi shabiki wa yanga,ila sijui kwanini simba wameuacha ule wimbo wa naipenda simba shabiki wa damu,ulikuwa bonge la wimbo la hamasa,ule ndio ulikuwa wimbo wa kutumiwa
 
Mimi pia ni shabiki wa Simba lakini kwa wimbo huu kuwa ndio Simba Anthem ni big no. Hata ile Iga ufe ilikuwa ni kosa la kiufundi pia. Mtazamo wangu, Haji Manara ni muhasishaji mzuri lakini si kila kitu kinachohusu club kwenye eneo lake la kiutendaji aamue peke yake. Nasema hivi sababu sioni kama bodi ya simba ilikaa na ikapitisha hivi vitu viwili.
 
Mimi ni Simba niseme tu hatuna wimbo rasmi wa simba
Tukihitaji wimbo rasmi tutangaza tender na wimbo lazima utungwe kitaalamu
 
Wangewatafta akina simbaaa wawatengenezee nyimbo za maana
 
Back
Top Bottom