Kwa Jinsi 'Kiboko ya Wachawi' anavyowadhihaki Watanzania, ipo haja ya mamlaka inayosajili makanisa na taasisi nchini kuongeza umakini

Inauma hiyo,yaan mtu anakutapeli alafu anakutukana.
 
Huwa mara nyingi hawapo kwenye akili zao,hawa Waamini wahanga wengi wao ni watu waliokuwa na shida mbali mbali,yaani desperate ones chukulia mmama ambaye hana mtoto na anaona umri unamtupa mkono. Anaenda kwa Mchungaji huyu na anaambiwa Leta Laki Tano shida yako itaisha...!

Sasa kwa yule mwenye shida hasa atajiuliza Laki tano kitu gani? Iwapo shida itaisha,Ni wazi atatoa tu..!

Chonde waathirika tuwahurumie Zaidi kuliko kuwashutumu.!
 
Sasa akili zitakaa sawa fikiria serikali imemfukuza lakini bado wanamlilia arudi ni ukichaa huu. Fungua vitabu vya dini kwa imani zote kuna mistari ya nguvu imewekwa . Dini zote kuna kufunga na kumuomba Mungu, Dini zote zina kutoa sadaka , Dini zote zinaamini kusaidia yatima sasa leo mtu anakuambia nipe pesa nikusaidie kweli mbona hospitali tunalalamika kwa nini hawa matapeli tunakubali? Mbaya zaidi ni wamama tuu ndiyo kinawakuta. Mimi mtanisamehe ila acha wapigwe akili irudi. Usishangae kesho utasikia wengine nao wamepigwa.
 
Yes serikali ina mambo mengi haina uwezo wa kumfuata kila raia na kumfundisha kuwa asiende kusali kwenye kanisa fulani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…