Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
MH MAGUFULI AENDE PEKEE YAKE, AMEJIONGEZEA SIFA NYINGINE YA KUIONGOZA NCHI KUFIKIA UCHUMI WA KATI.
Na Elius Ndabila (Lali Ibaba).
0768239284
Jana nikiwa jijini kwetu, nilisoma twitter ya Mh Rais akitupongeza na kutushukuru Watanzania kwa nchi yetu kutangazwa kuwa kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa kati. Nilipoona twitter ile nilijihisi ninaota ndoto, hasa nikizingatia dira ya nchi tulikuwa tuna matarajio ya kufika huko miaka ya 2025.
Ninakumbuka tuliambiwa na viongozi wetu kuwa kati ya malengo makuu ya Tanzania kiuchumi ni kuwa nchi ya uchumi wa kati. Azma hii imeelezwa sehemu mbalimbali kama vile katika Dira ya Maendeleo 2025. Chini ya lengo la kuwa na uchumi imara wenye ushindani.
Inawezekana kuwa baadhi yetu hatukuelewi tunakwenda kwenye uchumi wa kati tukitokea kwenye uchumi upi? Lakini tukiwa tunajiuliza maswali haya ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa kwenye uchumi wa chini.
Uchumi huu ulizijumuisha nchi zenye kipato cha wastani kwa kila mtu cha Dola za Marekani 1,025 (wastani wa Shilingi 2,194,000) au chini ya hapo kwa mwaka kwa takwimu za mwaka 2015.
Ukisoma kwenye ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia mwaka 2015 kuna nchi 31 katika kundi hili la nchi zenye uchumi wa chini.Pamoja na Tanzania, nyingine ni kama vile Afghanistan, Burundi, Congo, Ethiopia, Liberia, Malawi, Msumbiji, Nepal, Somalia, Zimabwe, Uganda na kadhalika.
Katika juhudi za kuelekea uchumi wa kati ni muhimu kwa wadau wote kuelewa huu uchumi ni wa namna gani na nini kinatakiwa kuufikia. Jambo la kwanza kabla ya haja zote, Taifa linapaswa kujanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo ambacho ndicho kinaweza kusababisha kuwepo kwa mapinduzi ya kilimo. Kilimo kikisimamiwa vizuri ni rahisi kutoa matokeo chanya pale mazao yanapoanza kuchakatwa na kutenenezewa munyororo wa thamani.
Nimesoma katika marejeo mbali mbali nikatambua kwamba hata uchumi wa kati umegawanyika katika makundi makuu mawili.
Haya yameainishwa kwenye benki ya Dunia. La kwanza ni lile la uchumi wa kati wa ngazi ya chini na la pili ni uchumi wa kati wa ngazi ya juu.
Huu ni uchumi ambapo wastani wa kipato cha kila mtu kwa mwaka ni kati ya Dola za Marekani 1,026 na 4,035, yaani wastani wa kati ya Shilingi 2,195,640 na Shilingi 8,634,900.
Nchi zilizopo katika kundi hili ni 51. Hizi ni pamoja na India, Ghana, Indonesia, Morocco, Sudan, Tunisia, Pakistani, Bangladesh, Kosovo, Lesotho, Misri, Kenya, Nigeria, Zambia, Syria na kadhalika.
Jambo kubwa la kupongezwa ni kuwa Tanzania tulikuwa na ndoto ya kufikia uchumi huu mwaka 2015 ambayo yalikuwa ni malengo yetu kwenye mipango ya millenium. Lakini mwamba JPM miaka mitano kabla ameshafika.
Wakati nafikiria hili nimejiuliza kuna mtu wa kusimama na JPM 2020 Mwenye akili timamu? Atakaye simama anataka akatutoe Kanani aturudishe Misiri? CCM wamefanya uungwana kumuachia JPM kuendelea kutuvusha, ni matumaini hata vyama vya upinzani waliokuwa wanafikiria fikiria kusimamisha wagombea wa Urais wapige mahesabu kama watapata kura. Ni vema wakahamishia Majeshi huku chini kwenye udiwani na ubunge ili wamwachie JPM aendelee kuijenga nchi.
Mimi siyo mchumi, lakini ukiangalia kwa jicho la kawaida lisilo la kiuchumi hadi kufikia miaka 2020 inawezekana JPM atakuwa ametupeleka Mbali mno. Tuendelee kumuombea ili Mungu azidi kumpa nguvu na ujasiri katika kusimamia maslahi ya nchi. Tanzania imeandika historia kubwa!