Kwa huu usawa acha nihamie tu Hybrid, kutumia milioni 5 kwajili ya mafuta, its above my grade,

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Kwenda kazini: 13 km
Mizunguko : 12 km
Kurudi nyumbani: 13 km

Jumla ni takribani 38 km kwa siku.

Gari langu linatumia wastani wa lita 1 kwa km 9 hadi 10, hivyo kwa siku natumia takribani elfu 15 hadi 16

Kwa mwaka hata nikipumzika jumapili, matumizi ya mafuta yanakaribia milioni 5.

Baada ya kukaa chini na kufanya mahesabu, nimeamua kuweka ego yangu pembeni, Ni wakati wa kuhamia kwenye hybrid.

Wabongo wengi tunaziogopa sababu ya story za vijiweni, wanaziogopa sababu wanaomba ushauri wa kununua magari kwa kina fundi Nyundo ambao wakiona gari linahitaji computer, scanner na diagnosis badala ya kugonga nyundo jibu lao la kwanza ni, "Achana nalo, litakusumbua."

lakin nimefanya research na nimebaini zipo garage zinazoweza kumudu zikiwemo garage certified za Toyota ambazo zipo majiji yote nchini. Makadirio ya matengenezo ukiondoa gharama za kawaida ambazo zipo kwa kila gari, may be yanaweza kuwa 300K kwa mwaka.

Kwa hiyo, tuki assume matengenezo yatakuwa 300k garage za kisasa na mafuta tufanye yatakuwa takribani milioni 1.5 kwa mwaka mzima, bado naona ni uamuzi wenye faida kubwa, naokoa kibunda kirefu tu.

Kwa kifupi, it pays off a lot.
 
Hybrid cars ndiyo mwisho wa matatizo
Shida ya Wabongo wakitishwa kidogo tu na stori za vijiweni, wengi wanaogopa bila kufanya utafiti.

Halafu maneno hayo yanaanziaga kwa wale wanaoenda kuwaomba ushauri kina fundi Nyundo kama gari wanalotamani kuagiza linafaa, hapo wakiona tu gari linahitaji computer, scanner na proper diagnosis badala ya kubahatisha, jibu lao la kwanza ni, "Achana nalo, litakusumbua." πŸ˜‚

Sometimes matengenezo yanaweza kuwa mepesi ila ukatandikwa kisawa sawa sheli lakini ni heri ugharamike matenegezo hata kwa laki 3 ya ziada ila safari za sheli zipungue
 
Tatizo Wabongo miundo mbinu yetu ya hovyo! Public transport hoi.
Imagine mtu ananunua gari kwa ajili ya kwenda kazini.
Na sio kwa ajili ya mambo mengine binafsi.
 
Tatizo Wabongo miundo mbinu yetu ya hovyo! Public transport hoi.
Imagine mtu ananunua gari kwa ajili ya kwenda kazini.
Na sio kwa ajili ya mambo mengine binafsi.
Gari ukizunguka nayo miji ya japan unapata hadi 16 km kwa lita, barabara ni za viwango yaani ule mkeka grade A, mafuta safi ya uhakika hakuna usanii.

njoo nalo bongo sasa πŸ˜‚ kwanza sheli zenyewe zinatofautiana ulaji wa mafuta tayari hapo kuna uchakachuaji, unaingia road mara ukutane na tuta, shimo, boda, n.k. kila dakika unakanyaga mafuta na breki, hapo ukiweka lita 5 zinakata baada ya km 40 tena ni engine ndogo kama 1nz, ukitumia mark x unaweza kujuta kama huwezi afford wese
 
Dunia ndiyo inaenda Huko kwenye hybrid cars hakuna mwenye ubavu wa kuzuia revolution time kwenye ulimwengu wa magari.
Mafundi wa chini ya mwembe lazima wabadilike tu
 
Kiasi fulani kuna mabadiliko, sasa hivi gari hizi barabarani ni nyingi si haba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…