Kwa hili namsifu kikwete!

Kwa hili namsifu kikwete!

Kasimba G

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
3,428
Reaction score
2,612
Kuna vyama vingi wengine huvitambua kama vikundi kama POLISALIO, PKK e.t.c. Ambavyo chimbuko lake ni madai yao ya kuwa wamemezwa au wanaonewa au Wanatawaliwa kimabavu. Suala kama hili si mssamiati mgeni hapa kwetu Tanzania, Kuna upande mmoja kama siyo zote! U/Wanadai wamemezwa, lakini tofauti na POLISALIO ni kwamba bado embe ni mbichi, yaani wamezwaji hawajawa tayari kuanzisha mapambano ya siraha ili waachiwe.

Kama nchi tumshukuru saana MUngu kwa kuwa bahati nzuri alitujaalia chokochoko za mdomoni tuu pasi na kutumia siraha, Nampongeza saana Kikwete kuruhusu na kutokuwekea mapenzi binafsi na unafiki kuhusu serikali tatu, japo katika chama chake wamejipanga kuhujumu zoezi kwa kubainisha ati suala la serikali mbili ni suala la kikatiba katika chama chao, Kuna mambo ambayo kibinafsi na kipekee kabisa nampongeza Kikwete, Kwanza amekuwa unpredictable kwa wanafiki wengi katika chama chao, kwahili nasema amezingatia zaidi masrahi ya chi zaidi ya masrahi ya chama chake, mfano ni pale mwanasheria mkuu plus waziri wa sheria walivyosema katiba ya sasa ni ya wananchi na haihitaji marekebisho yoyote na inatufaa, yeye akaja na nia ya kuandika katiba mpya!

Kikwete amekuwa sio mnafiki kama most of African politician wanavyo react ikija suala la masrahi binafsi katika hili la uandishi wa katiba mpya, Tunajua most of African countries hazijawahi kuwa na katiba zao binafsi zaidi ya kuwa na katiba zilizorithiwa toka kwa wakoloni, ambazo, hazizingatii maslahi ya nchi na wanachi wake, zaidi zaidi zinalinda masrhi binafsi ya watawala, from watawala wakoloni to watawala waafrica!

Namuombea kwa Mungu, aendelee na moyo huo huo wa kutokuwa mnafiki kama wateule wake wengi na atufikishe pazuri zaidi katika suala hili la katiba mpya, tupate katiba mpya nzuri na yenye kujari zaidi maslahi ya wananchi na nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Africa!
 
kikwete hakutaka katiba mpya,alijua kuwa chadema wangewahamasisha watu pasingekalika.
unatumia sana r kwenye l,kwani we mkurya?
kikwete na ccm wameikubali katiba mpya huku roho inawauma sababu wanajua wanatimiza matakwa ya chadema.
kikwete ni mnafiki na dha.ifu
NB.tokea melo apate ajali amekuwa anapiga ban ovyo ukimtaja jk kwa jina jingine...
 
Mmh, labda sijakuelewa, unamsifia kwa kitu gani?
Kwa kuruhusu serikali tatu au kuruhusu katiba kuandikwa?
 
both, kwa kuruhusu katiba iandikwe na kuweka suala la tanganyika manaake kwa siku za usoni lingekuja kuleta maafa katika taifa letu hili!
 
Back
Top Bottom