Kwa hiyo FIFA na TFF Wamekurupuka katika kutoa taarifa kuwa Yanga imefungiwa? Au TFF na FIFA hawana mawasiliano?

Kwa hiyo FIFA na TFF Wamekurupuka katika kutoa taarifa kuwa Yanga imefungiwa? Au TFF na FIFA hawana mawasiliano?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
“..tulishawalipa, hakuna kesi yoyote FIFA inayoihusu Yanga” – Ally Kamwe anafafanua kuhusu madai ya timu hiyo kudaiwa na baadhi ya wachezaji iliyoachana nao, atangaza tarehe ya kuanza kutoa ‘thank you’ kwa wachezaji wao, asisitiza kufanya usajili mkubwa na wa kishindo.

Kama kawaida ya watanzania. Wazee wa deadline...dirisha linafungwa tar 15 , malipo tar 14 😂
 
Mpaka Jana Yanga walikuwa wanadaiwA
Orodha ya wanaodaiwa inakuwa updated kila Jumatatu
 
Attachments

  • Screenshot_20240618_234643_Chrome.jpg
    Screenshot_20240618_234643_Chrome.jpg
    301.8 KB · Views: 3
Kwani amkumuelewa alichokisema Aly kamwe, mbona kaweka wazi kwamba taarifa ya tff imetoka wakati washafanya Clearence ya madeni yote, inawezekana kilichotokea ni masuala mazima ya mawasiliano na uthibitisho wa nyaraka husika kwenda fifa, ivyo Yuko sahihi
 
Swala la malipo, ukishalipa FIFA inabiadi wasubiri uthibitisho wa Nyaraka kutoka kwa Mlalamikaji na mlalamikiwa.

Timu ikisha Fanya malipo watatuma Nyaraka FIFA, wakati uo FIFA wanasubiri Nyaraka za Mlalamikaji athibitishe kama amelipwa, Wakisha thibitisha kutoka pande zote mbili ndio wanaondoa iyo ban kwa kuwaandikia FA husika ya mwanachama mdaiwa.

Kama Yanga wanaongopa na hawajafanya malipo ni swala la muda tu kila kitu kitakua wazi.
 
Kila mwaka Yanga na madeni ya wachezaji , madeni na Yanga .GSM tapeli wala tusione aibu kusema ukweli.

Haya madeni ingekuwa simba ndiye anaedaiwa yule mhindi angeshambuluwa Sana na wachambuzi uchwara. Lakini kwakuwa ni tapeli pendwa wa wachambuzi huwezi kusikia wakikemea hii tabia.

Halafu wale Mashabiki uchwara wa uto nao unasikia wanarusha lawama kwa tff kwamba wanaihujumu timu yao badala ya kukemea uongozi wa timu yao.

Na bado kuna la Okrah nalo liko jikoni linapikwa.
 
Mbona kama una hasira na uliye changanyikiwa, ki ufupi Yanga watalipa madeni na watasajili wachezaji wapya wanao wataka katika dirisha ili.
Bado wataendelea kuondoa wachezaji wasio na tija, na katika kurekebisha kikosi madeni yatendelea kuwepo sambamba na Mataji.
Swala la utapeli wa GSM bahati mbaya au nzuri FIFA/ CAF hawajalizungumzia swala ilo unaweza kutuma malalamiko Yako FIFA/CAF waliangalie na ilo.
 
“..tulishawalipa, hakuna kesi yoyote FIFA inayoihusu Yanga” – Ally Kamwe anafafanua kuhusu madai ya timu hiyo kudaiwa na baadhi ya wachezaji iliyoachana nao
Aache kubishana na teknolojia, onyeshe risiti. Isije ikawa jamaa aliyepewa jukumu la kulipia amezichepusha hela

1718783791432.png
 
Kwa vile wamejitahidi kuwa mabingwa wa ligi,mashabiki na wanachama wanatulia.
Janja janja Fc
 
Mbona wadaiwa ni timu nyingi za Tanzania zikiwemo Fountain Gate ,Singida Big Stars na Tabora United mbona hamzisemi ? Mnangángánia Yanga tu ?
 
Back
Top Bottom