Kwa hili tatizo la umeme Mama hasikii kilio cha wanaye

Kwa hili tatizo la umeme Mama hasikii kilio cha wanaye

Umeme umekuwa shida kuu hapa nchini, kila kona ni vilio kutokana na uhaba wa umeme.

Mama hasikii kilio cha wanae, tumekuwa watoto yatima ingawa tunaye mzazi.

Nani atakuja kusikia kilio cha watanzania kutokana na uhaba wa umeme?
kwa taarifa yako hakuna tatizo ambalo mama halioni,anaona kila kitu,na juhudi anazofanya ni kubwa sana kurekebisha na kutatua hayo matatizo,elewa nchi ina matatizo mengi,na uwezo wa kifedha sio mkubwa,tuvumilie tu
 
Si tunawachekea hawa wapumbavu, hapa hata sijaamka umeme washakata!
 
Wanasema Julias Nyerere hakuna transmission line na umeme upo tuu na hakuna pesa za kuweka line hivi hii inaingia akilini? na Mtera nasikia kinu kimoja kimetumbukia majini sijui habari hizi kwetu sisi zinatusaidia nini.
 
Sasahivi Kama umeme haujakatika unaona kama ni zawadi fulani .
 
mama anachakarika si mchezo ndugu yangu

itoshe kusema huyu mama ni kiongozi mchapa kazi haijawahi kutokea
Anachakarika kivipi. Mimi sioni kama anachakarika bali ameuchapa usingizi mzito.

Ni JPM tu alikuwa na uchungu na maisha duni ya watanzania, ndo maana wakati wote wa utawala wake hakukuwa na shida ya umeme, hakukuwa na vibaka mitaani, hakukuwa na ubabaishaji katika ofisi za umma, vitendo vya rushwa vilipungua sana nk. Kwa sasa hali ni mbaya kuliko wakati mwingine wowote ule.

Lakini Mungu ni mkubwa zaidi. Ipo siku tutapata Kiongozi anayejali shida za wananchi wake.
 
Umeme umekuwa shida kuu hapa nchini, kila kona ni vilio kutokana na uhaba wa umeme.

Mama hasikii kilio cha wanae, tumekuwa watoto yatima ingawa tunaye mzazi.

Nani atakuja kusikia kilio cha watanzania kutokana na uhaba wa umeme?
Ukitaka mama afanyaje ili uamini anasikia!?..habari za bwawa la mwalimu Nyerere na mgao kuisha huwa unalisikia!?..unafuatilia kinachoendelea huko bwawani!?
 
Back
Top Bottom