Li ngunda ngali
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 707
- 2,572
Moto chiniTumekusikia
View attachment 3080807
na huo ndio ungwana,Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Nachukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa KUTIMIZA WAJIBU wake kwa kuhakikisha Tanzania nzima inao mtandao wa mwanga wa nishati ya umeme karibu Miji na Vijiji vyote.
Tunaweza kuona ni jambo dogo lakini kwa wenzetu hiyo ni habari kubwa na maendeleo ya kupigiwa mfano!
Leo hii Nchi yetu yapo mambo baadhi tunaweza kujivunia kama Taifa pasipo kujali Itikadi zetu. Mtandao mpana wa barabara za lami na mtandao wa umeme hadi vijijini ni mambo yanayotupasa tujivunie kama Taifa.
Kwa mara nyingine, naipongeza Serikali kwa kutimiza wajibu wake kwalo.
TANESCO
Hapa sijaelewa. Ndiyo kusema pope kalewa mvinyo?Tumekusikia
View attachment 3080807
0ngea mambo mengine suala la umeme bado sana, asilimia kubwa umeme umefika ila asilimia kubwa sana watu hawana umeme na wahitaji ni wengi sana, serikali imeweza kufikisha umeme sehemu za mijini na sehemu yaliko makao makuu ya kijiji au vijiji na sehemu ambako kuna huduma za kijamii kama shule za sekondari au vituo vya afya lakini vitongoji vingi sana umeme hamna, nakupa mfano hai,kuna vitongoji vingi sana vimo ndani ya km zisizo zidi mbili au tatu kutoka yalipo makao makuu ya wilaya au miji lakini hakuna umeme. Mbali na mijini, ni wilaya moja tu ambako hapa Tanzania umeme umefika kwa zaidi 97 %Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.