Kwa hiyo eneo la Tanganyika Packers kamilikishwa rasmi Mwamposa? Serikali haitaki tena kufufua kiwanda cha nyama?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,120
Siku ya leo, Rais Samia kazindua rasmi hema (jengo?) la kanisa la Rise and shine (Kanisa la Mwamposa) kwenye viwanja vilivyokuwepo kiwanda cha Tanganyika Packers. Imeelezwa jengo (hema) hilo lina gharama ya zaidi ya bilioni 15.

Huenda ndio gharama za juu zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania kwa taasisi za kidini kumiliki. Hakuna kanisa wala msikiti uliowahi kuelezwa kujengwa kwa gharama kukaribia bilioni 15 hapa Tanzania. Na bila kumumunya maneno, ujenzi wa gharama hizo unaashiria kilichotengenezwa pale ni kitu chenye miundo mbinu ya kudumu katika eneo lile.

Lakini uzinduzi huo umezaa utitiri wa maswali, na vyema tukayajadili hapa ili kuweka wazi sasa ili huko baadaye isije ikaleta maneno, mivutano na kushikana masharti.

1. Je, serikali imeamua kummilikisha rasmi Mwamposa lile eneo?

2. Je, serikali imebadili matumizi ya eneo lile kutoka kuwa kiwanda kilichokufa au eneo la wazi la kutumiwa kwa matukio ya kupita na kuwa eneo rasmi binafsi la taasisi ya kidini?

3. Je, serikali imefuta uwezekano wa mtu au taasisi zingine tofauti na Mwamposa kutumia eneo lile kwa sasa au baadaye?

4. Kisheria lile eneo lilikuwa likimiliwa na nani, na matumizi ya sasa (kidini) yanamfaidisha vipi mmiliki?

5. Kwa hatua hizi za sasa, je inaashiria serikali haina tena mpango, mikakati au mawazi kuja kufufua kiwanda cha Tanganyika Packers?
 
Sisi tunajua kitu basi? Si ukamuulize mama yuko hapo magogoni kajaa tele?
 
Mwamposa ni agent wa serikali katika kupumbaza watu na kuisafisha CCM.

Ndiyo maana hata akiua watu huwezi kusikia kafungwa au kashitakiwa.

Ndiyo maana leo umeiona serikali katika jambo lake.

Huelewi wapi?
 
Siku ya leo, Rais Samia kazindua rasmi hema (jengo?) la kanisa la Rise and shine (Kanisa la Mwamposa) kwenye viwanja vilivyokuwepo kiwanda cha Tanganyika Packers. Imeelezwa jengo (hema) hilo lina gharama ya zaidi ya bilioni 15.

Huenda ndio gharama za juu zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania kwa taasisi za kidini kumiliki. Hakuna kanisa wala msikiti uliowahi kuelezwa kujengwa kwa gharama kukaribia bilioni 15 hapa Tanzania. Na bila kumumunya maneno, ujenzi wa gharama hizo unaashiria kilichotengenezwa pale ni kitu chenye miundo mbinu ya kudumu katika eneo lile.

Lakini uzinduzi huo umezaa utitiri wa maswali, na vyema tukayajadili hapa ili kuweka wazi sasa ili huko baadaye isije ikaleta maneno, mivutano na kushikana masharti.

1. Je, serikali imeamua kummilikisha rasmi Mwamposa lile eneo?

2. Je, serikali imebadili matumizi ya eneo lile kutoka kuwa kiwanda kilichokufa au eneo la wazi la kutumiwa kwa matukio ya kupita na kuwa eneo rasmi binafsi la taasisi ya kidini?

3. Je, serikali imefuta uwezekano wa mtu au taasisi zingine tofauti na Mwamposa kutumia eneo lile kwa sasa au baadaye?

4. Kisheria lile eneo lilikuwa likimiliwa na nani, na matumizi ya sasa (kidini) yanamfaidisha vipi mmiliki?

5. Kwa hatua hizi za sasa, je inaashiria serikali haina tena mpango, mikakati au mawazi kuja kufufua kiwanda cha Tanganyika Packers?
Hizi dini za vitabu zinatumika kuwapumbaza sana waafrika. Nchi za dunia ya kwanza zinawekeza kwenye sayansi na teknolojia, sisi kwenye maombi. Sioni ni kwa namna gani tutatoka kwenye mkwamo huu. Watawala hawana maono, wakishiba wao na familia zao inatosha. Waafrika tunaangamia, sio kwa kukosa imani bali kwa kukosa maarifa
 
1751757726867.png
 
Siku ya leo, Rais Samia kazindua rasmi hema (jengo?) la kanisa la Rise and shine (Kanisa la Mwamposa) kwenye viwanja vilivyokuwepo kiwanda cha Tanganyika Packers. Imeelezwa jengo (hema) hilo lina gharama ya zaidi ya bilioni 15.

Huenda ndio gharama za juu zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania kwa taasisi za kidini kumiliki. Hakuna kanisa wala msikiti uliowahi kuelezwa kujengwa kwa gharama kukaribia bilioni 15 hapa Tanzania. Na bila kumumunya maneno, ujenzi wa gharama hizo unaashiria kilichotengenezwa pale ni kitu chenye miundo mbinu ya kudumu katika eneo lile.

Lakini uzinduzi huo umezaa utitiri wa maswali, na vyema tukayajadili hapa ili kuweka wazi sasa ili huko baadaye isije ikaleta maneno, mivutano na kushikana masharti.

1. Je, serikali imeamua kummilikisha rasmi Mwamposa lile eneo?

2. Je, serikali imebadili matumizi ya eneo lile kutoka kuwa kiwanda kilichokufa au eneo la wazi la kutumiwa kwa matukio ya kupita na kuwa eneo rasmi binafsi la taasisi ya kidini?

3. Je, serikali imefuta uwezekano wa mtu au taasisi zingine tofauti na Mwamposa kutumia eneo lile kwa sasa au baadaye?

4. Kisheria lile eneo lilikuwa likimiliwa na nani, na matumizi ya sasa (kidini) yanamfaidisha vipi mmiliki?

5. Kwa hatua hizi za sasa, je inaashiria serikali haina tena mpango, mikakati au mawazi kuja kufufua kiwanda cha Tanganyika Packers?
Hii nchi ngumu sana
 
Kamilikishwa sababu mwamposa ana watu wengi sana wanaosikiliza na kumuamini, serikali itamtumia mwamposa kwa jambo lolote hata kwa kuhamasisha waumini wake wakapige kura na watamsiliza watanzania wengi ni bumbumbu
Hata Lissu ana wafuasi wengi sana, mabeberu wanaweza kumtumia akahamasishe watu wasipige kura.
Ngoma droo.
 
Back
Top Bottom