Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Kumbe wamarekani wanayajua mapenzi kuliko sisi. Kumbe tena wako wazi kuliko sisi. Wako wazi kiasi cha kuwa na ndoa za mikataba. Wako wazi kiasi cha kuruhusu mahusiano ya jinsia moja! Kumbe wanaona mapenzi yetu yamejaa ububu. Kwamba mke/mume nizungumze nae na ikishindikana tuvunje mkataba. Kumbe watanzania wanaogopana kupashana ukweli kuhusu uwazi katika mahusiano, na ndio maana ukimwi hauishi. Kumbe wamarekani wanatupenda hivi? Wito wangu kwenu. Utakapoanza kutaka kuvunja ukimya na mwenza wako uanze na KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI...