Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Tulikuwa na Mr Clean kwa miaka 5 ya kwanza. Miaka 5 iliyofuata hata hatujui tusema alikuwa Mr nani
Tukawa na Ari mpya miaka 5 ya mwanzo, mwisho wa siku ndiyo haya ya makontena

Kama tunaweza kufanya analysis kwa kutumia siku 25 na ku project kwa miaka 5 tutakuwa na takwimu zetu duniani

Ngoja kamati kuu na NEC zikae kitako kuangalia jinsi anavyogusa 'maeneo' muhimu ya shughuli za watu

By the way, Nyani Ngabu kauliza intriguing question, tunahitaji uchaguzi kwa mwendo ulioonekana?

Kwa kweli hii mihemuko tunayoishuhudia mimi inanishangaza sana.

Inadhihirisha jinsi Watanzania tulivyo watu wasahaulifu na wepesi wa kuchotwa akili kirahisi rahisi.

Lakini nadhani hayo yote ni matokeo ya kuwa 'deprived' kwa muda mrefu sana.
 
Utaendelea kutawaliwa na CCM mpaka mwisho wa maisha yako.

Teh teh teh
Kutawaliwa na CCM wala sio shida! Shida isiwe inaongozwa na mtu wa dizaini ya Kikwete! Magufuli akiendelea na nguvu aliyoanza nayo wala mimi sina shida! Kikwete alikuwa amefanya ikulu kama pango... ndio ilikuwa shida yangu
 
Uchaguzi ni kupoteza pesa tu, hela za uchaguzi tuzitumie kujenga madarasa na nyumba za walimu nchi nzima.
 
Kutawaliwa na CCM wala sio shida! Shida isiwe inaongozwa na mtu wa dizaini ya Kikwete! Magufuli akiendelea na nguvu aliyoanza nayo wala mimi sina shida! Kikwete alikuwa amefanya ikulu kama pango... ndio ilikuwa shida yangu
Safi sana kama umejisalimisha CCM.
 
Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?

hilo swali Nyani Ngabu very controversial, curious, food of thought, school of thought, intriguing and thoughtful in a big way. ukawa must work hard to answer that question before the polls are open in 2020 otherwise no one will show up to vote again.
 
Hata hiyo 2025 tutamuomba atuchagulie wa kumrithi tu baaasi anaanza kazi, hatutaki kupoteza pesa eti kuchagua rais
 
Pasco,
Kwanza nikiri wazi kwamba huwa naheshimu sana maoni ya watu. Pili huwa nafuatilia na kuvutiwa na hoja zako nyingi hapa jukwaani! Ila niseme ukweli leo umeongea kijinga sana kwenye hii hoja! Nasema kijinga kwa sababu bado unaweza kujielimisha,kuelimishwa na ujinga wako ukaondoka!
Tanzania hatufanyi uchaguzi eti kwa sababu Nchi haina uongozi mzuri ama kwa sababu hakuna kiongozi shupavu. Mpaka sasa anachokifanya magufuli sio kitu kigeni,kiliwahi kufanywa huko nyuma na waliomtangulia lkn bado tulilazimika kuingia ktk uchaguzi! Tulikuwa tunafanya uchaguzi tukiwa na mfumo wa chama kimoja, leo tunao mfumo wa vyama vingi unakuja na mawazo ya kijinga namna hii?
Kati ya wakati huu na wakati wa uongozi wa Mwl Nyerere ni wakati upi ulikuwa muafaka wa kufuta uchaguzi?
Mawazo yako nayaona kama ni matokeo ya athari za uongozi mbovu wa CCM ya baada ya Mwl Nyerere! Watu walikuwa wamepoteza aina ya uongozi shupavu wa Nchi unavyopaswa kuwa! Leo Magufuli anaoneka kama katoka peponi!
Pasco umesahau kwamba Magufuli anatoka katika mfumo ule ule ulioyalea matatizo tuliyonayo? Hivi sio Rais wetu huyu aliyekuwa anasimamia Wizara iliyokuwa inanunua vivuko vibovu? Umesahau nini? Nashauri tusijisahu.
Unafahamu kwamba kwenye dunia hii kuna Nchi hazijui maana ya ufisadi,hazijui watu wanaokwepa kodi,hazijui kama kuna watu wanaolala chini hospitalini, hazijui kama kuna sehemu watu wanashindia mlo mmoja kwa siku, hazijui kama kuna watoto wanakaa chini shuleni n.k, lkn bado Nchi hizo zinafanya uchaguzi kama takwa muhimu katika kukuza Demokrasia na kuleta Maendeleo ya kweli katika Nchi zao?
Tanzania tuna nini cha kujivunia mpaka sasa? Dakika 10 tu za Magufuli Ikulu watu mnakuja na mawazo ya kutaka tuondoe uchaguzi wa Rais?
Umeandika hoja zako ukiwa na akili timamu ama una mihemko ya kutoujua ukweli?
Umefanya makusudi ama ndo akili yako imekuongoza hivyo leo? Siamini kama ni wewe!
Tanzania Tunaizidi nini Nchi ya Norway? Tunawazidi nini Denmark? Hizi ni Nchi zilizo na kila kitu anachohitaji kuwa nacho Raia katika Nchi yake! Ni Nchi ambazo hazina ujinga wa ufisadi! Mpaka sasa wao wanatupatia misaada kibao lkn still wanafanya uchaguzi kila inapofika wakati!
Sisi tuna nini?
Jisahihishe uache ujinga!
Tumpongeze Rais Magufuli kwa kufanya kile walichoshindwa kukifanya wengine, hata kama nae alikuwa sehemu ya uongozi mbovu uliopita, lkn tuache mawazo ya kijinga na hatari kwa ustawi wa Nchi yetu!
 
Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?

Hili ndilo swali la msingi......na ni mapema mno kusema chochote kwa sasa kwa sababu huwa wanaingia hivyo hivyo.........kwangu bado sana........sijaona kipya mpaka sasa.......zaidi ya upepo wa kisulisuli usiokuwa na direction........
 
Pasco ni mapema mno kuwaza haya.

Tumpongeze kwa kiasi fulani lakini pia tusisahau kuweka akiba ya maneno.
 
Last edited by a moderator:
Safi sana kama umejisalimisha CCM.

KAMA atafanya vizuri mimi sina shida kuiunga mkono CCM! Mimi sina chama ila ninataka uongozi mzuri! Naona mnatumia nguvu nyingi sana kumsifu Magufuli japo bado hajafanya chochote kipya. Mtaweza kucheza na bongo za wabongolala ambao hawana kumbukumbu. Alikuwepo Mrema na alitingisha kuliko Magufuli mara kumi... lakini uongozi wa kutegemea mtu badala ya mfumo haudumu na haubadilishi chochote!
 
Huwa nikiona comment za kuibiwa kura huwa nacheka sana...maana nakumbuka Lowasa aliwambia wapige kura kazi ya kulinda amwachie...!
Haikutosha makamanda walimsajili mtu aliye wadanganya kuwa yeye ni mtaalam wa kuiba kura lakini wapi...!
 
Rais JPJM ni mchapakazi sana na anatufaa sana, ila ni kosa kubwa kudhani kwamba akina Magufuli wengine wameisha au kudhani kuwa hakuna wa kuweza kumzidi Magufuli katika utendaji iwe ndani ya chama tawala au nje
 
attachment.php

tutaheshimiana tu!
 
Attachments

  • ukawa.jpg
    ukawa.jpg
    38.8 KB · Views: 312
Pasco,
Kwanza nikiri wazi kwamba huwa naheshimu sana maoni ya watu. Pili huwa nafuatilia na kuvutiwa na hoja zako nyingi hapa jukwaani! Ila niseme ukweli leo umeongea kijinga sana kwenye hii hoja! Nasema kijinga kwa sababu bado unaweza kujielimisha,kuelimishwa na ujinga wako ukaondoka!
Tanzania hatufanyi uchaguzi eti kwa sababu Nchi haina uongozi mzuri ama kwa sababu hakuna kiongozi shupavu. Mpaka sasa anachokifanya magufuli sio kitu kigeni,kiliwahi kufanywa huko nyuma na waliomtangulia lkn bado tulilazimika kuingia ktk uchaguzi! Tulikuwa tunafanya uchaguzi tukiwa na mfumo wa chama kimoja, leo tunao mfumo wa vyama vingi unakuja na mawazo ya kijinga namna hii?
Kati ya wakati huu na wakati wa uongozi wa Mwl Nyerere ni wakati upi ulikuwa muafaka wa kufuta uchaguzi?
Mawazo yako nayaona kama ni matokeo ya athari za uongozi mbovu wa CCM ya baada ya Mwl Nyerere! Watu walikuwa wamepoteza aina ya uongozi shupavu wa Nchi unavyopaswa kuwa! Leo Magufuli anaoneka kama katoka peponi!
Pasco umesahau kwamba Magufuli anatoka katika mfumo ule ule ulioyalea matatizo tuliyonayo? Hivi sio Rais wetu huyu aliyekuwa anasimamia Wizara iliyokuwa inanunua vivuko vibovu? Umesahau nini? Nashauri tusijisahu.
Unafahamu kwamba kwenye dunia hii kuna Nchi hazijui maana ya ufisadi,hazijui watu wanaokwepa kodi,hazijui kama kuna watu wanaolala chini hospitalini, hazijui kama kuna sehemu watu wanashindia mlo mmoja kwa siku, hazijui kama kuna watoto wanakaa chini shuleni n.k, lkn bado Nchi hizo zinafanya uchaguzi kama takwa muhimu katika kukuza Demokrasia na kuleta Maendeleo ya kweli katika Nchi zao?
Tanzania tuna nini cha kujivunia mpaka sasa? Dakika 10 tu za Magufuli Ikulu watu mnakuja na mawazo ya kutaka tuondoe uchaguzi wa Rais?
Umeandika hoja zako ukiwa na akili timamu ama una mihemko ya kutoujua ukweli?
Umefanya makusudi ama ndo akili yako imekuongoza hivyo leo? Siamini kama ni wewe!
Tanzania Tunaizidi nini Nchi ya Norway? Tunawazidi nini Denmark? Hizi ni Nchi zilizo na kila kitu anachohitaji kuwa nacho Raia katika Nchi yake! Ni Nchi ambazo hazina ujinga wa ufisadi! Mpaka sasa wao wanatupatia misaada kibao lkn still wanafanya uchaguzi kila inapofika wakati!
Sisi tuna nini?
Jisahihishe uache ujinga!
Tumpongeze Rais Magufuli kwa kufanya kile walichoshindwa kukifanya wengine, hata kama nae alikuwa sehemu ya uongozi mbovu uliopita, lkn tuache mawazo ya kijinga na hatari kwa ustawi wa Nchi yetu!

Asante mkuu
 
Back
Top Bottom