Kwa hili wanawake tunakosea sana

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Unaamua kuwa na mchepuko,unamficha mume wako kwa miezi kadhaa bila yeye kujua

Unanogewa na penzi la mchepuko,na mapenzi kikohozi taratibu inaanza kufahamika una mwanaume mwingine

Mmeo anakubana kuhusu huo usaliti,unaona ni kero unaamua kumwambia mchepuko akutoe akupangishie,utoke kwa mume wako na ikumbukwe una watoto na mume wako

Mchepuko anakupangishia na unaondoka na watoto wako wawili,mchepuko unakushawishi ubadilishe majina ya kuzaliwa ya watoto,unaenda Rita ,unabadilisha majina yanakuwa ya mchepuko

Baada ya miaka 2,mchepuko anaoa binti au mwanamke mwingine ambaye hajawahi kuolewa anakuacha kwenye mataa na watoto wako,unaanza kulia mitaani unaomba msaada usaidiwe urudi kwa mume wako wa awali

Muda mwingine wanawake hatuna akili ya kufikiria

Ni kisa cha kweli kimetokea mtaani kwetu

Na kumbe wanaume ambao waliwahi kuoa wakashindana na wake zao,wanaongoza kuwadanganya wanawake waliomo kwenye ndoa,na ndio wanaongoza kuchepuka na wake za watu
 
Unajua cutelove haya mambo ni mazito. Huyo ndio yule mwanamke mpumbavu ambae Biblia huwa iliandika.

Hata kama unacheouka jali familia yako sana sana.. huyu kaenda mzima mzima.. mambo yeharibika anaomba msaada.

Hivi anadhani huyo mume atamuelewa?
 
Unajua cutelove haya mambo ni mazito. Huyo ndio yule mwanamke moumbav ambae Biblia huwa iliandika.
Hata kama unacheouka jali familia yako sana sana.. huyu kaenda mzima mzima.. mambo yeharibika anaomba msaada. Hiv anadhani huyo mume atamuelewa?
Kwa kweli kaka angu,ni hatari sana
 
Men have no expiry date, Mwanamke akicheat huamisha moyo na kila kitu huko they don't use brain. Wanasahau

kwamba wao huweza kupoteza urembo wao ndani ya muda mfupi kutokana na uzazi au umri compare na wanaume,

Alifikiri kuhama kwa mbwembwe ni kukimbilia nchi yenye maziwa na asali na kumwona mmewe hana jipya ndo ujanja

et leo anatafuta msaada wa kumrudisha kwenye chaka la kujifichia ili apate mpenzi mwingine, du!,,
 
Kila dhambi ina mshahara tunalipana hapa hapa duniani
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Sijui hata uliwaza nini wakati unaandika hivi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ex darling si nimeupokea ushauri jamani, nisiache mbachao kwa msala upitao.
 
Inasikitisha saana kwa kweli!

Mwanamke, ukitumia akili na fedha kiasi kumhadaa; atakubali hata kwa mambo yasiyowezekana katika dunia hii.
Hasa akikolezwa na penzi la nje.

Sasa hapo ndipo anayaona makosa yake.
 
Reactions: THT
alafu unasikia," ...yani wanaume wa siku hiziii...ni wahuniiiiii......"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…