Uchaguzi 2020 Kwa hizi sababu Lissu anaweza kukosa sifa za kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye kumpa changamoto Mgombea wa CCM

Nchi hii ina utawala wa sheria ukiona

Rais Magufuli amefanya mambo mazuri ni lazima tumsifie
 
Ni kwa mara nyingine tena, ningependa nishiriki nanyi wanabodi wenzangu katika kuyasema yale ambayo nastahili kuyasema wazi kuhusu siasa zetu na wanasiasa wetu wa Tanzania.

Siku ya jana ni siku muhimu kwa kikundi fulani cha watu ndani ya Tanzania. Ni muhimu kwao kwa sababu kamanda wao Tundu Anthipas Lissu alitangaza nia ya kugombea Urais kwa makamanda wenzake! Sina hakika kama ni Urais wa nchi au wa chama.... Lakini kama ni hivyo, basi ngoja niendelee kuandika.

Kuna mambo kadhaa yamejitabainisha kutoka kwa kamanda huyo. Hata kuonekana wazi kuwa hatoshi kushika nafasi kubwa Kama kiongozi/Rais wa nchi. Mambo hayo ni Kama yafuatayo.

Mosi: Ni dhahiri kwamba, Kamanda Lissu hafahamu nini hasa mahitaji ya wananchi, kwa maana kujua shida za wananchi na kuzitatua. Yumkini hajazungumzia hata suala la afya kwa wananchi ikiwa ni njia moja wapo ya kuleta maendeleo nchini, ingawa ni eneo ambalo linahitaji uongozi madhubuti ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka. Lakini ajabu hajalipa mkazo hata kidogo, na mengine mengi yahusuyo Huduma za jamii. Hakika Kamanda huyu hafai kuwa Rais wa nchi yetu pendwa Tanzania!

Pili: Kamanda Lissu, ameonesha wazi, kuwa yeye ni mtu wa visasi, kwa sasa anashindwa kulipa kisasi kwa sababu hana mamlaka. Na hata hivyo amejitahidi kuficha roho mbaya ya kisasi kwa yule anayemkusudia kwa kuzungu zunguka na hoja nyepesi za kikatiba! Kwa hiyo ni dhahiri kuwa, ikiwa akapata nafasi ya Urais wa nchi, basi kazi kubwa atakayoifanya ni kulipiza kisasi tu. Mtu huyu hafai hata kidogo!

Tatu: Kamanda Lissu ni mtu ambaye anajifanya anajua kila kitu na kwamba analolifanya ama kusema yeye ndilo lililosahihi kuliko wenzake. Alichobarikiwa ni kupiga kelele, kutosikiliza, dharau na ujuaji wa kijinga. Na ndio maana kwa sababu hiyo, ye yote ambaye anamtazamo tofauti naye atampa maneno ya vijembe na dharau dhidi yake. Huyu hauwezi uongozi!

Nne: Kamanda Lissu si mtulivu katika maamuzi na maongezi, yeye ni mpayukaji, kwa mfano kulikuwa hakuna haja ya kusema "sitakimbia kwenda kijijini hata katika wakati mgumu, kwa mfano kipindi hiki cha Covid-19!" Maneno hayo Ni dhahiri kuwa hana utulivu wa akili wakati anapokuwa anazungumza ama kutenda jambo, lenye manufaa kwa wote, ni mbinafsi wa mawazo, wa kusema na hata kutenda. Huyu jamaa hawezi kabisa kuwa Rais wa nchi!

Tano: Kamanda huyu ni mtu wa ovyo na asiyejiamini. Hilo limethibitika kwa maneno na matendo yake, ni wazi kuwa akishika madaraka ya Urais si ajabu akauuza Uhuru wetu na umoja wetu wa kitaifa kwa mataifa ambayo yeye ni vibaraka wake. Huyu mtu hana uzalendo kwa taifa, hana uwezo wa kudumisha uhuru na umoja wetu wa kitaifa. Hafai huyu mtu kuwa Rais wa Tanzania. Yupo tayari kuiuza nchi yetu, kwa kutojiamini kwake. Sifa ya kujiamini kama kiongozi hana Kamanda huyu wa ovyo.

Mwisho, ni ukweli ulio sirini kwa makamanda wa ngazi za juu hata kwa Mbowe mwenyewe, kwamba Tundu anakosa sifa na uwezo wa kuongoza katika nafasi ya Urais na hata nafasi ya uenyekiti. Lakini kwa kuwa siasa ni watu, wameona ni afadhali kamanda huyu ambaye anaoujasiri wa kuiuza nchi kwa vibaraka vyake na kutegemea msaada wa vibaraka hao wa bwana Lissu, ili kuwalaghai wananchi wakifikiri kwamba watanzania ni wadanganyika. Basi wameona na iwe hivyo, hata kukubali kumpa Lissu Umakamu Mwenyekiti na hata kufikiria kumpa ridhaa hiyo ya kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA.

Ni lazima CHADEMA ikubali kuwa watanzania wanajua chaguo lao sahihi ni lipi, watanzania hawataki watu wajuaji wa kueleza wala wajuaji wa kupinga, wala wajuaji wa sheria. Watanzania wanataka jambo moja tu, wanataka maendeleo. Na maendeleo hayo ni dhahiri yameonekana kuwa yanaweza kupatikana ndani ya uongozi imara wa CCM. Ni mtu aliyechanganyikiwa tu kama alivyochanganyikiwa Kamanda Lissu, ndiye atazungumzia habari za Corona na vijijini na visasi, na kushindwa kuzungumzia habari za shule, maji, afya, nishati, miundombinu, maliasili, Mawasiliano, kilimo n.k kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Kamanda Lissu ugua pole, ni dhahiri kuwa bado unaumwa, lakini pia hongera kwa kuonesha nia ya kutaka kuwa Rais wa CHADEMA na Rais wa watanzania wa mitandaoni. Huku kwenye Urais wa Jamhuri, uache kabisa na usiufikirie, kwani wananchi wameshakujua kuwa hujui na huna sifa za kuongoza. Huku Tanzania iache Chama Cha Mapinduzi CCM na Dkt. John P. Magufuli. Maana ndio hao pekee ambao wanaouwezo wa kuwaletea matumaini wananchi na kuleta maendeleo ya nchi kwa kipindi kingine cha 2020-2025.

Karibu 2020
Sauti ya Mdodomia.
 
Pumbavu, Umendika Upumbavu wewe ni kiongozi wapi? ulishawai kuongoza nini ukute hata famia huna unadanga tu.
 
CCM imefika pabaya Now yaani pamoja na kujipa serikali za mitaa, baraza la wawakilishi Zanzibar, ila Hamna furaha [emoji23][emoji23][emoji23]
Sawa na kupata 100% wakati umepiga chabo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna wakati najiuliza ulimaliza shule kweli au ndio unaanza kindergarten maana si kwa uandishi huu na mawazo haya
Ningekushauri urudi shule kwanza kha unachefua ujue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…