PostGE2025 Kwa hiyo SADC wana Tume yao, Serikali ina Tume yake? Kwanini Stergomena anatambulishwa kwa title yake ya SADC?

PostGE2025 Kwa hiyo SADC wana Tume yao, Serikali ina Tume yake? Kwanini Stergomena anatambulishwa kwa title yake ya SADC?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ukiongoza watu kwa mabavu na control lazima ipo siku utafikia “Crisis”.

CCM wamefikia Crisis, hakuna wanaloweza kufanya wakawa politically right, Tutegemee maigizo ya kila rangi kuelekea anguko lao.

Katika haya yaliyotokea miaka minne 2021-2025 wananchi hatumuachii Mungu wala hatutasubiri muda wenu muandike vitabu kuomba msamaha.
 
Viongozi wakitiwa Upofu huwezi kuwambia kitu wakakuelewa kabisa wananchi wanalamikia Uongozi wako unateua mtoto wako naibu waziri kweli? Upofu kitu kibaya sana Omba Mungu akupe macho ya kuona wamekuepo hapo kupitia vyombo vya dola Wananchi kuleta katiba mpya sahau kwa Wanayo fanya sasa wako Top point mbaya Wanaleta karata ya Udini kwenye vitu serious wananchi wamepuuza Viongozi wa badilikeni wale na wananchi wa chini wamekata Cycle top uko wenyewe juu
 
Tume!!!!

Siamini aisee. Kwa hiyo SADC wana Time yao, serikali ina Tume yake?

Kwanini Stergomena anatambulishwa kwa tutle yake ya SADC badala ya title aliyokuwa nayo wakati haya yanatokea? Wana maanisha kwenye hiyo tume yeye ndiye Mwakil8shi wa SADC??

Naona hatuko serious na suala la mauaji

Tax so alikuwa Waziri wa Ulinzi? Anaenda kujichunguza?
HAPANA, hii Tume haipo sawa.
Nadhani tumeamua kulipuuzia hili swala


Britanicca View attachment 3503817
Wahuni
 
Licha ya ukweli kuwa kila kiongozi hupanga safu yake ya kumsaidia kufikia malengo yake, ila kitendo cha kumpa mtoto wake unaibu kimenistaajabisha kidogo ukizingatia pia mume wa huyo mtoto wake ni waziri.

Anaweza kuwa na sifa kabisa lakini kuna mambo kama kiongozi ni bora kujiepusha nayo! Narudi palepale, ni ama washauri wake sio wazuri au hasikii la mtu.
​
Hili kajishauri mwenyewe,Tusipende kusingizia washauri kila uchao. Baraka kaunda mwenyewe
 
Samia kawashika pabaya jamani haya akina mwabukusi/ Heche walikua wanaomba tume ya kijaji iundwe na kuchunguza yaliyotokea hiyo hapo imeshaundwa mnataka nini?

..Tume inaundwa na wajumbe.

..sasa watu wanalalamikia baadhi ya wajumbe walioteuliwa.

..kuna baadhi ya wajumbe, kwa mfano, Jaji Mkuu Mstaafu Prof.Ibrahim, na Waziri wa ulinzi mstaafu Dr.Tax, wanahusishwa na mifumo iliyosababisha machafuko ktk taifa letu.
 
Halafu ukiangalia majina ya wnatume asilimia kubwa wamehudumu kwenye serikali ya aliyekuwa rais ambaye pia anatuhumiwa kuwa kama ndiyo remote controller
 
Watu waliojipitisha kwa 98% na kuapishana chini ya jeshi..don't give a fvck about common civilians
 
SIFA ZA DALALI WA UPATANISHO ALIYE MKWELI

Rais Martti Ahtisaari - Ili Ufanikiwe Katika Upatanishi wa Amani unapaswa kuwa Dalali Mwaminifu​


View: https://m.youtube.com/watch?v=HXLLAo_3eXI

Rais Martti Ahtisaari - Ili Ufanikiwe Katika Upatanishi wa Amani unapaswa kuwa Dalali Mwaminifu

Ili Kufanikiwa katika Upatanishi wa Amani inabidi uwe Dalali Mwaminifu 21 Oktoba 2015 Martti Ahtisaari, Profesa Mgeni wa Humanitas katika ujenzi wa Serikali na Diplomasia 2015-16, anatoa mihadhara miwili ya hadhara, kushiriki katika Mazungumzo na wazungumzaji wengine walioalikwa, na kuhudhuria kongamano la kuhitimisha, kwa kuzingatia Mandhari ya Amani?

Hii ni ya pili kati ya mihadhara yake miwili ya hadhara. Katika mhadhara swali la msingi ni nini masharti ya utatuzi wa migogoro uliofanikiwa.

Je, unawezaje kupatanisha na kutatua migogoro kwa namna ambayo inajenga msingi imara na endelevu kwa jamii kuendelea au kuanza maisha yake kwa amani?

Kwa mpatanishi ni muhimu kuelewa jinsi ya kushughulikia utu wa vyama na kuhakikisha kwamba jamii ina misingi ya kuelekea kwenye upatanisho wa kweli na amani.

Katika kazi hii kujenga uaminifu ndio kila kitu. Amani haitekelezwi tu na taasisi, bali na watu.
Martti Ahtisaari ni balozi wa zamani wa Finland nchini Tanzania na pia mtaalamu wa UN katika masuala ya migogoro, upatanishi .
In Order to Succeed in Peace Mediation you have to be an Honest Broker21 October 2015Martti Ahtisaari, the Humanitas Visiting Professor in Statecraft and Diplomacy 2015-16, will give two public lectures, participate in a Conversation with other invited speakers, and attend a concluding symposium, based on the theme of How Can Peace be Made?. This is the second of his two public lectures. In the lecture the underlying question is what the preconditions are for a successful conflict resolution process. How do you mediate and solve conflicts in a manner that creates solid and sustainable foundation for a society to continue, or begin, its life in peace? For a mediator it is important to understand how to deal with dignity of the parties and to ensure that the society has the grounds to move in the direction of true reconciliation and peace. In this work creating trust is everything. Peace is not implemented only by institutions, but by people
 
Kuuhadili huu ujinga ni kama mmeshakubali kuwa mlifanya uchaguzi.

Tume ya nini ya kipumbavu hiyo, tume zisizoleta majibu kwa watanganyika ni ujinga.

Ama mkubali uchaguzi ulifanyika au muache kujadili mambo ya ccm humu.
 
..Tume inaundwa na wajumbe.

..sasa watu wanalalamikia baadhi ya wajumbe walioteuliwa.

..kuna baadhi ya wajumbe, kwa mfano, Jaji Mkuu Mstaafu Prof.Ibrahim, na Waziri wa ulinzi mstaafu Dr.Tax, wanahusishwa na mifumo iliyosababisha machafuko ktk taifa letu.
How?
 
..Tume inaundwa na wajumbe.

..sasa watu wanalalamikia baadhi ya wajumbe walioteuliwa.

..kuna baadhi ya wajumbe, kwa mfano, Jaji Mkuu Mstaafu Prof.Ibrahim, na Waziri wa ulinzi mstaafu Dr.Tax, wanahusishwa na mifumo iliyosababisha machafuko ktk taifa letu.
Tungewaweka Sugu, Bwege na Lema??
 
Nina wasiwasi na impartiality ya hiyo tume. Ukiondoa Balozi Meela na Balozi Kapya ambao siwafahamu na Prof IbrahimJuma waliobaki ni washikaji wa Kikwete. Walikuwa watu wa Mwanzo kushugulikiwa na Magufuli.
Umeichungulia hii.. janja janja tu.
 
Rejected
 

Attachments

  • 20251118_192639.jpg
    20251118_192639.jpg
    162.6 KB · Views: 18
Tume!!!!

Siamini aisee. Kwa hiyo SADC wana Tume yao, serikali ina Tume yake?

Kwanini Stergomena anatambulishwa kwa title yake ya SADC badala ya title aliyokuwa nayo wakati haya yanatokea?

Wanamaanisha kwenye hiyo tume yeye ndiye Mwakilishi wa SADC?

Naona hatuko serious na suala la mauaji

Tax si alikuwa Waziri wa Ulinzi? Anaenda kujichunguza?

HAPANA, hii Tume haipo sawa.
Nadhani tumeamua kulipuuzia hili suala


Britanicca View attachment 3503817
Nadhani indicator ya kwanza ya kupuuzia yaliyotokea ilionekana tangu kipindi cha kutangaza matokeo

Watu serious na wanaojali wasingeweza kutangaza matokeo katika mikoa ya Dsm, Mwanza, Arusha, Mbeya, Songwe na Tunduma sehemu ambazo kwa hakika hakuna kura zilizohesabiwa

Kutotilia maanani kwingine ni kuamua kutangaza 98% ya ushindi. Hapa mwenye kuwaza vizuri alishagundua hawa watu wanalao jambo tofauti na linalohusu maslahi ya nchi na raia wake

Kingine ni baraza lililoundwa linaloenda kwa jina la "wanafamilia". Hapa bado tu unaona kuna mtu anajali chochote?

Hii tume ni kanyaboya kama zilivyokuwa zile kanyaboya za 4R ambazo kila siku asubuhi mchana na jioni walikuwa wanaziimbia kuanzia vijijini hadi ngazi za kimataifa ili ziwasaidie kupata wanachokitaka wao vile vile watatumia ripoti ya hiyo tume kutimizia mahitaji yao yanayopatikana nje ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom