SoC01 Kwa jinsi namba D 'zilivyotutesa', zikianza namba E, tufanye mabadiliko haya

SoC01 Kwa jinsi namba D 'zilivyotutesa', zikianza namba E, tufanye mabadiliko haya

Stories of Change - 2021 Competition

Bemendazole

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2020
Posts
2,649
Reaction score
6,680
Ukisoma chapisho la Profesa wa uchumi, ndg George Akerlof, lijulikanalo kama 'market for lemons' utaona anavyofafanua juu ya ugumu wa kupata gari bora pale unaponunua gari lililotumika hasa kutokana na taarifa mbonyeo (information assymetry) anazokuwa nazo mnunuzi ukilinganisha na muuzaji ambaye analijua gari kinagha ubaga

Kutokana na ugumu wa kulitambua gari kwa muonekano tu (mere looking) wananchi wengi wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali ili kufikia maamuzi ya kununua gari husika.

Moja wapo ya approach inayotumika ni kwa kuangalia namba za usajili.

Kwa sasa wanunuzi wengi wanaamini kuwa gari yenye recent registration number, yaweza kuwa bora kuliko gari yenye namba za zamani. Yani yaweza kuwa rahisi kumuuzia mteja gari ya Toyota Stout yenye namba D kuliko kumuuzia Hilux Vigo yenye namba A

Hii pia huchangiwa na kitu kinachoitwa owenership utility. Yani mteja anapata satsfaction kumiliki kitu kipya ingawa kipya chaweza pia kuwa kinyemi.

Tangu usajili wa magari kwa batch ya D uanze nchini takrabini mwaka 2014, batch hii imeendelea kuwepo kwa kipindi kirefu na huenda ikaisha mwaka 2022.

Kukaa kwa batch moja ya namba kwa muda mrefu huchangia kuharibu information symetry kwa kuwa si kweli kwamba gari yenye namba D iliyosajiliwa mwaka 2015 itakuwa na viwango sawa na gari yenye namba D iliyosajiliwa mwaka 2021.

Batch moja inapokaa muda mrefu huharibu taswira ya bidhaa na kumchanganya mteja juu ya bidhaa mbili zenye ubora tofauti lakini zilizowekwa kwenye batch moja.

Pia kuweka magari ya zamani na magari mapya (recently registered cars) kwenye batch moja, huchangia kudidimiza ownership utility au uhondo/ furaha anayoweza kupata mmiliki wa gari 'jipya' endapo angekuwa kwenye batch tofauti na mmiliki wa gari ya zamani.

Ikizingatiwa kuwa tangu tupate uhuru mpaka sasa nchi ina magari yaliyoko bara barani yasiyozidi milioni mbili na kwa kuzingatia kuwa batch moja mathalani namba D peke ake ina uwezo wa kuchukua hadi magari laki tano na elfu 19, haitokuwa busara pale namba E itakapoanza kuweza kuchukua magari laki tano na ushee wakati jumla ya magari nch nzima hayafiki milioni mbili.

Ipo haja ya kupunguza idadi ya magari yanayosajiliwa kwa kila batch kutoka hiyo takrabini laki tano na ishirini elf mpaka kwenye laki mbili na nusu.

Jambo hili si geni kwani limekuwa likifanyika kwenye mambo mengine.

Mathalani, mtoto ukimpa sahani moja ya chipsi mayai akashindwa kumaliza au akatumia siku nzima kuimaliza, kesho yake si utampa nusu sahani ili aimalize fasta?

Sasa basi kuliko kusajili magari kwenye range ya kutoka 101 hadi 999 kama sikosei, ni bora usajili ukomee kwenye magari mia tano kabla ya kurukia herufi nyingine ili kupunguza wigo wa batch wa kubeba magari mengi hivyo kuondoa uhalisia.

Mfano zitakapo anza namba E, usajili wa gari utaanza na T101 EAA. Pale itakapofikia T500EAA basi usajili urukie kwenye herufi inayofuata yani B na kuwa na namba T101EAB badala ya T501EAA.

Soko la 'mtumba wa magari ya mtumba' ni kubwa sana hasa kwa mkoa kama Dar Es Salaam.

Kwa kukadiria takrabin 90% ya magari yenye namba A yaliyokuwepo Dar hayapo tena kwa sasa maana yameshauzwa mikoani.

Takrabini 80% ya magari yenye namba B yaliyokuwepo Dar, hayapo tena kwa sasa kwa kuwa yamekwisha uzwa mikoani na takrabini 60% ya magari yenye namba C yaliyokuwepo Dar hayapo tena kwa sasa kwa kuwa yamekwisha uzwa mikoani.

Hivyo kwa ukubwa huu wa soko unaona ilivyo muhimu kutengeneza information symetry itakayo wasaidia watu wa mikoani kupata fair view ni kwa kiasi au muda gani gari analotegemea kulinunua limetumika hapa nchini with a single information displayed on a plate number.
 
Upvote 12
Kweli binadamu haturidhiki.. sasa herufi si zitaisha haraka na kuanza kusumbua serikali kuingia gharama za kubuni herufi mpya mara kwa mara.
Hapana. Mfano kwa mtiririko huu wa sasa namba E, itaisha mwaka 2030! Namba ZZZZ itaisha baada ya miaka mia mbili ikiwa magari yataendelea kuingia kwa rate hii. Kwa hiyo gari yenye namba T999ZZZ itasajiliwa kwenye mwaka 2230!
 
Na kwa nini mtirirko uwe ule ule wakati idadi ya watu inaongezeka na tunazidi kutusua mapene
 
Na kwa nini mtirirko uwe ule ule wakati idadi ya watu inaongezeka na tunazidi kutusua mapene
Kuna kitu kinaitwa market saturation. Kwa hiyo hata kama tunaongezeka, kasi ya uagizwaji wa magari yaweza kupungua kwa kuwa tayari wengi wanayo.
 
Halafu anadanganya anaposema kuwa magari na A,B,C Hayapo tena DSM, sio kweli binafsi nina magari ya namba zote hizo.
Mkuu, sijadanganya. Pengine wewe ndio hujaelewa. Labda usome tena.
 
Takrabini 80% ya magari yenye namba B yaliyokuwepo Dar, hayapo tena kwa sasa kwa kuwa yamekwisha uzwa mikoani na takrabini 60% ya magari yenye namba C yaliyokuwepo Dar hayapo tena kwa sasa kwa kuwa yamekwisha uzwa mikoani.
aisee kumbe!
 
Hapana. Mfano kwa mtiririko huu wa sasa namba E, itaisha mwaka 2030! Namba ZZZZ itaisha baada ya miaka mia mbili ikiwa magari yataendelea kuingia kwa rate hii. Kwa hiyo gari yenye namba T999ZZZ itasajiliwa kwenye mwaka 2230!

Miaka 200 watakaokuwepo wataendelea kutumia pia.. mbona makanisa kama st joseph na azania front posta yamejengwa miaka zaidi ya 100 iliyopita.. ila watu vizazi vya leo wanaendelea kuyatumia kufanya ibada.

Usijiwazie wewe tu. Hata hizo herufi za namba sio lazima tuzimalize sisi wa kizazi hiki
 
Wewe unayenunua gari Kwa kuangalia namba ndio unapata tabu.Angalia Ubora wa gari Kwa kulikagua.
Mathalani mimi Niko Moshi, Huku gari # A ni misumari ya maana haina mkwaruzo hata wa sindano kwenye body,lakini # DV za Dar zimeshaongezeka uzito Kwa kupigwa puti.

Mfano unauziwa gari #DW na Kumbe imetoka Zanzibar ww unaona Iko nzima maana Unaangalia #.Nunueni magari sio # za usajili
 
Kuna kitu kinaitwa market saturation. Kwa hiyo hata kama tunaongezeka, kasi ya uagizwaji wa magari yaweza kupungua kwa kuwa tayari wengi wanayo.
Naelewa lakini sio sasa. Si unaskia meli imevunja rekodi kwa kuingiza magari mengi hivi karibuni. Bado hatujafikia kiwango hicho.
 
Wewe unayenunua gari Kwa kuangalia namba ndio unapata tabu.Angalia Ubora wa gari Kwa kulikagua.
Mathalani mimi Niko Moshi, Huku gari # A ni misumari ya maana haina mkwaruzo hata wa sindano kwenye body,lakini # DV za Dar zimeshaongezeka uzito Kwa kupigwa puti.

Mfano unauziwa gari #DW na Kumbe imetoka Zanzibar ww unaona Iko nzima maana Unaangalia #.Nunueni magari sio # za usajili
Hapo hatuja kagua mashine ikoje bado
 
Alafu ujue huyu dada anatuchukulia wa mikoani warugaruga laiti ungejua tunajua zaidi kuliko wa mjini. Kama hapo Moshi hakuna spare unakosa. Wengine tunaele hadi tunaleta 0 km gari mpya kabisa.
 
Back
Top Bottom