Ifike wakati hata nyinyi majirani muwe na akili timamu vichwani mwenu. Kwa Askari Polisi yoyote yule anayekuja kumkamata mtu kwa utaratibu kama huo ulioeleza huyo atakuwa ni Mhalifu, wala siyo Askari Polisi. Utaratibu wa kukamata Watuhumiwa upo wazi umeelezwa ktk Sheria za nchi.
Majirani mlipaswa kutoa ushirikiano kwa Mwananchi mwenzenu, mlipaswa kumkabili vilivyo huyo Askari Polisi kwa sababu alikuwa ni mhalifu kama Wahalifu wengine, ni jambazi au mtekaji.
But all in all, Sheria za Umiliki wa Silaha hapa Tanzania zinatakiwa kubadilishwa, kumiliki bunduki iwe iwe ni HAKI ya kila raia mwenye akili timamu hapa nchini.