Kwa hili Stewart Hall, Hongera

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Taarifa nilizozipata toka Blog ya Bin Zubeiry ni kua kocha Mkuu wa Azam Stewart Hall amegoma kuwasajili wachezaji Nelson Lukong toka Cameron na Alan Watende Wanga kwa madai kua lazima wafanye majaribio, ili awaone. Huku wachezaji hao wakigoma kwa madai kua wao sio wakufunya majaribio.

Sterwart ameonesha ni jinsi gani alivyo na msimamamo, na nadhani hata kipindi kile anaondoka, alikua anepukana na huu uswahili. Kama nasi tungekua na mfumo kama huu, tungeondokana na magarasa kama KANU Mbiyavanga, Paschal Ochieng' na Daniel Akufo.

Naimani usajili wa dirisha Dogo msimu ujao, nasi tutaiga haka kamfumo.
 
Hall huwa anasepa na kurudi Azam kwa kuwa kuna figisu za Kibongo kutoka kwa uongozi.

Azam ililazimika kuwachukua wafitini wa Bongo Soka ili kukabiliana na hujuma nyingi kutoka kwa timu za Kariakoo, sasa jamaa wamekuwa pia wajasiriamali na kuingilia mambo ya kiufundi ya timu.

Hii aliisema mwenyewe mwaka juzi wakati akitupa mafunzo ya ukocha pale Chuo Kikuu Mlimani. Kufanya kazi kitaalamu kwenye mazingira yetu ni vigumu sana, hata Serikalini!
 

Hiyo ni picha ya jinsi walivyo viongozi wetu. afu huwa wanakuwa kama hawajaenda shule. sijui wanakuwa wamesoma wapi au ni makusudi
 
Hiyo ni picha ya jinsi walivyo viongozi wetu. afu huwa wanakuwa kama hawajaenda shule. sijui wanakuwa wamesoma wapi au ni makusudi

"Kama hawajaenda shule" ni kauli ya kibaguzi na ya kijinga. Mpuuzi ni mpuuzi bila kujali amesoma, hajasoma, masikini, tajiri, maarufu, mwanasiasa na mengineyo.

Waliosoma wengi ndio wameliangusha taifa, hakuna waziri wala katibu mkuu wa Wizara ambaye hajaenda shule. Tafakari hili kwanza!
 
Huyo stewart nae sio kocha bora si kila mchezaji anastahili majaribio, allan wanga si mtu wa kufanya majaribio azam kwa mtu anayefuatilia soka la africa amekua na msimu mzuri el merreick ya sudan ambao binafsi ni level ya juu kuliko azam, kuna sehemu za allan wanga kufanya majaribio na sio azam
 
Apendaye, chongo huita kengeza. Kama Hall ni kama anavyotakaswa, ni kipi kinachomfanya awe akirejearejea kwenye timu anayoijua haiendeshwi kitaalamu? Waswahili husema 'kugombana kutaka', Waingereza wao 'It takes two to make a quarrel' au 'it takes two to tango'. Sasa kama yeye hana tatizo, figisu zitamfikaje? Atagombanaje? Fikiri zaidi.
 

Labda kuna anachokihitaji kutoka Azam, nasikia mazingira ya Soka letu ni bora na rafiki kuliko ligi nyingi za ukanda huu. Jamaa alihapewa fursa pia kwenye Kituo cha Soka cha Serikali pale Kidongo Chekundu, akiwa kama Mkurugenzi, hii ilikuwa mwaka jana. Sijui ilikuwaje akarejea tena Azam.

Kinachoiangusha Azam ni kukubali kuiga mfumo wa fitina baada ya kufanya kazi kitaalamu kushindikana. Azam FC ni kati ya taasisi za Baharesa zinazofanya hovyo na kuendeshwa kifitina fitina.
 

'Pamoja na majibu mazuri' ya maelezo ya hapo juu, jambo moja linajionesha waziwazi: Stewart hana msimamo. Kocha mwenye msimamo hawezi kurejea katika timu ikiwa na kasoro zilezile alizoondokea mwanzo. Tena anafanya hivyo kutoka katika ajira zisizo na upuuzi kama huo, kama vile Sofapaka na Kituo cha Kidongochekindu. Wala anaporejea haonekani kufanya juhudi zozote za kuondokana na upuuzi uliomwondoa awali.
Kigezo shaihi cha kutojiamini kwa Stewart ni kukubali kumrejesha Wanga bila ya hayo majaribio aliyosisitiza (chanzo: Bin Zubeiry Blog) na hivyo kumwangusha hata huyo aliyeanzisha mnyororo huo. Kama si unafiki wa waandishi wa habari, tukio hilo lingebeba vichwa habari viliyojaa bezo na kebehi: 'Stewart aufyata kwa Wanga', 'Azam yageuka nguzo ya chumvi, yageuka nyuma kwa ajili ya Wanga', 'Stewart alamba matapishi yake', n.k.
Licha ya hayo, utamwitaje kocha mwenye mzunguko huu ndani ya miaka michache: Zanzibar Heroes, Azam, Sofapaka, Azam, Kituo cha Kidongo Chekundu, Azam?
 
Hii ya majaribio majaribio waga inaponza... Arsene Wenger alimkosa hv hv ibrahimovic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…