Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 413
Jana nilipokuwa naangalia taarifa ya habari TBC1 kulikuwa na habari ya ziara ya JK nchini misri na alipata nafasi ya kuonana na watanzania wanaosoma nchini humo.
Katika mazungumzo yake na hao wenzetu walioko huko alisema anafikiria kushauriana na wizara ya elimu hapa Tz ili waanzishe mtaala wa somo la kifaransa kwa shule za msingi kwa kigezo kuwa lugha ni jambo muhimu na ni vizuri vijana wetu wakaanza nao kujifunza kifaransa pia.
Sasa nashindwa kuelewa kama hili aliliongea kwa dhamira ya dhati au kutaka kufurahisha wale aliokuwa akiongea nao pale au sisi tulioko huku. Ukizingatia kuwa elimu yenyewe ya msingi hapa Tz ni mshikemshike, kuna sekondari za kata ambazo mpaka leo hazionyeshi dalili ya kutengemaa kwa mahitaji muhimu kama vile walimu, madarasa, madawati, maabara, vitabu etc. Sijui kama ameshafanya utafiti wa mahitaji ya kuanzisha somo la kifaransa katika shule za msingi ikiwemo walimu wa kufundisha somo hilo, vitabu nk...Wadau hebu tulijadili hili....