Kwa hili Wanayanga hatukubali lazima Wananchi tuambiwe ukweli

Rajab_Omar

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2016
Posts
16,482
Reaction score
27,182
Salaaam Wananchi Wenzangu,

Kwa masikitiko makubwa timu yangu Pendwa ya Wananchi Dar Young Africans imesajili wachezaji wapya lakini jezi wanazovalishwa ni za Zamani.

Kwa nini Eng. Hersi Saidi ambaye mara nyingi anatuhumiwa kwa uongo alituahidi kuwa kwenye kilele cha siku ya Wananchi zitatambulishwa Jezi mpya lakini hatimae akatambulishwa Komando Hermonize badala ya Jezi mpya?

Watani zetu Simba walituonya mapema kuwa GSM hawatotoa Jezi mpya mpaka Stock za zamani iishe lakini tuliwabishia, ona sasa tunavyoumbuka.

Eng. Hersi saidi Mimi nikiwa Mwanachama halisi wa Timu yangu pendwa ya Yanga naomba utueleze Wananchi kuhusu mustakbali wa Jezi mpya! Kuna Mtu aliumislead uingozi akawaambia kuwa Mashabiki wa Yanga nchini wapo 20M tukachapisha Jezi 5M hatimae zimenunuliwa only 115K.
Mzigo wa 4885 upo Stoo unasibiriwa umalize ingawa mategemeo ya kumaliza hakuna.

Haiwezekani Simba avae Jezi mpya halafu sisi tuvae Used.


 
mkuu timu yangu yanga mimi naijua ,haina tofauti na chelsea ya pale London, wenyewe wanajiona wanashindana na timu kubwa nyingine kama Liverpool, Manyumbu na Arsenal wakati kiuhalisia kwa sasa hata Tottenham wamewaacha kwa mbali sana,

alichofanya GSM ndio kama alichokifanya Roman Abromovich,

GSM wamechukua pesa za kununulia jezi wamenunua wachezaji wakati Abromovich ametumia pesa za kujengea uwanja wa timu ananunua wachezaji matokeo yake kitimu kinamiliki uwanja kama kilabu cha Gwambina,

Wenzao Arsenal walipitia kipindi kigumu sana wakati wanajenga uwanja wao ndio maana wapo hapo leo hii maana walipitia kipindi cha madeni yaliyowalazimu kushindwa kucompete na vilabu vingine katika soko la usajili wa wachezaji na kununua cheap players lakini hawakuyumba sana,
Siku wao watapoanza kuboresha miundombinu ya klabu iendane na vilabu vingine basi hii timu itashuka daraja,amini hivyo,

Tukirudi katika klabu yangu ya Yanga mambo ni yaleyale kama suala la uboreshwaji wa uongozi wa klabu pamoja na miundombinu ya klabu yetu ikiwemo ujenzi wa Arena kama ya wenzetu Simba ukifanyika basi tujiandae na aibu kubwa sana,maana itatubidi tutumie local players ili kusave resources zitumike katika maboresho ya klabu na hapo ndipo tutapigwa na gap na majirani zetu Simba maana wao kwa muda huo watazidi kujichimbia kileleni,hivyo ili tuendelee kuwa vifua mbele kama tumepigwa ngumi la mgongo inabidi tukubali kuishi pale matopeni, tukubali kuvaa majezi ya zamani , ambayo hayo hayo ya mazoezi hayohayo ya mechi,.

Daima mbele ,Nyuma mwiko
 
HUNA jipya
Utakagua na chupizaooooo kama mpyaaaa
SIMBA AIBU
MaliAzaneni na moo kwanza
 
Waandishi wenu na wachambuzi ni utopolo kama ninyi wenyewe yanga.Hao ndio waliwapa data za uongo kuwa mna mashabiki milioni 20.Msipoangalia mtaweka mipango hewa kwa takwimu za mihemko.
Kwa vile hamtaki kushirikisha akili,shauri yenu na hizo jezi zenu ambazo hazijanunuliwa.

Nina ushauri mzuri lakini mjue mi ni Simba damu
 
Utopolo saizi wanajaa hawewezi hata kuhoji
 
yaani wewe ni mshamba sana,arsenal ya nane uifananishe na timu iliyopo top 4?na hapo umechambua kabisa kwa chuki zako kwa chelsea.
 
HUNA jipya
Utakagua na chupizaooooo kama mpyaaaa
SIMBA AIBU
MaliAzaneni na moo kwanza

Hapa ndiyo sisi Yanga tunapofeli, Tunakomaza mishipa ya Shindo kumshughulikia MO wakati ya kwetu kwa Wananchi yanakwenda Ndivyo sivyo.

Ukichunguza kwa makini utagundua MO hana mgogoro wowote na washabiki pamoja na Wanachama wa Simba, ukweli mchungu ni kwamba Washabiki wote wa Simba wanampenda na kumkubali MO wala hawajali kuhusu hizo 20B.

Waliokomaa na kutengeneza mgogoro hewa ni sisi Washabiki wa Yanga kwa kumdai MO 20B utadhani akizitoa na sisi Yanga tutagaiwa.
Na yule Kigwangwala kilichomuumiza ni kukoseshwa mkopo wa Bodaboda tu kutoka kwa MO.
 

Sisi Washabiki wa Yanga ni kweli huwa tunakosea sana kwa tabia yetu ya kuamini kila tunachoambiwa
 
yaani wewe ni mshamba sana,arsenal ya nane uifananishe na timu iliyopo top 4?na hapo umechambua kabisa kwa chuki zako kwa chelsea.
hivi duniani kuna mshamba atakayeweza kuvunja rekodi yenu nyinyi kina ngosha?khaaaaaaaaaaaa
 
Naamini sasa,hiyo hofu yako imekwisha maana leo,yanga wanazindua jezi mpya rasmi,tujifunze kuwa wavumilivu,tuache kutoa shutuma,bila ya kuwa na ushahidi
 
Eti na wewe Yanga
 
Mwanzo ulivyoleta mada nilidhani una hoja ila sasa hivi naona umekaa kishabiki zaidi.

Nimeona bora kupuuzia tu.
 
Una maanisha Hon. kigwa bado anakisununu cha bodaboda!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…