Kwa huu Ukweli Mchungu wa huyu Mtangazaji wangu bora wa Michezo nchini Alex Luambano wa Clouds FM naomba atunukiwe Tuzo ya Heshima upesi

jezi wameuza nyingi wamemuuzia nani? kama 98% ya mashabiki walivaa old model, hizo takwimu za 1M sold ni uzushi kama tulivyodanganywa kua kipa anadaka hadi risasi
 
Uzi umeandikwa na yule jamaa wa kutoka Rwanda aka Popoma...
 
"Yanga SC haiandaliwi Kiushindani Uwanjani ila kilichopungua tu sasa ni Strategy ya Kibiashara zaidi ambapo kila mwaka Timu inasajili Wachezaji wengi wa Kigeni kisha kuwatengenezea Hamasa ya Kimvuto kwa Mashabiki halafu wanatumika Kujaza Uwanja na Kuuza Jezi zao nyingi na Kutajirisha Kampuni na Watu wachache wachache tu", Alex Luambano.

Chanzo: Hili Game Program Clouds FM

Mtangazaji Alex Luambano hujawahi Kuniangusha ( hasa katika Suala la kusema Ukweli ) na Kitu pekee ninachokupendea huwa huna Upendeleo katika Kuvisema hivi Vilabu vikubwa na vikongwe nchini Tanzania vya Simba na Yanga.

Kwa hiki ulichokisema leo najua utachukiwa na Wapuuzi na Wanafiki wengi ( hasa wenye Upeo Hafifu ) ila kwa Wanamichezo tunaojitambua na Kichwani zimetimia tumekuelewa na ndiyo maana tunasema unastahili Tuzo ya Heshima.

Anajua sana kutangaza, kitu asipokijua huwa anakaa kimya huwa hana haraka ya kujifanya anajua kilakitu.
 
Hawa Wachambuzi wetu wangekuwa smart wangetakiwa kuzingatia yafuatayo:-

1. Ligi yetu ilichelewa sana kumalizika!
2. Yanga wamemaliza mashindano July 25.
3. Baada ya kumaliza mashindano WAKALAZIMIKA kufanya usajiri wa kuziba mapengo ambayo kila anayefuatilia soka aliyaona msimu uliopita!!
4. Yanga wamekuja kukamilisha usajiri katikati ya August.
5. Baada ya kukamilisha usajiri, wakaanza safari ya Morocco kwa ajili ya maandalizi.
6. Kabla hawajatulia, mara ratiba ya CAF inatoka na Yanga wanatakiwa kucheza michezo ya awali muda mfupi ujao (sikumbuki vizuri nini kilianza kati ya safari na ratiba manake vilifuatana)
7. Kwahiyo ndani ya chini ya mwezi mmoja Yanga wakajikuta wanatakiwa kuwa Morocco, Wiki ya Mwanachi, Mchezo wa awali wa CAF!
8. Wakalazimika kuvunja kambi Morocco
9. Kwavile wameshachukua mpunga wa kutosha kutoka Azam, ilikuwa LAZIMA Wiki ya Mwananchi ifanyike kwa sababu hakuna content bora kwa Azam kama Wiki ya Mwananchi
10. Swali lilibaki ifanyike lini hiyo Wiki ya Mwananchi!! Hutakiwi kuwa genius kufahamu ilitakiwa ifanyike mapema iwezekanavyo ili angalau wapate muda kidogo kuelekea mechi ya CAF!

Kinachowasaidia Simba ni kwa sababu tu wao wanaanza mzunguko wa pili, na tarehe ipo mbali kwahiyo hawana pressure! Ndo vile tu Baba zake wadogo na shangazi zake na Mwamedi wamegoma kutoa pesa zaidi kwa Mwamedi za kuendelea kuwaweka Makorokoro huko Morocco, vinginevyo Makorokoro bado walikuwa na uwezo wa kubaki Morocco hata kwa wiki 2 zaidi na wasiathirike! Kama sivyo, hata Simba nao wangepata hili tatizo kwa sababu na wenyewe wamesajiri wachezaji wengi ambao wala wasingepata muda wa kuwaunganisha na timu yao ya zamani.

Halafu hawa Wachambuzi uchwara wajaribu kutumia akili kidogo!! Mbwembwe za kutambulisha akina Manara hazifanyi mazoezi kwenye pitch kusimama kwa sababu wanaohusika na mambo kama hayo, including maandalizi ya Wiki ya Mwananchi sio watu wa Benchi La Ufundi. Kama Mwamedi asingegomewa zile pesa za urithi, Makorokoro FC wangekuwa na uwezo wa kubaki Morocco na kurudi Dar siku 1 au mbili kabla ya Kilele cha Simba Day na bado kusiwe na tofauti yoyote ile, unless changamoto iwe usafiri.
We ndiyo mchambuzi uchwara kabisa, unatetea timu yenu kukosa uweledi wa kiuendeshaji?

Mtamlaumu nani kama mtatolewa hatua za awali ( preliminary stage) za CAF CL?
 
Unaweza kueleza huo weledi unaosema wewe umekosekana ni weledi upi?!
 
Hawa Wachambuzi wetu wangekuwa smart wangetakiwa kuzingatia yafuatayo:-

1. Ligi yetu ilichelewa sana kumalizika!
2. Yanga wamemaliza mashindano July 25.
3. Baada ya kumaliza mashindano WAKALAZIMIKA kufanya usajiri wa kuziba mapengo ambayo kila anayefuatilia soka aliyaona msimu uliopita!!
4. Yanga wamekuja kukamilisha usajiri katikati ya August.
5. Baada ya kukamilisha usajiri, wakaanza safari ya Morocco kwa ajili ya maandalizi.
6. Kabla hawajatulia, mara ratiba ya CAF inatoka na Yanga wanatakiwa kucheza michezo ya awali muda mfupi ujao (sikumbuki vizuri nini kilianza kati ya safari na ratiba manake vilifuatana)
7. Kwahiyo ndani ya chini ya mwezi mmoja Yanga wakajikuta wanatakiwa kuwa Morocco, Wiki ya Mwanachi, Mchezo wa awali wa CAF!
8. Wakalazimika kuvunja kambi Morocco
9. Kwavile wameshachukua mpunga wa kutosha kutoka Azam, ilikuwa LAZIMA Wiki ya Mwananchi ifanyike kwa sababu hakuna content bora kwa Azam kama Wiki ya Mwananchi
10. Swali lilibaki ifanyike lini hiyo Wiki ya Mwananchi!! Hutakiwi kuwa genius kufahamu ilitakiwa ifanyike mapema iwezekanavyo ili angalau wapate muda kidogo kuelekea mechi ya CAF!

Kinachowasaidia Simba ni kwa sababu tu wao wanaanza mzunguko wa pili, na tarehe ipo mbali kwahiyo hawana pressure! Ndo vile tu Baba zake wadogo na shangazi zake na Mwamedi wamegoma kutoa pesa zaidi kwa Mwamedi za kuendelea kuwaweka Makorokoro huko Morocco, vinginevyo Makorokoro bado walikuwa na uwezo wa kubaki Morocco hata kwa wiki 2 zaidi na wasiathirike! Kama sivyo, hata Simba nao wangepata hili tatizo kwa sababu na wenyewe wamesajiri wachezaji wengi ambao wala wasingepata muda wa kuwaunganisha na timu yao ya zamani.

Halafu hawa Wachambuzi uchwara wajaribu kutumia akili kidogo!! Mbwembwe za kutambulisha akina Manara hazifanyi mazoezi kwenye pitch kusimama kwa sababu wanaohusika na mambo kama hayo, including maandalizi ya Wiki ya Mwananchi sio watu wa Benchi La Ufundi. Kama Mwamedi asingegomewa zile pesa za urithi, Makorokoro FC wangekuwa na uwezo wa kubaki Morocco na kurudi Dar siku 1 au mbili kabla ya Kilele cha Simba Day na bado kusiwe na tofauti yoyote ile, unless changamoto iwe usafiri.
Usingeingiza ushabiki ungeeleweka vizuri zaidi
 
Mbona sijaingiza ushabiki wowote?! Hayo ya Mwamedi ni matani ya kisoka tu, lakini hoja ni kwamba, kwavile Makorokoro mechi yao ipo mbali sana, wangekuwa na uwezo wa kuendelea kujifua Morroco hata kwa wiki 2 zaidi zijazo na wasiathirike, advantage ambayo Yanga hatukuwa nayo!!

Najua wengi wanachanganya sana kati ya mbwembwe za Wiki ya Wananchi na Pitch Outcome wakati hizo idara watendaji wake ni tofauti!! Timu haipo imara kwa sababu tu hapakuwa na muda wa kuiandaa timu! Hoja ingekuwa tofauti kama tusingekuwa kabisa na Wiki ya Mwananchi kama ilivyo kwa Azam ambao, pamoja na wao kuwa na muda mfupi, lakini they've undivided attention.
 
Kwa taarifa yako tu sasa nina Miaka 15 ya Kumsikiliza Mtangazaji Alex Luambano wa Clouds FM na hajawahi kuwa Mnafiki au mwenye Upendeleo katika kutoa maoni yake kwa Vilabu vya Simba na Yanga.

Fuatilia huko nyuma ameshawahi Kutuchana vilivyo Simba SC mpaka Siku Moja Crescetius Magori na Ismail Rage wakamsifu kwa kutusema Simba SC na wakamuahidi kuwa aliyosema Simba SC itayafanyia Kazi na mengi yameshatatuliwa.
Shaffi dauda aliai sema kwamba simba imeingia makundi na katika kundi lake yeye ndo underdog basi tangu hapo alichukiwa
 
Back
Top Bottom