Hivi karibuni vyuo mbalimbali vimekuwa vikitoa majibu ya maombi ya watu waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za post graduate yaani postgraduate diploma, masters na PHD. Chuo kikuu cha mlimani kikiwa kimoja wapo. Cha kushangaza ni kwamba kumekuwa na tangazo la kupanda maradufu kwa ada yaani tution fee kiasi cha kukatisha tamaa. Fikiria kozi za Arts zilizokuwa zikilipiwa 2.8mil sasa ni 6.35 hadi 8.0 mil ongezeko ambalo halijalishi unauwezo kiasi gani. jambo la ajabu zaidi ni pale ambapo mpaka watu wanajaza form hakukuwa na mabadiliko yoyote hvyo basi kuwa umejiandaa na hy 2.8 ambayo ungelipa kwa mafungu. Sasa kama hy tu ilikuwa ngumu jamani leo 6.3 mil itawezekana kweli?! Na hiki ndo chuo cha umma na ndo kimbilio la masikini! Nachelea kusema kwamba tabaka tawala na lile tawaliwa au la wenye nacho na wasionacho litakuwa kwa kasi ya ajabu miaka 5 ijayo. Tutafakari jamani je 2tafika kwa hali hii?!