Kwa hili UDSM mmetia aibu

ashukur

Senior Member
Joined
Jan 23, 2013
Posts
110
Reaction score
15
Hivi karibuni vyuo mbalimbali vimekuwa vikitoa majibu ya maombi ya watu waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za post graduate yaani postgraduate diploma, masters na PHD. Chuo kikuu cha mlimani kikiwa kimoja wapo. Cha kushangaza ni kwamba kumekuwa na tangazo la kupanda maradufu kwa ada yaani tution fee kiasi cha kukatisha tamaa. Fikiria kozi za Arts zilizokuwa zikilipiwa 2.8mil sasa ni 6.35 hadi 8.0 mil ongezeko ambalo halijalishi unauwezo kiasi gani. jambo la ajabu zaidi ni pale ambapo mpaka watu wanajaza form hakukuwa na mabadiliko yoyote hvyo basi kuwa umejiandaa na hy 2.8 ambayo ungelipa kwa mafungu. Sasa kama hy tu ilikuwa ngumu jamani leo 6.3 mil itawezekana kweli?! Na hiki ndo chuo cha umma na ndo kimbilio la masikini! Nachelea kusema kwamba tabaka tawala na lile tawaliwa au la wenye nacho na wasionacho litakuwa kwa kasi ya ajabu miaka 5 ijayo. Tutafakari jamani je 2tafika kwa hali hii?!
 
1.Master sio kozi muhimu. Kama umeshapata bachelor inatosha.
2. Serikali imekataa kutoa OC kwa ajili ya kuendesha shughuli za chuo. Hii ndio sababu kuu ya ongezeko la gharama za masomo.
 
mmmmmmhhhh...wanataka maprof wabak mukandara,maboko,mugaya wengine tuuckie tu huo u dr,
 

Kwani ukisoma ndiyo utakuwa na HELA au Mtawala?
 
1.Master sio kozi muhimu. Kama umeshapata bachelor inatosha.
2. Serikali imekataa kutoa OC kwa ajili ya kuendesha shughuli za chuo. Hii ndio sababu kuu ya ongezeko la gharama za masomo.

Kama hiyo ni sababu ya msingi kwanini vyuo vingine hawajapandisha bei kwa pupa kiasi hicho
 
Kwa sie wa-CoET mambo sio mabaya kwa masters
 
Hilo la ada ni moja, ajabu la pili ni pale walipokua wanabip uwapigie, au kutuma sms kukwambia "this is from UD conserning ur application for masters, plz call back".
Serious? Institution kama hii applicant anaombwa kupiga yy?
 
Kwani ukisoma ndiyo utakuwa na HELA au Mtawala?

inaonesha elimu bado haijakukomboa! we ushaona wapi watu wanaongozwa na mbumbumbu?! inawezekana huoni faida ya shule na huenda wewe ni mmoja wa wale wanaopigia debe shule za kata wakiona hakuna haja ya kuwa na shule za maana zenye maabara, walimu na vitabu. sio kosa lako
 
Hilo la ada ni moja, ajabu la pili ni pale walipokua wanabip uwapigie, au kutuma sms kukwambia "this is from UD conserning ur application for masters, plz call back".
Serious? Institution kama hii applicant anaombwa kupiga yy?

hahhahahahhahha!!
 
We vipi,Kwan lazima usome udsm?nenda hata saut,ruco,tumain,mzumbe,ifm,teku etc.shida yako we si upate mastaers tu au?
 

Mbona Rais wetu hana Master wala PHD na mambo yanaenda vizuri tu. Mkwawa haukufika Hata la 1 lakini ni bora kuliko viongozi wetu tulionao, Mbona mifano ipo mingi tu. ACHA USHAMBA WEWE? ELIMU siyo kuwa na HELA wala kuwa KIONGOZI.
 
Nilishashauri tena kuwa kama mtu ana malalamiko aandike barua ya wazi kwenye gazeti, au kupeleka malalamiko yake kwa mamlaka zinazoweza kumsaidia badala ya kulalamika humu mwisho utaishia kunawa tu.

Kingine si kwamba nawatetea UDSM bali ni kukumbusha tu kwamba hapo mwanzo gharama za postgraduate studies pale UD haikua tofauti na garama za Undergraduate degrees na za undergraduate hazikua tofauti na za sekonadary za kawaida siyo za wenyenazo. Hata sasa baada ya kushoot sana bado ni ndogo maana hiyo 6.35 ni kwa miezi 18 na 8.00 kwa miezi 24 yaani mpaka umalize masomo yako ya masters. Kuna mleta mada alishaleta hii kitu tena na nikamshauri kuwa pamoja na hayo yote hakuna chuo chenye ada nafuu kama UDSM hapa tanzania katika level hiyo ya postgraduate.

Nadhani cha kulalamikia hapa ni timing; kwamba watu wameshafanya applications wakiamini ada ni kiasi fulani alafu mwisho wanapokaribia kuingia wanapewa ada nyingine. Kwa hilo kuna sababu ya kuandika barua kwa mwenyekiti wa baraza la chuo, au kwa waziri au kwa rais au kwa wale wanaoamini kila kitu ni siasa wapeleke kwa wabunge wao au viongozi wao wa vyama wawapigie kelele ili angalau wapate punguzo kwa sasa miaka mingine ndiyo ipande.

Swala la kusema sijui kina maboko walisoma kwa garama nafuu hapa ni siasa tu maana wao ilikua ni scholarship kusoma nnje, au kusomeshwa na serikali mpaka mwisho sasa ukisema hilo lirudi utajikuta darasni mwenyewe, wengine wote tutabaki mtaani hatuna pa kwenda.
 

hebu fafanua na hili la huyu mdau hapo juu..........
Hilo la ada ni moja, ajabu la pili ni pale walipokua wanabip uwapigie, au kutuma sms kukwambia "this is from UD conserning ur application for masters, plz call back".
Serious? Institution kama hii applicant anaombwa kupiga yy?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…