Kwa hili tukio polisi Mwanza wanapeleleza nini?

Kwa hili tukio polisi Mwanza wanapeleleza nini?

Tueleze vizuri walifanya kosa gani?
Kuna kijana dalali aliletewa milango atafute wateja.Ni dalali maarufu sana eneo hilo.Yule marehemu aliyepigwa mpaka kufa ndio alimletea. Kwa hiyo alikutwa na mlango ambao unadaiwa ni wa wizi.Ila pale kata kulikuwa na mwanajeshi ambae alikuwa ameibiwa Tv. Yeye akadai hawa ndio wezi wake. Akaanza kumpiga na magongo yule aliyeleta milango akishirikiana na migambo.Baadae tukapigiwa simu ofisi ya kata wamefunga milango wanawatesa humo ndani waseme Tv ipo wapi. Watuhumiwa walikuwa wanne.ila mmoja alifariki.Ila sisi tulijua kwa kuwa wako katika mikono salama ya mtendaji watapelekw polisi.lakini walipigw na kuteswa.mmoja alifariki na mwingine alig'olewa jino.
 
Kibaya zaidi mtendaji alifanya ofisi yake kama mahakama.na hata mpelelezi pale kirumba aliandika marehemu amepigwa na wananchi wenye hasira kali.kaulize kata ya kahama hata mtoto mdogo anajua juu ya tukio hili.
 
Hao wahuni ndio majambazi wewe ulikua unatakaje apo ..ata hospitali wagonjwa huwa wanakufa
Ilikuwa ni kwenye mkutano unaendelea...ni madogo tu hivi bangibangi wakawa wanapita pale...wakaanza kuporomosha matusi na lugha chafu....wananchi wakaona dharau kwao na kwa mwenye kiti...kipigo kikafuata...kuna baadhi walitumia silaha ndo hasa kilichofanya washkaji wakate moto.... Katika mazingira ka hayo ni lazima wakwanza kutiwa mbaroni awe mwenyekiti.... Mi sikuwepo eneo la tukio ila nilipata taarifa.... Nilikuja kuthibitisha siku za baadaye nilipokutana na wahuni wengi wamebeba mwili wa mwenzao wanaelekea maraloni....inaonekana hata wananchi wenyewe hawakujihusisha na mazishi coz walikuwa wahuni tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibaya zaidi mtendaji alifanya ofisi yake kama mahakama.na hata mpelelezi pale kirumba aliandika marehemu amepigwa na wananchi wenye hasira kali.kaulize kata ya kahama hata mtoto mdogo anajua juu ya tukio hili.
Akikamatwa mwizi ni vizuri apelekwe polisi kama itashindikana kumuua akiwa eneo la tukio wezi ni kama kansa haina budi kuondolewa dunuani, ata ndugu yangu akiwa mwizi siwezi mtetea kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamevunja sheria kuendesha mateso na kusababisha mauaji kihalifu.

Lakini kama mnahisi ameonewa, si mwizi
Ongozeni vuguvugu la kumtoa huyu mwenyekiti madarakani kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Ishu hapa ni ukiukwaji wa sheria na tararibu. Hamna anaejua kama ni mwizi au vipi? Maana ilitakiwa wapelekwe polisi.Alafu mahakamani ili sheria ifuate mkondo. Ila baaada ya kipigo kikali marehemu alianza kutamka maneno hovyo .Ili bidi akubali kama ni mwizi. Lakini hiyo Tv ya mwanajeshi inadaiwa hafahamu chochote kabisa.
 
Ni sawa lakini ni vyema wananchi wamtoe huyo mwenyekiti ili uchunguzi uende vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao Wahalifu wao wametenda kosa gani? maana mimi hapa ndio huwa nabaki njia panda.

Mwezi uliopita Mwenzangu/jirani yangu alipata tatizo la kuvamiwa, walivyoruka geti kuvunja grili mpaka kuingia ndani mpaka sasa hivi hajui.

Mke wake amesafiri na Jamaa amebaki mwenyewe, sasa akawa anaweka godoro sebuleni ili asikilizie usalama huko nje, ingawa siku ya kufa Nyani miti yote huteleza...ametuamsha saa kumi kasoro jamaa wakiwa wameshakamilisha tukio...Jamaa alikuwa kama amechanganyikiwa kwani Mtoto wa Mama yule hakuwahi ku experience tukio kama hilo tangu amezaliwa.

Ni wiki inaenda ya tatu sasa tangu tukio Jamaa ameikimbia nyumba anaishi kwa Ndugu zake Mjini huko, anakuja mara moja moja anachekicheki anaishia...cha ajabu Gari ilikuwa hapo nje wala hawakuigusa.

Tulienda Polisi usiku ule,ilishafika saa kumi alfajiri kwenda kumi na moja hivi... yaani tuliona Polisi wanachukulia mambo kirahisi sana, hawakujali sanasana wakaanza kuturudishia lawama kwamba kwa nini tumeruka vituo vyote tukaenda mpaka central, pia wakasema kama hatujui vitu vyote vilivyoibiwa hawafungui ripoti..tuliondoka pale tumefura hasira tukaishia zetu maana Jamaa nae alikuwa harudi tena huku Mtaani anabaki mjini kwa ndugu zake....kwa hiyo suala la ripoti likawa limetoka hilo.

Kwa muda sasa kila mara nimekuwa najiuliza hivi ni Binaadamu wa aina gani hawa wanaosubiri Mwenzao afanye kazi yake halali, ajikusanyie mali zake na Mkewe wao waje waingie wachukue tu? maana Jamaa huwa anaondoka saa kumi na mbili na nusu alfajiri na kurudi saa moja jioni/mbili kasoro kila siku, na mara moja moja jpili pia huenda kazini.

Jamaa anatia huruma sana, alipunguzwa kazi mwaka jana mwishoni, baadae akapata kazi nyingine ila mshahara huku ni nusu ya aliokuwa anaupata awali...hivyo gharama zimemuelemea kodi ya nyumba na Mlinzi a.k.a Masai ikawa mzigo, baadae ilibidi Masai aondoke tu baada ya malipo yake kuwa yanasuasua.

Ukiongea na Wanazengo huku kitaa wanasema Polisi huwa wanapita pita patrol ila baadae wanakuwa chimbo mahali Kitaani wanachapa zao ulabu.

Yaani picha niliyopata pale Central ni kuwa hawa jamaa hawana msaada, yani wapo wapo tu wamekata tamaa ya kazi, hawana ushauri wowote...wana ku treat kama vile "umevamiwa..kwa hiyo sisi tufanyeje"

Hizi stunt za kwenye Runinga ndio wanaziweza, ila huku chini ni tia maji tia maji.

Nimejiuliza hivi kama tungefanikwa kuwaotea wale Wezi tukiwa na silaha tungewaacha hai kweli? au kama wangekamatwa baadae usiku ule na waliowakamata wakatuita na kutuuliza "hawa wapelekwe Polisi au tumalizane nao hapa hapa?" hivi tungejibu nini?

Juzi kuna redio moja walimuhoji Kamanda wa Polisi kutokana na matukio kadhaa yaliyojitokeza eneo moja huku Arusha, Mtangazaji alionyesha kutokuridhishwa na majibu yale, ofcoz yeye alisema 'Wasikilizaji hawajaridhika' lakini kivyangu vyangu huku nilipo nilijisemea hapo ndio amemaliza Mzee...business as usual.

Najua Polisi utetezi wao utakuwa wao wapo Wachache blah blah, lakini usalama wa raia bado ni jukumu lao la msingi, Polisi wajiongeze, waongeze ubunifu..kuna teknolojia sio lazima wawe wengi.

Hivi kwa nini moja ya masharti ya hawa Wenyeviti wa mitaa isiwe kuji commit kwamba watahakikisha Wakazi wao wanaishi kwa amani?

Hofu yangu hawa Wahalifu wakishakamatwa ni sisi tena tunaanza kuwatetea, kwa upande mmoja hatutaki kufanyiwa uhalifu lakini hatutaki Wahalifu waangamizwe kisa tu ni ndugu au Majirani zetu.
 
Attachments

  • 1673304_6.jpg
    1673304_6.jpg
    107.3 KB · Views: 10
Back
Top Bottom