Hivi karibuni kumetolewa madai na kenya kuhusu mahindi yetu kuwa na sumu kuvu. Swala la milipuko ya watu kuugua na kufa kwa kula mahindi yenye viwango vya juu vya aflatoxin limekuwepo nchini kenya tangu mwaka 1981. Mfano, mwaka 2004 wakenya 317 waliugua na 125 walifariki kutokana na kutumia mahindi yenye viwango vya juu vya sumu kuvu aina ya aflatoxin.
Chanzo cha tatizo yalikuwa ni mahindi yaliyokuwa yamezalishwa na wakulima wenyewe na kuhifadhiwa katika mazingira mabovu. Kwa hiyo utaona hayo mahindi hayakutoka Tanzania.
Nchini kenya kumekuwa na kawaida ya Wafanyabiashara wakubwa kuagiza na kuhodhi mahindi kwa muda mrefu hali inayopelekea sumu kuvu kuendelea kuzalishwa yakiwa yamehifadhiwa, na baadaye kutolewa kwa bei chee kwa watu maskini ambao wanakuwa wamekumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, na hivyo kutokea milipuko ya aflatoxin.
Haiwezekani uagize na kuhifadi mahindi, miaka mitano baadaye useme hayo mahindi yenye aflatoxin yametoka Tanzania. Utafiti umeonyesha mahindi yaliyovunwa maeneo mbalimbali nchini Tanzania yana viwango vya chini sana vya aflatoxin ambavyo ni chini ya viwango vya wastani vinavyopendekezwa na mamlaka za usalama wa chakula nchini Tanzania.
Kenya wanapokuja na tuhuma zisizokuwa na mashiko maana yake wana ajenda nyingine ambazo wanakuwa wamebeba na hii si mara ya kwanza. Kwa hiyo ili kuweka mazingira ya kuheshimiana ni bora serikali ichukue hatua mathubuti dhidi ya hizi sarakasi za kila mara kutokea Kenya.