Kwa hio unataka kuniambia ni roho chafu na dhambi zangu ndio chanzo cha majanga yangu huku anaenihubiria amenunua gari kali kwa kutumia sadaka zangu!

Kwa sababu yeye ndiye kamtaja Mungu, mimi sijamtaja.

Anayeanzisha dai kwamba kuna Mungu ndiye mwenye burden of proof.kuthibitisha Mungu yupo kweli.
Mi nafikiri bado hujaufungua ufahamu wako kujua undani wako! Unatumia few details kuendelea kudanganya watu na pengine we kudanganywa kuwa MUNGU hayupo!? MUNGU yupo sana tuu... Ni vile hujui Njia sahihi ya kumfikia na si pekeako wengi huishia ku assume hayupo kwa7bu hawana Njia ya kumfikia Wala kumjua
 
Hujathibitisha Mungu yupo, unahubiri Mungu yupo.

Unapoanza na "mimi nafikiri..." tayari umeshatuonesha hutuambii habari za impartial facts, unatuambia unachofikiri wewe tu, fikra zako tu ambazo hazina uthabiti.

Thibitisha Mungu yupo, acha kutuambia unachofikiri tu.
 
"Mtu ukihitaji uthibitisho inabid useme unahitaji uthibitisho aina gani?"
 
"Mtu ukihitaji uthibitisho inabid useme unahitaji uthibitisho aina gani?"
Ninahitaji uthibitisho:-

1. Ulio logically consistent (habari yoyote yenye logical inconsistency si uthibitisho).

2. Unaoweza kuwa verified independently (hapa kwa mfano habari za "personal experience" zisizoweza kuwa verified independently si uthibitisho).

3. Usioweza kuwa contradicted ( habari za Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anayeweza kuwa contradicted na Epicurean oaradox/problem of evil si uthibitisho).

Majaribio yote ya kumuelezea Mungu hayapo logically consistent, hayawezi kuwa verified independently, na yanaweza kuwa contradicted.
 
Mpaka sasa hakuna mtu aliyeweza kuthibitisha Mungu yupo.
Mkuu unaweza kutuambia origin ya mwanadamu imetokea wapi?
Kama unapinga uwepo wa Mungu, bhas utuambie chanzo cha huu ulimwengu ni kipi
 
Mkuu unaweza kutuambia origin ya mwanadamu imetokea wapi?
Kama unapinga uwepo wa Mungu, bhas utuambie chanzo cha huu ulimwengu ni kipi
Naam, tunaweza kwenda kote huko.

Kimsingi unataka kujua kama jibu la Mungu si sahihi, jibu sahihi ni lipi?

Lakini awali kabisa, unaweza kukubali kwamba, katika kutafuta jibu sahihi, ukijua mambo fulani ya msingi kuhusu jibu sahihi linatakiwa liweje, unaweza kujua jibu fulani si sahihi hata kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi?

Mfano, tunafanya hesabu za base ten math. Unaambiwa utafute 10 - 5 = ?.

Unajua hii ni hesabu ya kutoa. Hujui jibu, lakini unajua kwamba jibu linatakiwa liwe dogo kuliko 10. Maana hesabu yenyewe ni ya kupunguza 5 kutoka 10.

Hivyo, mtu akikuambia kuwa 10 -5 = 15, hapo utajua tu kuwa hiki jibu la 15 si sahihi.

Kwa sababu 15 ni kubwa kuliko 10 na jibu ka 10 - 5 linatakiwa kuwa dogo kuliko 10.

Hivyo hapo hata kabla hujajua jibu la 10 - 5 ni nini, ukipewa jibu la 10 - 5 = 15, utaweza kujua hili jibu si la kweli.

Unakubaliana nami kwamba mtu anaweza kujua jibu hili si sahihi hata kabla hajajua jibu sahihi ni lipi?
 
Daah! Bro Kiranga! Unaishi kwenye utaratibu wko wa kisayansi!! Duniani hapa si kila mtu anaishi kweny maisha unayoyaona kwa macho! Halafu uthibitisho unaotaka wew kwa Njia unazotaka wew! Hizo procedure za utafiti ni za kwao hata wew waweza kuwa na procedure zako.... Usilazimishe upate uthibitisho kwa Njia yako wew
 
Kwanza kabisa, huo si uthibitisho ninaoutaka mimi.

Huo ni uthibitisho wa kimantiki katika kutafuta ukweli.

Umekuwa hivyo hivyo kabla mimi sijazaliwa na utaendelea kuwa hivyo nikifa, usiuite uthibitisho wangu. Ukiuita hivyo unakuwa unaudogosha kama ni uthibitisho wangu tu, nimeweka masharti yangu mimi tu.

Hiyo ni mantiki ya ukweli.

Umeelewa?
 
Daah kwahio wew unataka uthibitisho unaotaka wew!!πŸ˜…πŸ˜…...! Labda tu nikusaidie ndugu:
Wew umerelay kweny scientific research!
" Usichofahamu ni hiki, hizo stages za research ni mtu alizitunga tena mtu Kama wew" hivyo Kuna critics kibao kwenye procedure zake:
Nikusaidie namna aina tofauti za uthibitisho labda:
1. Uthibitisho wa taaluma
2. Uthibitisho wa kikawaida(common sense)
3. Uthibitisho wa kiroho (spiritual power)
4. Uthibitisho wa kihisia (kutumia milango ya fahamu) instinct.
5. Uthibitisho wa kiuwepo wa jambo Fulani
Ukibase kweny uthibitisho kwa kutumia mfumo mmoja wa uthibitisho wew bado hujapanua ubongo wako kweny kufikiri! We still seek GOD who created all this we see and we don't see! And the right way to reach him. Let's search for that kuliko kubisha with alot of English grammars kweny text zako.
....I stnd to be corrected..
 
Bado hujathibitisha Mungu yupo kwa njia yoyote.
 
Idadi ya wajinga ni kubwa mno hivyo lazima watumike kama daraja la wajanja kwenda kwenye mafanikio. Wajinga wa kwenye dini wapo hadi wasomi wakubwa. Kuna maprofesa, madokta na wasomi wengine. Nampongeza huyo Tapeli kwa kutumia fursa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…