Kwa 'intolerance' waliyoonesha CCM kwa Ndugai, Wapinzani si watawapiga risasi?

Kwa 'intolerance' waliyoonesha CCM kwa Ndugai, Wapinzani si watawapiga risasi?

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
Najua wengi hawampendi Ndugai, ni kutokana na uvunjifu mkubwa wa katiba na utawala wa sheria alioufanya tokea awamu ya 5, mi binafsi pia simkubali

Sasa kilichonishtua ni hii reaction ya CCM iliyoonyeshwa kwa Ndugai kwa maoni aliyotoa ambayo kimsingi yalikuwa yamelenga kutetea tozo za Serikali

Wamejitokeza viongozi wa CCM kila upande wa nchi wakimshambulia Ndugai hadi wengine kusema kuwa Ndugai ni mgonjwa na Samia anatakiwa akamtibu

Simuonei huruma Ndugai, nashangaa tu kama CCM wameweza kumshabulia vile mtu ambaye wamempa cheo kikubwa kama Uspika kwa ukosoaji wa kawaida tu, je watawafanyaje kwa Wapinzani ambao watatumia lugha kali zaidi kuwakosoa na hawana cheo kama cha Ndugai?

Wapinzani wataungana na CCM kumshambulia Ndugai, sababu Ndugai ni kweli amefanya ufedhuli mwingi dhidi yao, lakini kumbuka kuwa ni CCM hawahawa walikuwa wakimuunga mkono Ndugai au kumtuma kufanya ufedhuli huo

Kwa Polepole ni hivyo hivyo, sasa kuna baadhi ya Wapinzani wameahidiwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mikutano na wakaamini, kwa akili ya kawaida tu, CCM hii ambayo inakuwa kama mbogo aliyejeruhiwa Serikali yake inapokosolewa kidogo tu, ndio itawaruhusu wapinzani wachaguliwe au wafanye mkutano ya kuwakosoa vikali?
 
Mimi napenda kuona watu wanakosoa uongoz hyo ndo democracy

Hao wanaomgombeza sabufa ni njaa zao tu wanalenga teuzi ila wanajua kabsa mashungi hakufanya poa
 
Kuna kitu kinapikwa jikoni, soon mtashuhudia,Ndugai hawezi kwenda front kizembe hivyo.
Hii nchi kuna watu wapo kwaajili ya kutengeneza tatizo na kulitatua wenyewe.
Tunachezeshwa ngoma ya kitoto sanaa
 
Back
Top Bottom