maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,345
- 15,851
Leo nimepigwa surprise ya hatari,nimetoka zangu job nikasema nipite millennium tower nikae Montana kusubiri foleni ipungue nishushe na one for the road...ila nikasema kwanza niingie ATM nizagamue cardless maana ATM card huwa sina, ajabu nafika sehemu ilipokua ATM nakuta peupe..nikahisi nimekosea..nikarudi tena nyuma nikaingia upya labda ntaiona..hola. Nikasema anyway labda wamehamishia ndani pembeni ya branch ngoja niende..napo hola.... He! Mbona na hata branch yenyewe haipo. Nikahisi nimekosea jengo.. bahati askari akawa anapita nikamuuliza kwani CRDB walihama?.. akanambia wamehamia Dar Village mall?..kama vp nenda makumbusho stand.. Mweh! . Nikabaki kushangaa ..ndio hadi kung'oa huduma ya ATM..au mligombana na landlord