livewise1
JF-Expert Member
- May 25, 2019
- 837
- 967
Nimestuka yaani the same scenario imetokea mtaani kwetu mpaka nikahisi tunakaa mtaa mmoja niniii....ila tofauti imekuja kwenye idadi ya watoto...huyu hapa mtaani kwetu ana mtoto mmoja ila pia hajabadilisha ubini wa mtoto (jina la baba mtoto)Unaamua kuwa na mchepuko,unamficha mume wako kwa miezi kadhaa bila yeye kujua
Unanogewa na penzi la mchepuko,na mapenzi kikohozi taratibu inaanza kufahamika una mwanaume mwingine
Mmeo anakubana kuhusu huo usaliti,unaona ni kero unaamua kumwambia mchepuko akutoe akupangishie,utoke kwa mume wako na ikumbukwe una watoto na mume wako
Mchepuko anakupangishia na unaondoka na watoto wako wawili,mchepuko unakushawishi ubadilishe majina ya kuzaliwa ya watoto,unaenda Rita ,unabadilisha majina yanakuwa ya mchepuko
Baada ya miaka 2,mchepuko anaoa binti au mwanamke mwingine ambaye hajawahi kuolewa anakuacha kwenye mataa na watoto wako,unaanza kulia mitaani unaomba msaada usaidiwe urudi kwa mume wako wa awali
Muda mwingine wanawake hatuna akili ya kufikiria
Ni kisa cha kweli kimetokea mtaani kwetu
Na kumbe wanaume ambao waliwahi kuoa wakashindana na wake zao,wanaongoza kuwadanganya wanawake waliomo kwenye ndoa,na ndio wanaongoza kuchepuka na wake za watu
Ila jamaa hajafanya ajizi mkewe alivoondoka tu (baada ya miezi 3) akaleta pini moja kali mpaka aibu.
Mchepuko kamtelekeza mke wa jamaa juzi kati tu.
Hatari sana!! Saivi vijana wanajichapia tu ili apate matumizi walau.