Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Wana Jamvi,
Nipo Moshi baada ya kitambo kirefu cha kuhudhuria hili ambalo sasa tuliite tamasha la mbio za marathon la Kili Marathon.
Kwa hizi siku mbili za tamasha kuelekea kilele chake siku ya jumapili tarehe 23 Februari, kimsingi ni leo siku ninayoandika uzi huu. Hili tamasha limekuwa kitu kikubwa sana.
Nakumbuka, mbio za Kili Marathon kipindi zinaanza bahati nzuri nilikuwa bado nipo nyumbani Moshi, zilikuwa za kawaida tu zaidi tuliona wageni wengi wa ulaya ambao pia tulikuwa tumezoea kuonana nao mtaani wakiridi kwa ajili ya kushiriki mbio.
Lakini sasa kuna hadi siku tatu za bata na shangwe, sasa hivi sio tu wadau kuyoka Moshi na Arusha bali ni dunia sasa.
Tukirudi nyuma kidogo kuanzishwa kwa mbio hizi hakutengani na aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini Hayati Philemon Ndesamburo. Nakumbuka tulikuwa tunaenda kukata ticket pale hotel ya Keys leo ticket tunapewa kimfuko chenye vifaa kadhaa.
Naona tunaposherekea leo hii mafanikio ya mbio hizi tusiache kumkumbuka Hayati Ndesamburo ambaye naweza kusema ni moja ya waasisi wa mbio hizi.
Sina mengi zaidi ya kusema ahsante kwa.Hayati Ndesamburo aliyewezesha mbio hizi leo kufikia hapa, hakika hii ni zawadi kubwa aliyotuachia.
Royal Tour tuchomekee hapo pia. Mgeni nasema haya nikiwa tena nyumbani Moshi.
Wasalimu.